Usipoona mfano, ipo wewe utaonwa mfano

Usipoona mfano, ipo wewe utaonwa mfano

Amani Dimile

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
243
Reaction score
399
Urembo ni hadithi ya muda mfupi, ukiusoma bila kujali wakati lazima muda utakuhukumu.

Je, umeamua kuwekeza kwenye nini, kwenye uzuri ambao haudumu. Fahamu ya kuwa ile miruzi na sifa njema nyingi zenye chombwezo la huba kuna wakati itakoma lakini maisha yatasonga. Au unataka kukumbushwa kuwa hata bibi alikuwa mwali?

Alisikika mmoja akisema "ukiona tunda limeiva, ujue hata kuoza limekaribia".

Kuna muda mchache sana kutoka kwenye ujana kwenda kwenye uzee, amua kufanya lililo sahihi.

Siongei pumba abadani

Labda, nikuulize tu yupo wapi yule Celine Dion wa zama zile, ambae alitawala dunia kwa uzuri wake na sauti yake nyororo.

Huyu ndio Celine Dion wa leo, hivi sasa yupo kitandani anaugulia maumivu mazito ya gonjwa hilo kali. Ukijihisi una nguvu basi tambua Muda una nguvu kuliko wewe. Zile Dimpozi za ujanani ndio zimekuwa makunyanzi ya uzeeni. Iko wapi ile sauti yake njema iliyokuwa nzuri sana kiasi kwamba unaweza ukala nayo ugali. Mungu anajua sana, akaamua kutofautisha uwezo wake na pesa .......... Ikiwa unaona mfano na huelewi, basi subiri uonwe mfano tuelewe

Anyway nisikuchoshe sana. Ila tambua baadhi ya mambo haya

1. Uzuri sio mtaji, tumia akili yako na ujikite kwenye malengo yako binafsi yenye manufaa zaidi. Ukitumia urembo kama kipato, basi muda utajidhihirisha ukuu wake kwako. Kumbuka hata biblia imesema mwanamke mzuri asie na akili, ni kama Pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe (Mithali 11:22)

2. Tamaa ya kutaka kufanikiwa haraka isikutawale kuliko uwezo wako halisi, utajikuta unapita njia zisizo salama. Matokeo yake utaishia kusema ningejua kipindi ambacho majuto ndio malipo yako halali.

3. Maisha ya watu wengine yasikupe msukumo wa kuwatamani, utajikuta unashindana na watu wenye historia ya familia tofauti na yako. Pia mafanikio ya watu wengine yasikufanye uumie kiasi kwamba uanze kuwachukia. Sisi sote ni tunda la aina moja kwenye mti mmoja, lakini kila tunda litaiva kwa wakati wake.

4. Si lazima kuendana na kila aina ya marafiki, si lazima kuendana na kila fashion. Baadhi ya style za maisha kubali tu zikupite, ni bora kuonekana mshamba kwenye mada za kipumbavu ili kutunza utu/thamani ya uwepo wako.

5. na mwisho

Mkumbuke sana Muumba wako, yeye ambae akitaka kitu hukiambia kuwa na hua (Quran Tukufu, surah Maryam 19). Mtegemee yeye, kuwa karibu nae atakusaidia. Zama za sasa za dhambi zinahitaji nguvu kubwa ya kiimani.

Ahsante kwa kunisikiliza, naitwa Amani Dimile

#amanidimile #misemo_ya_hekima #tungomaridadi #tusomevitabu #menarefrommarswomenarefromvenus #fikrazadimile

a945daa180f4-celine-dion-mental-health-t.jpg
 
Back
Top Bottom