Using'ang'anie watu ambao unatakiwa kuachana nao

Nimeshawahi kupoteza VITU ambavyo niliamini bila kuwa navyo sitaweza kuishi vizuri.

Nimeshawahi kupoteza WATU ambao niliamini bila kuwa nao sitaweza kufika ninakokwenda.

Nimeshawahi kupoteza NAFASI ambazo niliamini nikizikosa sitaweza kutimiza malengo yangu tena.

Kuna wakati unafika katika maisha UNAJIAMINISHA MOYONI...
.
...au unaaminishwa na WANAOKUZUNGUKA kuwa bila MTU FULANI au KITU fulani basi ndio utakuwa MWISHO wa safari yako.

Katika nyakati kama hizo niliwahi kupewa neno la HEKIMA ambalo limekuwa msaada mkubwa sana siku zote za maisha yangu.

Niliambiwa kuwa “Sio kila UNAYEMPOTEZA au kila UNACHOPOTEZA ni HASARA KWAKO”.

Ukiambiwa neno hili katikati ya maumivu hauwezi kuelewa.

Ila baada ya muda nimegundua lina ukweli ndani yake.

Kuna mabadiliko lazima yatokee kwanza ili uwe vile unavyotaka.

Kuna watu ambao lazima WAONDOKE kwenye maisha yako usogee hatua unayopata.

Kuna wengine inalazimika wapoteze kazi zao za sasa ili wapate kazi kubwa zaidi.

Kuna wengine inalazimika WAKATALIWE kwenye mambo fulani ili wapate hasira ya kufanya kitu wanachotakiwa kufanya.

Kuna wakati mtu unakuwa “so relaxed” na hautaki kusumbuliwa kwa namna yoyote.

Mungu anapokuangalia anajua ukiendelea hivyo HAUTAKUWA vile unatakiwa KUWA na HAUTAFIKA kule unatakiwa KUFIKA.

Lazima meli ipitie DHORUBA ili UTUPWE BAHARINI na umezwe na SAMAKI kisha akakutapike unakotakiwa kwenda.

Sio kila DHORUBA inapokuja, ukimuomba MUNGU ataiondoa.

NYINGINE AMEILETA ili: AKUTENGE na baadhi ya VITU, akutoe katikati ya WATU FULANI...

..au akutoe kwa LAZIMA eneo ambalo ukiendelea kuwepo UTADUMAA na utashindwa kufikia kilele cha MAFANIKIO YAKO.

Nakuombea AKILI yako ifunguke na USING’ANG’ANIE WATU ambao unatakiwa kuachana nao.

Somo kwa hisani ya Joel Nanauka

#timizamalengoyako.
Mtumishi barikiwa sana AMEN
 
Andiko sahihi kabisa na ukweli mtupu so zile .
Nimekutana na jamaa rafiki yangu kuanzia form one mpaka tunaenda advance tukawa pamoja baada ya matokeo yeye alipata chuo kingine na Mimi kingine hapa hapa Dar ,ila urafiki ulipotea kapata washkaji wengine na mmi Nina washkaji wengine.

Niliowapata chuo baada ya kumaliza kila mtu kapotea kivyake... Nipo kweny mishe nimepata washkaji wengine sio kama nimeloose coz hata nilioishi nao kitaa tuliachana miaka 8 nyuma hatujaonana watu niliokuwa nao pamoja.

Ushauri wangu angalia kampani na kilicho mbele yako ndo maisha hayarudi ,usijiumize sana historia zitabaki tu milele ishi kwa wema kama mapenzi kuachana kwa wema dunia inasonga ..Binafsi nishazoea kujichanganya siangalii dini wala kabila ndo maisha hayarudi nyuma tujiamini kila mtu atasurvive kwa nafsi yake hamna kumtegemea mwingine
Hongera sana kiongozi kwa kufanya hayo uliyoyafanya, Mungu akubariki unaposonga mbele.
 
Ukweli kwenye maisha ya kibongo hakuna rafiki wa Kama financially haupo stable.

