Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 39,741
- 92,197
USISAHAU MAMBO HAYA.
MWANDISHI. Robert Heriel.
HATIMILIKI@2019
TAIKON PUBLISHER.
Maandishi ya Robert Heriel Kwa Lugha ya Kiswahili.
UTANGULIZI
Kitabu hiki ni zawadi kwa watu wote. Kitabu hiki ni matokeo ya fikra zenye manufaa ambazo nataka kila mmoja wetu awe nazo. Maisha ni kama njia nyingi inayohitaji mpitaji. Mtu mmoja hawezi pita katika njia mbili kwa wakati mmoja.
Bali njia moja kwa wakati mmoja.
Kutokana na uwepo wa njia nyingi mpitaji huhitaji kuwa na kumbukumbu ili asijekupotea wakati wa kurudi au wakati wa kwenda. Hapo ndipo kitabu chetu cha
USISAHAU MAMBO HAYA kinapojitokeza na kupata maana kubwa kwetu.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa watu wa rika na hadhi zote. Hakibagui Umri wala hadhi ya mtu. Mtu yeyote anaweza kukitumia na kikamnufaisha.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili lakini kutokana na uwepo wa
lugha nyingi tutafanya tafsiri kwa lugha ya kingereza panapo majaliwa.
Ni matumaini yangu kuwa Kupitia kitabu hiki. Utakuwa umebarikiwa na kupata
mambo yatakayobadili maisha yako.
Kabla hatujaanza sura ya kwanza. Tusisahau Kumuomba mwenyezi Mungu aliyetupa nafasi hii muhimu katika maisjha yetu.
OMBI:
" Ushukuriwe wewe uishiye juu na chini. Juu kupita juu. Chini kupita chini.
Uishiye mahali tusikoweza kufika. Jina lako ndilo litupalo kuishi lihimidiwe.
Tunajua unatupenda. Tufanye tukupende kama unavyotupenda sisi. Kwa maana
tukikupenda tutashika maagizo yako.
Mungu wetu, tunaomba kitabu hiki cha USISAHAU MAMBO HAYA kigeuke baraka kwa kila atakaye kisoma. Kwa maana sio kwa utukufu wetu bali kwa
utukufu wako wewe uliyemkuu siku zote.
Mungu wetu, wewe ndiye uliyetupa maisha. Nasi kupitia wewe tunaishi. Bariki kila mmoja wetu kulingana na mapenzi yako. Nasi tunaomba utupe akili zenye
kukumbuka mambo unayotuagiza ikiwa ni pamoja na mambo nitakayoyaandika
humu.
Tunyime kila kitu katika hii dunia lakini usitunyime uso wako.
Ninaomba nikiamini katika Mungu Mmoja ambaye kupitia watumishi wake
tumemtambua. Amina"
USISAHAU
Njia tuliyojia ilikuwa ni nyembamba sana. Tena Bila ya msaada tusingefika hapa tulipo. Siku ile hatukuwa na nguvu yoyote. Tulikuwa tumefumba macho yetu
kwani kulikuwa na giza. Kwa maana macho huona kwenye mwanga. Kama kuna giza yafaa nini kuangalia. Basi ndio maana tulifumba macho yetu kwa kuwa
hapakuwa na mwanga. Wala hapakuwa na kitu cha kutazama.
Tulikuja tumekunja mikono yetu. Kwa maana mikono hukunjuka ikiwa kuna kitu cha kushika. Ikiwa kunakitu cha kupokea au kutoa mikono yetu hukunjuka. Lakini
hatukuwa na kitu cha kushika iweje tukunjue mikono yetu. Hatukuwa na kitu cha kupokea iweje tunyooshe mikono yetu. Hatukuwa na kitu cha Kutoa kwa maana hatukuwa tunamiliki jambo lolote. Ndio maana tulikuja hivyo. Halikadhalika
tutaondoka hivyo.
Basi usisahau yakuwa ulikuja katika njia nyembamba. Uishi kwa nidhamu na kwa unyenyekevu kwa maana kama ulivyokuja ndivyo utakavyoondoka.
Nawe hukuwa na nguvu yoyote ile lakini ukapewa nguvu. Tena hata nguvu hizo hazikukusaidia mpaka uliposaidiwa. Bila ya kusaidiwa usingefika hapo. Basi uishi kwa akili na hekima ili uzidi kufanikiwa.
Ulipokuwa tumboni mwa Mama yako. Ukakaa miezi tisa usiku na mchana. Ukila anachokula. Ukipumua anachopumua. Naye akakutoa katika njia nyembamba kwa
kukusukuma. Nawe bila ya kusukumwa usingeweza kutoka. Basi usisahau kuwa
Wapo waliokusukuma mpaka ukafika hapo.
Maisha ni msukumo. Bila msukumo hakuna maisha. Kila mmoja humsukuma mwenzake. Hakuna anayeweza kujisukuma mwenyewe akasogea mbele. Ndio
maana nalikupa mfano wa kuja kwako duniani kupitia njia nyembamba. Ambapo bila Mama yako kukusukuma usingekuja hapa duniani.
Basi usisahau watu waliokusukuma ukafika hapo ulipo. Usiwasahau wale wote waliokufikisha hapo. Waliokuleta duniani hao usiwasahau. Waliokulea hao
usiwasahau. Watu wote waliokusaidia kamwe usiwasahau.
Kwa maana watu hao ndio waliokutoa katika njia nyembamba ambayo ulishindwa kupita. Lakini wao walikupitisha kwa msukumo wa nguvu walizopewa, na Nguvu
iliyokuu naam ndio Mungu wetu.
Lakini pia usiwasahau wale wote waliokurudisha nyuma. Wale waliokuwekea Vikwazo. Hao utawakumbuka siku zote kama unavyowakumbuka waliokusaidia.
Ingawaje usilipe kisasi ikiwa hakuna sababu ya kufanya hivyo. Uwasamehe kwa maana kusamehe ndio kunakufanya uwe mtu hodari.
Usisahau kuwa ulitoka kwenye njia nyembamba.
Tena hukuwa na lugha mdomoni mwako. Wala hukuwa na mwendo miguuni mwako. Lakini wao ndio walikutia lugha mdomoni mwako ukajua kuongea na
kuwasiliana na watu wengine. Mpaka sasa unajua kuongea. Basi usisahau kuwa wapo waliokufundisha lugha mpaka sasa unaongea. Kamwe usitumie mdomo
wako kuwatukana matusi mabaya masikioni mwao. Wala usiwakejeli au kuwatolea maneno yanayoudhi. Kwa maana hao ndio waliokufunza lugha.
Tena usisahau hao ndio walikufundisha kutembea kwa miguu yako miwili. Na uliposhindwa walikubeba mgongoni. Basi utakapokuwa mkubwa usiwakimbie
wakihitaji msaada wako. Nawe utawatembea kila upatapo nafasi.
Kamwe usiwasahau watu hao. Kama walivyokubeba ulipokuwa huwezi kutembea. Nawe
uwabebe siku watakaposhindwa kutembea.
Usisahau kuwa nao walikuvumilia ulipokuwa huwezi lolote. Hujui lolote.
Walikuvumilia ulipokuwa unakosea. Basi nawe wavumilie pale watakapoonyesha
uhitaji wa uvumilivu. Usichoke kuwavumilia kwa maana wao hawakuchoka.
SURA YA 1.
UTAKAPOTOKA NYUMBANI KWENDA KUTAFUTA MAISHA. USISAHA
HAYA.
Kwa vile walitaka ujitegemee ndio maana walikufundisha kujitegemea.
Walikufundisha mambo yafuatayo;
●Lugha............................................................................
Kitabu hiki kinapatikana kwa bei ya shilingi 20,000/=
Ipo sura ya utakapojenga nyumba yako usisahau mambo haya.
Pata nakala yako.
Nipigie simu
06933223300
0711345431
Au niandikie humu robertheriel99@gmail.com
Au fika Ofisini kwetu Kihonda kanisani, Morogoro.