Bei Rahisi Electronics
Senior Member
- Apr 4, 2025
- 197
- 583
USIRI NI NGUZO YA MAFANIKIO.
__________________________________________________
Si muda wote unatakiwa kueleza dhamira yako kwa watu unatakiwa kujua kuwa adui wa mtu ni watu. Sio ajabu yule unaemjengea dhana njema ndio akawa ni adui wa siri kwako kwahiyo ni vyema kuwa msiri kwenye mambo muhimu yanayojenga ustawi wako. Maisha ni mfano wa vita kila mmoja anajiami aweze kuwa mshindi.
Maanguko ya watu wengi chanzo kikuu huwa ni kuwaamini watu ovyo ovyo bila kujua undani wao. Mionekano ya watu huwa inatuponza na kuona ni salama kwetu tukasahau kuwa vitu feki huwa vinapambwa zaidi ili kutafuta uhalisia wa original.
Jiamini wewe mwenyewe na yule ambae umejiridhisha moyoni mwako kuwa salama kwako. Dunia ilivyokubali mabadiliko sio ajabu kabisa hata mke au mume ndio akawa adui namba moja wa maisha yako. Wapo watu wasiokuwa na idadi kuanguka kwao kumesababishwa na watu wa karibu yao.
Sikufundishi kumchukia mwandani wako ila nakufundisha kuwa na tahadhari na watu kwasababu uchafu uliojaa leo kwenye dunia chanzo mama ni watu. Lisilolazimika kulisema hadharani basi jitahidi ulifiche kwasababu kutoa kila kitu kinachohusu maisha yako hadharani ni dalili ya upungufu wa akili.
Kusudi la mitandao ya kijamii sio kuonesha nyumba unayomiliki au mume uliekuwanae sasa hapana. Kusudi la mitandao ni daraja la kufahamu vitu vingi vyenye faida maishani mwako na kuonesha ukubwa wa kipawa chako ili kinufaishe wengine. Kuwa makini na unachoamua kwasababu maamuzi ya leo ndio matokeo ya kesho.