Mimi wakati naanza maisha nilipoteza marafiki mpaka ndugu Ila focus yangu ilikuwa siku moja kuwashangaza.

Watu walifuta namba zangu za simu na wengine walisema Sina nidhamu kwa wakubwa Natakiwa kunyeyekea.

Ila Kuna siku media mmoja kubwa ilinihoji na nakumbuka kesho yake nilipokea simu nyingi Sana za ndugu na marafiki mpaka nilijishangaa.

Kiufupi nilikuwa nimejitenga na marafiki uchwara kwa muda Kama wa miaka 8 hivi Ila maisha yangu yalibadilika Sana nilitengeneza connection na watu ambao hata siwajui nje na ndani ya nchi.

Waliokuwa wakitaka niajiriwe serikalini wote walipigwa na butwaa maisha yangu yamekuwa Mara kumi zaidi ya maisha yao.

Kiufupi nimegundua katika maisha hakuna formula ni jinsi wewe unavuoamua yawe na usimamie misingi.

Na ukubali kuanza from the scratch pia uwe na mwenza mwenye mentality ambayo mnaendana.

Rafiki yako mkubwa duniani ni Mtoto wako, Mke wako au mme wako wa ndoa, Mama then Baba.

Hawa wengine wanatazama tu umefanikiwa vipi ndio wawe na wewe.
 
Kiufupi nilikiwa nimejiteanga na marafiki uchwara kwa muda Kama wa miaka 8 hivi Ila maisha yangu yalibadolika Sana nilitengeneza connection na watu ambao hata siwajui nje na ndani ya nchi.

Waliokuwa wakitaka niajiriwe serikalini wote walipigwa na butwaa maisha yangu yamekuwa Mara kumi zaidi ya maisha yao.

Kiufupi nimegundua katika maisha hakuna formula ni jinsi wewe unavuoamua yawe na usimamie misingi.

Na ukubali kuanza from the scratch pia uwe na mwenza mwenye mentality ambayo mnaendana.

Rafiki yako mkubwa duniani ni Mtoto wako, Mke wako au mme wako wa ndoa, Mama then Baba.

Hawa wengine wanatazama tu umefanikiwa vipi ndio wawe na wewe.
Umesema kweli kabisa
 
Vipi kwa wale ambao wakipoteza walivyodhani ni vya umuhimu kuliko hawanyanyuki tena inakua bora jana? na haijalishi ni kwa namna gani wamejitahidi kustawi ila bilabila.
 
K

Unajua kuna wengine huwa wanapokea malipo ya matendo yao hapa hapa duniani, ukiwa mwema utavuna mema, ukiwa mwovu utavuna uovu.
 
Nimeshawahi kupoteza VITU ambavyo niliamini bila kuwa navyo sitaweza kuishi vizuri.

Nimeshawahi kupoteza WATU ambao niliamini bila kuwa nao sitaweza kufika ninakokwenda.

Nimeshawahi kupoteza NAFASI ambazo niliamini nikizikosa sitaweza kutimiza malengo yangu tena.

Kuna wakati unafika katika maisha UNAJIAMINISHA MOYONI...
.
...au unaaminishwa na WANAOKUZUNGUKA kuwa bila MTU FULANI au KITU fulani basi ndio utakuwa MWISHO wa safari yako.

Katika nyakati kama hizo niliwahi kupewa neno la HEKIMA ambalo limekuwa msaada mkubwa sana siku zote za maisha yangu.

Niliambiwa kuwa “Sio kila UNAYEMPOTEZA au kila UNACHOPOTEZA ni HASARA KWAKO”.

Ukiambiwa neno hili katikati ya maumivu hauwezi kuelewa.

Ila baada ya muda nimegundua lina ukweli ndani yake.

Kuna mabadiliko lazima yatokee kwanza ili uwe vile unavyotaka.

Kuna watu ambao lazima WAONDOKE kwenye maisha yako usogee hatua unayopata.

Kuna wengine inalazimika wapoteze kazi zao za sasa ili wapate kazi kubwa zaidi.

Kuna wengine inalazimika WAKATALIWE kwenye mambo fulani ili wapate hasira ya kufanya kitu wanachotakiwa kufanya.

