Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
USIWE ADUI WA MAFANIKIO YA WATU WENGINE
Sisi binadamu ni vigumu kuona matatizo yetu, ila ya wenzetu huwa tunayaona haraka sana.
Kwa mfano watu wawili wakigombana na kila mmoja akaja kukueleza ugomvi ule kwa wakati wake mwenyewe, kila mtu ataonesha kwamba mwenzake ndio ana makosa. Lakini ukweli ni kwamba mpaka watu wawili wanafikia kugombana, kila mtu kati yao anakuwa amechangia tatizo linalopelekea kugombana.
Tutalijadili zaidi hili wakati mwingine.Tukirudi kwenye kuua ndoto, ni rahisi sana kusema umekatishwa tamaa, umerudishwa nyuma na mengine mengi. Lakini na wewe upo kwenye jamii hii hii ambayo unarudisha watu nyuma na kuwakatisha tamaa.
Hii ikiwa na maana kwamba na wewe umeshakatisha wengi tamaa.Huenda kuna maneno umekuwa unaongea tu kwa watu, kwa kujua au kutokujua lakini ukawa umewakatisha tamaa na kuwarudisha nyuma.
Huenda ukawa hujui kwa sababu ndivyo umezoea kuishi, kwa kupinga kila kitu ambacho hukijui na kuona hakiwezekani. Kwa hilo tu umeua ndoto za watu wengi sana.
Umekuwa adui mkubwa wa watu kufanya mambo makubwa kwenye maisha yao.
Na kama jamii imekupa heshima ya tofauti, kutokana na umri au nafasi fulani uliyonayo, basi ndio unaweza kuwa sumu kubwa zaidi.
Kadiri jamii inavyokuchukuli
a juu ndivyo sumu yako inavyoweza kuwaharibu wengi zaidi.Kuepuka wewe kuwa sumu, kuepuka wewe kuwa adui wa mafanikio ya wengine na kuepuka kuwa muuaji wa ndoto, jiwekee azimio hili;
NITAONGEA KITU KIZURI NA KAMA SINA KIZURI CHA KUONGEA NITAKAA KIMYA.
Unapojiwekea azimio hili unajizuia kuongea maneno yanayokujia tu bila ya kujali yana athari kiasi gani kwa yule anayeyapokea.Sema kitu kizuri, ushauri mzuri, kutoa moyo au kaa kimya.
Lakini vipi kama mtu anaweka mipango ambayo unaona kabisa haiwezekani?
Kwa mfano mtu anakuja na kukuambia ndani ya mwaka mmoja ujao lazima nitakuwa bilionea, hapo ukimwangalia ni kijana ambaye hana kazi na hana mpango wowote wa kufanya kitu cha tofauti.
Mtu kama huyu humwambii haiwezekani, baliunamwelewesha ana lengo zuri na kubwa, ila kabla hajalifikia kuna hatua nyingi ambazo anahitaji kupitia na zitahitaji muda zaidi ya aliopanga, hivyo aanze na hatua zile za msingi na huko kwingine mambo yatakwenda vizuri.
Kwa njia hii unampa moyo na hata pa kuanzia kuliko kumwambia acha kuota vitu ambavyo haviwezekani, huwezi kuwa bilionea wewe, unaanzia wapi, kwa njia gani na maneno mengine kama hayo.
Kuwa na kitu kizuri cha kusema au kaa kimya.
Haijalishi mtu kasema kitu cha hovyo kiasi gani, jivue kazi ya uhakimu wewe na mpe mwongozo ambao unaweza kumsaidia yeye mwenyewe akafikiri na kuboresha zaidi.
Usiwe adui wa mafanikio ya wengine, usiwe muuaji wa ndoto kubwa za wengine.

Last edited by a moderator: