Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,758
- 4,968
KILA MTU AMEUMBIWA KUFANIKIWA KWA NAMNA YAKE, KUFANIKIWA SIYO KUSHINDANA.
"Success is not competition"
Jamii yetu leo ni kama tumeaminishwa ili kufanikiwa sharti tushindane lakini Kanuni za uumbaji za asili hazioneshi umuhimu huo. Ni kama tumelipokea jambo ambalo tumelichukua kama imani katika maisha yetu lakini siyo kweli kuwa ni lazima kushindana ili kufanikiwa.
Tunapoingiza suala la kushindana "competitions" maana yake kuna anayeshinda na anayeshindwa lakini uumbaji haujawagawa watu katika makundi hayo. Uumbaji unatuonesha kuwa kila mmoja wetu ni mshindi wa aina yake ndiyo maana hayupo anayeweza kila kitu. Usichokiweza wewe anaweza mwingine na hii haimaanishi wewe siyo mshindi kwa sababu yapo uyawezayo haswaa.
Kila aliyeumbwa na Mungu amekuja Duniani kama mshindi. Vigezo vyote tunavyovitumia kuwagawa watu kama washindi au walioshindwa vina udhaifu mkubwa sana kwa sababu hayupo mshindi wa yote.
Kwa msingi huo "TUNAKAMILISHANA NA TUNATEGEMEANA" hayupo aliyekamilika kwa asilimia moja hata wale tunaowaona kama washindi. Tunapokamilishana wote kwa pamoja tunakuwa washindi ila kwa hakika kabisa hayupo mshindi mmoja peke yake.
Naandika andiko hili kwa sababu tupo wahanga wengi mno wa elimu hii potofu ya kuamini katika kushindana badala katika upekee na kukamilishana. Ni kama tumekubalianankuwa kila jambo sharti kushindana na kisha kupata makundi ya washindi na walioshindwa.
Tunachopaswa kujua kabla ya kushinda au kushindwa kinachotangulia ni kuamini tu. Kuamini katika kushindwa kunaruhusu ukubalifu wa kushindwa na ndivyo ilivyo. Halikadhalika, kushinda nako hutanguliwa na kuamini hivyo.
Akili ya Mwanadamu ina utata mkubwa sana katika kuamini. Kwa mfano hata kile unachokiamini sana katika maisha yako kikikutokea leo bado akili yako itatia mashaka. Swali la kujiuliza ni kwa nini tuendelee kukaa katika kuamini mafundisho haya potofu?..(don't waste your time)
Ushauri wangu, tujatibu kufanya kwa dhati (be committed) juu ya yale tuyafanyayo na kuacha kujikita katika kuamini kila tunachojifunza.
...................................................................................................................
Usimfundishe mwanao uongo uleule uliofundishwa.