Kuna wakati mtu unakuwa “so relaxed” na hautaki kusumbuliwa kwa namna yoyote.

Mungu anapokuangalia anajua ukiendelea hivyo HAUTAKUWA vile unatakiwa KUWA na HAUTAFIKA kule unatakiwa KUFIKA.

Lazima meli ipitie DHORUBA ili UTUPWE BAHARINI na umezwe na SAMAKI kisha akakutapike unakotakiwa kwenda.

Sio kila DHORUBA inapokuja, ukimuomba MUNGU ataiondoa.

NYINGINE AMEILETA ili: AKUTENGE na baadhi ya VITU, akutoe katikati ya WATU FULANI...

..au akutoe kwa LAZIMA eneo ambalo ukiendelea kuwepo UTADUMAA na utashindwa kufikia kilele cha MAFANIKIO YAKO.

Nakuombea AKILI yako ifunguke na USING’ANG’ANIE WATU ambao unatakiwa kuachana nao.

Somo kwa hisani ya Joel Nanauka

#timizamalengoyako.
"Kuna watu ambao lazima WAONDOKE kwenye maisha yako usogee hatua unayopata."

"Kuna wengine inalazimika wapoteze kazi zao za sasa ili wapate kazi kubwa zaidi."

"Kuna wengine inalazimika WAKATALIWE kwenye mambo fulani ili wapate hasira ya kufanya kitu wanachotakiwa kufanya."

FACT
 
Aisee wewe!
Haya boss
Ndio hivyo mkuu ukiwa weak watu watakuendesha kama gari bovu .Kuna jirani yangu mmoja nilikua namsalimia freesh tu akaanza uswahili nimekata mpaka salamu namuona kama jiwe tu.Akajipendekeza kuniuliza sababu ni nini nikamwambia kuanzia leo nimeamua tu sikuheshimu na maisha yanaenda.
 
Ulifunga kabisa muunganiko naye mtu asiyefaa, hiyo ni sawa.
 
"Kuna watu ambao lazima WAONDOKE kwenye maisha yako usogee hatua unayopata."

"Kuna wengine inalazimika wapoteze kazi zao za sasa ili wapate kazi kubwa zaidi."

"Kuna wengine inalazimika WAKATALIWE kwenye mambo fulani ili wapate hasira ya kufanya kitu wanachotakiwa kufanya."

FACT
Hakika kiongozi.
 
Ukweli kwenye maisha ya kibongo hakuna rafiki wa Kama financially haupo stable.

Mimi wakati naanza maisha nilipoteza marafiki mpaka ndugu Ila focus yangu ilikuwa siku moja kuwashangaza.

Watu walifuta namba zangu za simu na wengine walisema Sina nidhamu kwa wakubwa Natakiwa kunyeyekea.

Ila Kuna siku media mmoja kubwa ilinihoji na nakumbuka kesho yake nilipokea simu nyingi Sana za ndugu na marafiki mpaka nilijishangaa.

Kiufupi nilikuwa nimejitenga na marafiki uchwara kwa muda Kama wa miaka 8 hivi Ila maisha yangu yalibadilika Sana nilitengeneza connection na watu ambao hata siwajui nje na ndani ya nchi.

Waliokuwa wakitaka niajiriwe serikalini wote walipigwa na butwaa maisha yangu yamekuwa Mara kumi zaidi ya maisha yao.

Kiufupi nimegundua katika maisha hakuna formula ni jinsi wewe unavuoamua yawe na usimamie misingi.

Na ukubali kuanza from the scratch pia uwe na mwenza mwenye mentality ambayo mnaendana.

Rafiki yako mkubwa duniani ni Mtoto wako, Mke wako au mme wako wa ndoa, Mama then Baba.

Hawa wengine wanatazama tu umefanikiwa vipi ndio wawe na wewe.
"Kiufupi nimegundua katika maisha hakuna formula ni jinsi wewe unavuoamua yawe na usimamie misingi"

🤝🤝🤝
 
uko sahihi 100%
 
Back
Top Bottom