Using'ang'anie watu ambao unatakiwa kuachana nao

Using'ang'anie watu ambao unatakiwa kuachana nao

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,972
Reaction score
22,922
Nimeshawahi kupoteza VITU ambavyo niliamini bila kuwa navyo sitaweza kuishi vizuri.

Nimeshawahi kupoteza WATU ambao niliamini bila kuwa nao sitaweza kufika ninakokwenda.

Nimeshawahi kupoteza NAFASI ambazo niliamini nikizikosa sitaweza kutimiza malengo yangu tena.

Kuna wakati unafika katika maisha UNAJIAMINISHA MOYONI...
.
...au unaaminishwa na WANAOKUZUNGUKA kuwa bila MTU FULANI au KITU fulani basi ndio utakuwa MWISHO wa safari yako.

Katika nyakati kama hizo niliwahi kupewa neno la HEKIMA ambalo limekuwa msaada mkubwa sana siku zote za maisha yangu.

Niliambiwa kuwa “Sio kila UNAYEMPOTEZA au kila UNACHOPOTEZA ni HASARA KWAKO”.

Ukiambiwa neno hili katikati ya maumivu hauwezi kuelewa.

Ila baada ya muda nimegundua lina ukweli ndani yake.

Kuna mabadiliko lazima yatokee kwanza ili uwe vile unavyotaka.

Kuna watu ambao lazima WAONDOKE kwenye maisha yako usogee hatua unayopata.

Kuna wengine inalazimika wapoteze kazi zao za sasa ili wapate kazi kubwa zaidi.

Kuna wengine inalazimika WAKATALIWE kwenye mambo fulani ili wapate hasira ya kufanya kitu wanachotakiwa kufanya.

Kuna wakati mtu unakuwa “so relaxed” na hautaki kusumbuliwa kwa namna yoyote.

Mungu anapokuangalia anajua ukiendelea hivyo HAUTAKUWA vile unatakiwa KUWA na HAUTAFIKA kule unatakiwa KUFIKA.

Lazima meli ipitie DHORUBA ili UTUPWE BAHARINI na umezwe na SAMAKI kisha akakutapike unakotakiwa kwenda.

Sio kila DHORUBA inapokuja, ukimuomba MUNGU ataiondoa.

NYINGINE AMEILETA ili: AKUTENGE na baadhi ya VITU, akutoe katikati ya WATU FULANI...

..au akutoe kwa LAZIMA eneo ambalo ukiendelea kuwepo UTADUMAA na utashindwa kufikia kilele cha MAFANIKIO YAKO.

Nakuombea AKILI yako ifunguke na USING’ANG’ANIE WATU ambao unatakiwa kuachana nao.


Somo kwa hisani ya Joel Nanauka

#timizamalengoyako.
 
Vyema sana kupeana moyo na kuishi kwa Imani. Shukrani
 
Ahsante Mleta mada....Barikiwa sana...

Kitu nimejifunza na ninazidi kujifunza kuna mazingira au kuna vitu Mungu hawezi kutupatia katika mazingira tuliyopo au watu tulionao/Wanaotuzunguka....

Ni lazima aviondoe/ Waondoke..
Wakati mwingine anawaondoa hata Rafiki zako wa dhati kabisa..unajaribu kujiuliza ni nini kimetokea...hupati majibu...
 
Andiko sahihi kabisa na ukweli mtupu so zile .
Nimekutana na jamaa rafiki yangu kuanzia form one mpaka tunaenda advance tukawa pamoja baada ya matokeo yeye alipata chuo kingine na Mimi kingine hapa hapa Dar ,ila urafiki ulipotea kapata washkaji wengine na mmi Nina washkaji wengine.

Niliowapata chuo baada ya kumaliza kila mtu kapotea kivyake... Nipo kweny mishe nimepata washkaji wengine sio kama nimeloose coz hata nilioishi nao kitaa tuliachana miaka 8 nyuma hatujaonana watu niliokuwa nao pamoja.

Ushauri wangu angalia kampani na kilicho mbele yako ndo maisha hayarudi ,usijiumize sana historia zitabaki tu milele ishi kwa wema kama mapenzi kuachana kwa wema dunia inasonga ..Binafsi nishazoea kujichanganya siangalii dini wala kabila ndo maisha hayarudi nyuma tujiamini kila mtu atasurvive kwa nafsi yake hamna kumtegemea mwingine
 
Back
Top Bottom