Usiri katika mahusiano!

Usiri katika mahusiano!

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,374
Reaction score
38,248
Usiri ni kitu hatari sana ktk Mahusiano!

Usiri uliopitiliza ktk mahusiano ni sumu mbaya sana, huwa inasubiri siku na wakati tu, ili iweze kusambaa na kuuwa ikibidi. Kama una kitu moyoni, na kinakukereketa, na upo ktk mahusiano ama mapenzi, sio vizuri kuvificha, na hasa kama vina uhusiano wa moja kwa moja na mahusiano ama penzi lenu!

Kuna ukweli, kuwa si kila kitu unaweza kumueleza mwenza wako, na hasa vile ambavyo ima havimuhusu ama havina mashiko na mahusiano yenu. Cha msingi hapa, ni kuwa kuna vitu kama utafanya siri, na vikadumu kuwa siri kwa muda mrefu, ipo siku vitafunguka na vitaleta rabsha, ugomvi na kutokuelewana miongoni mwa wahusika! Mf. kabla ya kuwa na yeye, uliwahi kuolewa ama kuoa, leo imepita miaka 3 ama mi5, anagundua profile yako huko nyuma, italeta mtafaruku sana! Ni kweli yaliyopita si ndwele, lkn usiri wako utaleta maswali mengi zaidi kuliko majibu!

Wengi wa watu walio ktk mahusiano ya kimapenzi, huumizwa sana wanapogundua kuwa mwenzi wake amemficha jambo fulani kwa kitambo kirefu! Hii huleta shida sana ktk utetezi. Madhara ya kuficha ficha mambo ktk mahusiano, humfanya aliejua hiyo siri:


  1. kuhisi unamtenga
  2. kuhisi km umemficha kwa jambo X, basi nyuma ya pazia kuna Y na Z ambazo pia ulishamficha!
  3. kuhisi kuwa una mipango yako binafsi ambayo itakuja kuwa na madhara kwake
  4. kuhisi amedharauliwa
  5. kuhisi humkubali kivile

Kama kuna kitu umemficha mwenza wako, na unakiri moyoni akija kujua tena kupitia njia zake binafsi, itamuuma ama kumtia hasira, tafadhali tafuta namna ya kumfikishia ujumbe! Ni kweli kuna "surprise" lakini sio kila surprise hupokelewa vizuri, je? umejiandaa kwa mapokezi mabaya ya surprise yako? Na ukweli mchungu ni kuwa, wengine wameumbwa kutoelewa wala kuthamini kinachoitwa "surprises!"

Kwa mfano: umenunua kitu, kizuri tu, tena kwa manufaa yenu kama wenza, let say - kiwanja, miezi 6 ama hata mwaka mmoja, hujamwambia, kisha anakuja kujua kwa jitihada zake binafsi, unajitetea kuwa ni "surprise", hapana, utakuwa umesababisha matatizo ambayo yalikuwa yanaepukika, kwanza surprise haiitaji mwezi mzima! hata 1 hr inatosha kumfanyia mchuchu wk surprise! kwa nini usubiri kipindi kirefu kipite!

Nakiri kuwa yapo mambo ktk mahusiano ni siri, na upo uwezekano wa kujitetea pindi yakifumuka, lkn tuwe tunaangalia na kupima FAIDA na HASARA za kuweka u-siri huo!

Nawatakia jioni njema!
 
usiri ni kitu hatari sana ktk mahusiano!

Usiri uliopitiliza ktk mahusiano ni sumu mbaya sana, huwa inasubiri siku na wakati tu, ili iweze kusambaa na kuuwa ikibidi. Kama una kitu moyoni, na kinakukereketa, na upo ktk mahusiano ama mapenzi, sio vizuri kuvificha, na hasa kama vina uhusiano wa moja kwa moja na mahusiano ama penzi lenu!

Kuna ukweli, kuwa si kila kitu unaweza kumueleza mwenza wako, na hasa vile ambavyo ima havimuhusu ama havina mashiko na mahusiano yenu. Cha msingi hapa, ni kuwa kuna vitu kama utafanya siri, na vikadumu kuwa siri kwa muda mrefu, ipo siku vitafunguka na vitaleta rabsha, ugomvi na kutokuelewana miongoni mwa wahusika! Mf. Kabla ya kuwa na yeye, uliwahi kuolewa ama kuoa, leo imepita miaka 3 ama mi5, anagundua profile yako huko nyuma, italeta mtafaruku sana! Ni kweli yaliyopita si ndwele, lkn usiri wako utaleta maswali mengi zaidi kuliko majibu!

Wengi wa watu walio ktk mahusiano ya kimapenzi, huumizwa sana wanapogundua kuwa mwenzi wake amemficha jambo fulani kwa kitambo kirefu! Hii huleta shida sana ktk utetezi. Madhara ya kuficha ficha mambo ktk mahusiano,
humfanya aliejua hiyo siri:



  1. kuhisi unamtenga
  2. kuhisi km umemficha kwa jambo x, basi nyuma ya pazia kuna y na z ambazo pia ulishamficha!
  3. kuhisi kuwa una mipango yako binafsi ambayo itakuja kuwa na madhara kwake
  4. kuhisi amedharauliwa
  5. kuhisi humkubali kivile

kama kuna kitu umemficha mwenza wako, na unakiri moyoni akija kujua tena kupitia njia zake binafsi, itamuuma ama kumtia hasira, tafadhali tafuta namna ya kumfikishia ujumbe! Ni kweli kuna "surprise" lakini sio kila surprise hupokelewa vizuri, je? Umejiandaa kwa mapokezi mabaya ya surprise yako? Na ukweli mchungu ni kuwa, wengine wameumbwa kutoelewa wala kuthamini kinachoitwa "surprises!"

kwa mfano: Umenunua kitu, kizuri tu, tena kwa manufaa yenu kama wenza, let say - kiwanja, miezi 6 ama hata mwaka mmoja, hujamwambia, kisha anakuja kujua kwa jitihada zake binafsi, unajitetea kuwa ni "surprise", hapana, utakuwa umesababisha matatizo ambayo yalikuwa yanaepukika, kwanza surprise haiitaji mwezi mzima! Hata 1 hr inatosha kumfanyia mchuchu wk surprise! Kwa nini usubiri kipindi kirefu kipite!

Nakiri kuwa yapo mambo ktk mahusiano ni siri, na upo uwezekano wa kujitetea pindi yakifumuka, lkn tuwe tunaangalia na kupima faida na hasara za kuweka u-siri huo!

Nawatakia jioni njema!
watu wana watoto na mpaka watoto wamekua na wakaoa bado mke hajui chezea siri ww labda niamue kusema mwenyewe siri waweza kuifanya ikawa siri kweli usicheze na siri,
 
kuhisi kama hakukubali vileeeeeeeeeee
 
Uwazi katika mahusiano hauji by default settings, ni jukumu la wote wawili kuutengeneza.

Ila...??!!!!
 
watu wana watoto na mpaka watoto wamekua na wakaoa bado mke hajui chezea siri ww labda niamue kusema mwenyewe siri waweza kuifanya ikawa siri kweli usicheze na siri,

hkn siri ya watu wawili kumbuka mkui
 
Back
Top Bottom