Using'ang'anie penzi la asiekupenda

Using'ang'anie penzi la asiekupenda

haya mambo hayaaa, haya sasa maskin member wa watuu kashinda vizuri na afya yake sasahv analiaa
 
Umesema yote
Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona haelekei ujue hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila siku kwa kumuangalia yeye tu?

Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na unamuhitaji sana, ila kama yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia na wewe sasa.

Ona thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu asiyeona thamani yako.

Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani, bila kujali muonekano wala rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali na si anayekufanya kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa mapenzi kwa kuiona thamani yako.

Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au muonekano mzuri ikiwa hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha.

Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau shida zao. Ila jiulize kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno mazuri ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani???
 
Nimeamini hata sikutegemea kumbe hata ukiumwiza bado utapenda😍😍😍😍
 
Hili jambo linanikuta mimi sasa ivi.. Na Leo ndio siku ya kumove one rasmi
 
Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona haelekei ujue hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila siku kwa kumuangalia yeye tu?

Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na unamuhitaji sana, ila kama yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia na wewe sasa.

Ona thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu asiyeona thamani yako.

Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani, bila kujali muonekano wala rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali na si anayekufanya kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa mapenzi kwa kuiona thamani yako.

Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au muonekano mzuri ikiwa hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha.

Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau shida zao. Ila jiulize kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno mazuri ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani???
Wewe tafuta pesa pata hadhi kubwa .Hakuna atakayekuchukia wa kukuacha .Eti unataka mapenzi ya dhati nani akupe hayo mapenzi wakati huna hadhi yoyote katika jamii ya unayempenda wala huna pesa .Hakika nakuambia hata ukate mauno kama panga boi ukiwa huna pesa huna hadhi Kubwagwa ni kawaida tu.
 
Breakup is unhealthy!!
I remember when I got dumped, while I was on my way to pick my nephew at school. I came home with the wrong child
Nimecheka hadi, kijambo kimenipitia, bahati nzuri niko peke yangu tu hapa hakuna mtu mwingine.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Kuachwa kunauma sana, kunahitaji courage na busara ya juu sana kijistabilize .Ndo maana mtu akiachwa kama hana self determination anakuwa drug addicts au malaya wa kipindukia hii yote ni kutafuta relief. Kuna kijana mmoja aliyekuwa the only son kwa familia ya wazazi ambao walimgharamia kumpeleka India kusoma na wameshafika menopouse alijiua kwa sumu kisa kaachwa na girlfriend wake,sikuumizwa na kifo chake but niliumizwa na situation ya wazazi wake .Don't mess around with love breakups.
 
Bahati nzuri at that moment hakukuwa na masuala ya Whatsapp status, even mambo ya social media hazikuwa zimepamba moto kama sasa hivi
Kwa hiyo brother ulivyofika nae nyumbani na kugundua si yeye, ulifanyaje?
 
Back
Top Bottom