Usitishwe na historia yako ya mahusiano

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
USITISHWE NA HISTORIA...

Historia ina athari mbaya kwenye mahusiano. Unaweza kuogopa kuanzisha mahusiano kwa sababu ya mikasa uliyowahi kukutana nayo. Unajikuta ukichukua tahadhari nyingi kupindukia na hata kuapa hutakaa uamini wanaume/wanawake.
Ni kama unaamini,
"Wanaume/wanawake wote lao moja..."
"Wanawake/wanaume wote ni matapeli. Hawafai"

Kuumizwa na wasaliti wawili watatu, kunakufanya ufikiri kila mwanaume/mwanamke duniani ni msaliti. Huamini kuwa watu wanaweza kuwa na uhusiano usio na mikasa.

Sikusudii kukushauri. Nakumegea sheria ya mahusiano. Tunavutia kinachofanana na sisi. Kwamba huenda kuna kitu fulani unacho [na pengine hukijui] lakini ndicho kinachovutia watu wenye tabia fulani usizozipenda.

"Inakuwaje kila nikizama kwenye mahusiano naibuka na matapeli?"
"Mbona mwanzoni wanakuwa-ga kama malaika [...] lakini baada ya muda wanakuwa mashetani?"
"Kwa nini huwa najikuta naachana na wapenzi kwa mikasa ya kutisha?"

FUNGUA MACHO. Kwanza samehe historia. Imepita na maumivu yake. Pili, na muhimu, JISAMEHE na uamue KUBADILIKA. Badilisha namna unavyoingia kwenye mahusiano. Badilisha vigezo vinavyoongoza mahusiano yako. Badiliko hilo litaanza KUVUTIA watu sahihi. Utashangaa badala ya kuvutia wanaume 'wakware', utaanza kuvutia wanaume wanaoaminika.

Nikuachie swali, unadhani labda unahitaji badiliko gani kwenye mfumo wa mahusiano yako? Huna breki ya mahusiano? Unatumia mwili kama silaha? Unatafuta wenye uwezo wa kifedha? Kipi hasa? Usipobadilika, ndugu yangu, hakuna kitakachobadilika. Inaanza na wewe
 
Siku tamu leo,lecture kila kona. Mapenzi ni kama chakula ukipata allergy ya chakula hiki huwezi chukia kile.

Utulivu unahitajika katika kufanya maamuzi sahihi.
 
Back
Top Bottom