Usipoweza kupambana nao ungana nao

Usipoweza kupambana nao ungana nao

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,888
Reaction score
17,294
Tukiamini kuwa Tanzania hii ni ya kwetu sote hakuna haja ya kupambana ima fa ima hata kwa kutumia njia haramu ili kushinda. Kwa wananchi ambao ni wapenzi wa kwenda ulaya na Marekani kila mara wanafahamu namna wenzetu wanavyoendesha chaguzi zao. Wao uchaguzi sio kitu kinachoweza kuumiza au kutoa roho ya mtu wao, kwakuwa wao wanafahamu kuwa vyama vyote vinajenga nchi moja yenye dira moja lakini kwa njia tofauti.

Hata sisi hapa kama mgombea au chama kimezidiwa kwenye majukwaa tujenge utamaduni wa kukubali matokeo bila kulazimika kutafuta njia za pembeni za ushindi. Hizi njia za pembeni ndizo zitakuja kuligharibu taifa siku za mbeleni za vizazi vyetu, litakujakugeuka taifa la visasi kama vile kule Misri kwa akina Mubarak na Mossi.

Jambo la msingi ni kuungana na kutengeneza dira ya taifa na taasisi (katiba, jeshi, mahakama, bunge, NEC) ambazo kila atakayechaguliwa atakuwa na nafasi sawa na wengine ya kuchaguliwa, kuchaguliwa tena au kushindwa uchaguzi. Hapo tutalifanya taifa letu liwe na viwango vya kimataifa, na watu na rasilimali zao zitakuwa mbali kutoka kwa wezi wa kimataifa.

Kupambana na mtanzania mwenzio kwa matusi, kejeli, fedha, mabomu, ulangai, uwongo, wizi, n,k ili wewe lazima ushinde sio afya kwa taifa. Jiulize wewe nani hadi lazima ushinde?

Hela ngapi unahitaji kupewa ili ujue kuwa unahatarisha amani ya nchi?, utazikwa nazo? hutazeeka? familia yako hakuna siku itakujakuandamwa na vitendo vyako? maana tanzania haifi tunakufa sisi.
 
Jaji warioba aliliona Hilo Hata Ukasahau yaliyomkuta pale Ubungo plaza.

Ameungana na walioisibgina Rasim ya Katiba ya Wananchi. Aibu Makofi juu yake..
 
well spoken, tuwaulize hao maccm wanajiapiza kuwa lazima washinda katika uchaguzi wa mwaka huu hata kw goli la mkono, watambue Tanzania ni yetu sote na hakuna mwenye hati milki na nchi hii
 
Kwa hapa ni vigumu maana uongozi ni ajira inyolipa kuliko nyingine,kama mtu anaweza kujisevia noti kwa rumbesa na haguswi utamtoaje kwenye nafasi yake?
 
Unakuta mtu kwenye jukwaa hana lamaana, uadilifu ZERO, uchapakazi ZERO,sera HAZIELEWEKI, Kuteuliwa kwake HAKUJULIKANI , halafu watu wajipumbaze akili ooh tutashinda labda kushinda Hotelini mwenzie Anashinda IKULU, SICHAGUI CCM NAMCHAGUA MAGUFULI
 
Kwa hapa ni vigumu maana uongozi ni ajira inyolipa kuliko nyingine,kama mtu anaweza kujisevia noti kwa rumbesa na haguswi utamtoaje kwenye nafasi yake?
Hizo pesa nyingi za hivyo za nini sasa huku akijua kuwa anahitaji vijiko 20 tu vya ubwabwa kwa mlo na wakati huohuo magonjwa ya moyo, pressure, kisukari, mifupa, tezidume, macho na kanza vinamnyemelea huku watoto na wajukuu nao wakiadhirika kwa HIV na madawa ya kulevya kwa pesa hizohizo.
 
Ndg yangu wee acha siasa na ujinga wetu ndiyo mitaji yao unadhani pesa walizo nazo wangezipata wapi wasinge kimbilia kwenye siasa mf.kijana mdogo amemaliza juzi chuo kikuu leo hii tajiri kuliko wenzake aliomaliza nao chuo sababu ya siasa
 
Back
Top Bottom