Wanawake wengi kwenye ndoa au mahusiano hujisikia na kujiona hawapendwi na waume zao, hujisikia wanaume hawawajali, ukiangalia kwa undani moja ya sababu ni mwanaume ameacha kumpa zawadi hata ndogondogo, au maneno mazuri (
notes) au kadi kama alivyokuwa anafanya mwanzo na kwa sababu ulikuwa unampa na ueacha anajiona humpendi tena, si ulikuwa unampa? sasa imekuwaje? unampelekea nani tena? maana ulikuwa na tabia ya kutoa zawadi.
Kiwango cha attention unayompa mke wako ni alama muhimu ya Kuonesha upendo wako kwake.
Mwanamke hujisikia anapendwa na kwamba unamjali pale mwanaume:-
Unampompa zawadi iwe ndo au kubwa,
Unapompa zawadi ya kadi yenye maneno mazuri yanayoelezea hisia zako kwake,
Unapomhudumia kwa kumjali,
Unapomsikiliza yeye na kujiona anasikilizwa,
Unapjitolea kumsaidia kazi ndgondogo na mambo ambayo anajisikia upo na yeye,
Unapompa plan za mambo mbalimbali mnayotaka kufanya pamoja kama familia iwe "outing", likizo, business n.k,
Pale unapomuuliza anavyojisikia hasa baada ya kazi au unapohisi emotions zake hazipo sawa,
Unapochukua muda wa ziada kuwa naye na kuwa kwa ajili yake,
Unaposhirikiana naye ktk huzuni au tatizo huku ukimfariji na kumkumbatia,
Unapompa nafasi ya kujisikia huru kwako hata kudeka (si wote)
Unapogundua kwamba amevaa amependeza mavazi na nywele na kumpa sifa anazostahili.
Unapom-surprise na zawadi au notes na
Unapompigia simu ukiwa umesafiri na kumuulizia anaendeleaje na jinsi gani utakuwa unaongea naye na kuwasiliana naye.