Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,281
- 79,888
USITISHWE NA JINA LA M/WASHINDANI WAKO.
Kwa Mkono wa Robert Heriel
Leo nitazungumzia suala muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku ambalo ni Jina la Mshindani/washindani wako.
Makala hii inafaa kwa matumizi ya watu wa rika zote kuanzia mtoto mdogo mpaka mzee kabisa. Makala hii inalenga kukupa ari na ujasiri wa kushinda katika mashindano yoyote yale iwe mashindano ya kielimu, kiimani, kijeshi, kiuchumi, kisiasa, kisanaa, kimahusiano, kiutamaduni miongoni mwa mashindano mengine. Nitajitahidi kutumia lugha rahisi kufanya kila mtu aelewe.
Maisha ni mashindano kwa sehemu kubwa ingawaje kuna wakati maisha yanakuwa vita kamili. Ili maisha yasijawe na chuki basi inabidi yachukuliwe kama mashindano au mchezo fulani ambapo kuna mshindi na mshindwa. Mashindano yananoga zaidi pale kauli ya asiyekubali kushindwa sio mshindani ikitumika na kueleweka kwa washindani.
Kwenye mashindano kuna Washindani, uwezo wao, mbinu zao, silaha zao, muda wa mapambano, uwanja wa mapambano, washabiki na wafuasi wao na sababu ya kupambana. Hivyo kabla hujaingia kwenye mashindano lazima mambo hayo uyafahamu.
Leo tutajadili suala la jina la mshindani wako.
Kwenye mashindano kila mshindani ana jina lake, linaweza kuwa jina kubwa, mashuhuri na maarufu au lisiwe. Mshindani wako anaweza akakushinda kuwa na jina kubwa, na kama utaleta mchezo jina tuu linaweza kukufanya ushindwe katika pambano akakupiga mpaka ukachanganyikiwa.
Wakati ninasoma tangu shule ya msingi mpaka sekondari (O'Level na A'Level) wapo wanafunzi wenzangu walikuwa na majina makubwa katika mashindano yale ya elimu. Wapo ambao majina yao yalitokana na kujua lugha ya kingereza zaidi kuliko wengine hali iliyowafanya waheshimike pale wanapokuwa wanajibu maswali ndani ya Darasa, au wanapoongea Morning Speech au wakati wa Debate/midahalo ya shule ya kingereza.
Wengine walijenga majina yao kwa sababu walikuwa wanaenda Dar es salaam kusoma Tuition kwa kina Mzilikazi, Mchikichini hivyo walikuwa wapo mbele yetu kwenye topics za masomo. Hali hiyo iliwafanya wakaheshimika na kujenga majina yao hasa kwenye mitihani ya shule ya ndani.
Wengine walijenga majina yao kwa sababu walikuwa na dhana za kujifunzia/ materials kama vitini, vitabu na past-paper hali iliyowafanya wakariri maswali karibu yote, hivyo wakati wa mitihani ya shule ya ndani ikija wanafaulu kutokana na kuwa waalimu wengi hu-copy na ku-paste maswali kutoka kwenye vitini, vitabu au past- paper.
Wengine wana jina kutokana na wazazi wao kuwa cheo au wadhifa fulani katika jamii.
Sisi wenzangu tusio na majina tulipuuzwa, na ilikuwa halali kupuuzwa kwa sababu, Tution hatujawahi kusoma, materials kama vitini, vitabu na past paper hatukuwa navyo, Kingereza nacho kilikuwa patashika nguo kuchanika. Kwa nini usipuuzwe. Huna jina wewe.
Paper ya mwanafunzi mwenye jina shuleni inaposhikwa na mwalimu asahihishapo ni tofauti na akishika paper ya mwanafunzi asiye na jina. Ni rahisi kumkosesha mwanafunzi asiye na jina kuliko kumkosesha mwanafunzi mwenye jina.
Kitu ambacho nilijifunza ni kuwa USITISHWE NA JINA LA WASHINDANI WAKO. Mbali na kuwa sikuwa na jina lakini nilidhamiria kushinda katika mitihani yangu hasa ile mitihani ya mwisho ambayo ndio inamvusha mtu kwenda daraja jingine.
Usiwekeze kwenye Jina lako uwapo kwenye mashindano, bali wekeza kwenye uwezo wako, mbinu na mikakati ya namna ya kuwashinda washindani wako. Usipende kupoteza muda kwenye mechi zisizo na faida kwani utapata sifa zisizo na faida. Hujawahi kusikia kuwa mwanafunzi anaongoza tangu kidato cha kwanza alafu mtihani wa mwisho anafeli, pengine uliwahi kusikia au kuona hiyo.
Wengi hutishwa na majina ya washindani wao, usiwe mmoja wa watu watishwao na majina ya watu hasa uwapo katika mapambano.
Nilipokuwa nasoma niliazimia kuwa lazima mtihani wa mwisho niwe mshindi yaani nichukue kikombe licha ya kuwa tangu nasoma shule ya msingi mpaka kidato cha tatu sikuwahi kushika nafasi ya kwanza. Mungu akabariki mtihani wa mwisho wa kidato cha nne niliongoza darasa kiufaulu nikiacha wengine wakinishangaa hasa wale wasionijua vizuri.
