Afande Manyota kaja Boston kutoka Bongo kwenye Mkutano Longwood Medical Center. Amefikia CHARLES HOTEL mjini Boston. Afande Manyota (AM) amempigia simu Chiku kumsalimia. Wanapanga Chiku Aende hotelini jioni waonane ili Afande ampe zawadi kutoka kwa shangazi yake Bongo.Chumbani kwa Akande Manyota Hotelini. Afande Manyota anamgojea Chiku kwa hamu. Chiku anabisha hodi mlangoni chumba (suite) namba 610:
Chiku: (Taratibu kwa sauti ndogo) Hodi!AM: Karibu!Afande Manyota anafungua mlango
.
AM Oh, Karibu, karibu sana
Chiku Asante (Chiku anashangaa Afande Manyota alivyo handsome futi sita, anaonekana kama ana misuli ya bondia)
AM- Kumbe wewe ndiye Chiku, oh karibu sana, nilikuwa na hamu sana ya kukuona. Shangazi yako kaniambia mengi juu yako.
Chiku Asante nimekaribia. Shangazi hajambo siyo.
AM- Hajambo, anakusalimia sana. Karibu kiti
Chiku Ahsante, Oh, chumba kizuri sana, kumbe hii hoteli safi sana
..
AM- Na hata mimi nimeipenda sana, chumba kikubwa
Chiku Bila shaka kuna Jacuzzi bafuni?
AM Haha, Jacuzzi ipo dada, unajuaje ulishawahi kufika hapa nini?
Chiku Unastarehe wewe
.. hata hii hoteli inajulikana kwa anasa zake
SOMA ZAIDI
VISA VYA DADA CHIKU