Kidato cha sita nilisoma na watu wenye majina makubwa, waliosoma shule za vipaji na wenye uzoefu wa kukaa bweni, waliosomea shule za seminari na English medium, wanafunzi wenye nyenzo zote za ufaulu, lakini mtihani wa mwisho wa kidato cha sita tuliopata daraja la kwanza tulikuwa saba nikiwa mmoja wao.
Sisemi najisifu bali najaribu kukupa ari na ujasiri wa kupambana na kupata ushindi uwapo kwenye mapambano ya aina yoyote. Mimi sikuwahi kusoma Tuition, sikuwa na materials, familia yetu ni masikini lakini haikuwa sababu ya mimi kushindwa. Shule niliyosoma haikuwa inafaulisha wanafunzi wengi, wakizidi sana ni wanafunzi watano au saba ipo miaka shule yetu ilikuwa haifaulishi hata mtu mmoja. Alafu mimi sikuwahi kushika hata nafasi ya tisa labda kumi au kumi na moja. Nafikiri unaweza piga picha hapo.
Kingine wazazi ni muhimu sana kuwatia moyo watoto, mtoto anapokuambia kuwa atafaulu mtie moyo sio umkatishe tamaa. Mimi wakati nikiwa nawaambia wazazi na walezi wangu kuwa nitafaulu kidato cha nne walikuwa wakicheka wakiona kuwa ninaongea kama mtoto mdogo nisiyeweza kufikiri vizuri, waliona ni jambo lisilowezekana, walikuwa na sababu ya kusema hivyo na wala hawakunikatisha tamaa bali walinipa kazi ya kuwathibitishia maneno yangu.
Nimetumia mfano wangu mwenyewe ili kukufanya unielewe vyema lakini kama hutonielewa basi acha nitoe mifano mingine sasa.
Miaka ya 2007 /2008 Wasanii waliokuwa wanatamba miaka hiyo alikuwepo Ali Kiba, Marlaw, Dully Sykes, Mr. Blue, Rich Mavoko, Bob Junior, Matonya na wengineo. Wasanii hao ndio walikuwa na majina makubwa, watu mashuhuri ambao kuwang'oa katika nafasi zao ilikuwa mbinde lazima unye mavi. Kuna wakati ilikuwa kama haiwezekani. Kipindi hicho Diamond Platnum alikuwa mgonga urimbo, Apeche Alolo wa jana wa leo. Alikuwa hana lolote.
Diamond Platnum hakutishwa na washindani wake wenye majina makubwa na wenye uwezo na connection ya kutosha yeye akiwa dhoofu ilhali. Diamond kapigana, kapasuana na sasa hakuna asiyemjua Diamond isipokuwa yule asiyefuatilia muziki. Diamond ni mfano bora katika mashindano ya Muziki ambapo hakuogopa majina ya washindani aliowakuta.
Diamond yule aliyeitwa Domo zege, leo hii ni sukari ya warembo ambao wanaliona domo lile lile kubwa kuwa ni lips denda.
Kama hujaelewa bado, basi nikupe mfano mwingine.
Mwaka 2015 Mhe Magufuli hakuwa lolote wala sio chochote kwenye mashindano ya kisiasa hapa nchini. Pengine nawe uliwahi sikia mahali(inaweza kuwa kweli au sio kweli) kuwa Magufuli aliwahi kuambiwa na kigogo fulani mfanyabiashara mkubwa kuwa "haongei na mbwa bali anaongea na mfuga mbwa" kipindi hiko Kikwete ndiye Rais, kumaanisha Mhe. Magufuli alichukuliwa kama Mbwa na Mhe. Kikwete akichukuliwa mfugaji wa mbwa.
2015 Mhe. Magufuli alishindana na watu wazito akiwemo Lowasa na Membe ambao kwa kipindi hicho walikuwa na majina makubwa
Hakuna aliyedhania kuwa Magufuli angekuwa Rais wa Taifa hili, matokeo yalivyotoka Magufuli aliwagaragaza washindani wake wenye majina makubwa na yeye kuibuka mshindi.
Katika pambano la Goliathi na Daudi. Goliathi alikuwa na jina kubwa, alikuwa mashuhuri, shujaa na jitu lililoogopwa lakini licha ya sifa kede kede alizokuwa nazo Goliath hazikumfanya Daudi amuogope, Daudi hakuogopa Jina la Goliath, Daudi alipaanga safu yake na wote tunajua kuwa Daudi alishinda mechi ile.
Kwenye maisha watu wengi hushindwa kwa kuogopa Majina ya watu, hushindwa kabla hawajaingia katika mapambano.
Usikubali ukatishwa na jina la mtu unaposhindana kwenye shindano lolote lile. Iwe ni shindano la kutafuta Mchumba/mke alafu mwanamke unayempenda ni potential kwa wanaume wengi hivyo wanaomtaka ni wengi. Usiogope kumpambania mwanamke/mwanaume unayempenda kisa wanaomfuata wana sifa na majina makubwa kukuzidi. Ingia vitani, pigana kiume kufa na kupona kumpata mke/mume mzuri umpendaye,
Kuna watu wanaogopa kuoa wanawake wazuri wanaowapenda kisa kuogopa ushindani, acha uboya, pambania kombe hilo.
Lazima uwe na attitude ya mshindi usiyeshindwa na yeyote bila kujali sifa za mshindani wako.
Kwa leo niishie hapa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro