Using'ang'anie penzi la asiekupenda

Using'ang'anie penzi la asiekupenda

Nsam

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2018
Posts
212
Reaction score
290
Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona haelekei ujue hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila siku kwa kumuangalia yeye tu?

Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na unamuhitaji sana, ila kama yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia na wewe sasa.

Ona thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu asiyeona thamani yako.

Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani, bila kujali muonekano wala rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali na si anayekufanya kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa mapenzi kwa kuiona thamani yako.

Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au muonekano mzuri ikiwa hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha.

Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau shida zao. Ila jiulize kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno mazuri ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani???
 
kipindi umeachwa Automatic utajikuta mwanafalsafa mbobezi unayetambulika na Dunia kumbe ni swala la muda tu . vumilia tu mapenzi ni hisia sisizochosha utapata mwingine.
msikilize khalidi chokoraa 📩🎵

 
mkuu huyo mtoto uliwezaje kumrudisha
Mkuu acha kabisa, nakumbuka niliambiwa na sister nikamchukue nikasahau kwa sababu ya mawazo kibao, nakuja kukumbuka mda umekwisha pita wa kufuata watoto, nafika shuleni nikamkuta mtoto mmoja tu hajachukuliwa na wazazi, kibaya zaidi nilipokelewa na makelele ya teacher ananiambia muwe mnawahi kuchukua watoto wakibaki peke yao huwa wanalia, wakati namsikiliza teacher dogo akafungua mlango wa wa gari na kuchupa ndani, nafika kwa sister ananiuliza ni mtoto wa nani huyo, kumbe mtoto wa sister alirudi na jirani😂😂😂
 
Mkuu acha kabisa, nakumbuka niliambiwa na sister nikamchukue nikasahau kwa sababu ya mawazo kibao, nakuja kukumbuka mda umekwisha pita wa kufuata watoto, nafika shuleni nikamkuta mtoto mmoja tu hajachukuliwa na wazazi, kibaya zaidi nilipokelewa na makelele ya teacher ananiambia muwe mnawahi kuchukua watoto wakibaki peke yao huwa wanalia, wakati namsikiliza teacher dogo akafungua mlango wa wa gari na kuchupa ndani, nafika kwa sister ananiuliza ni mtoto wa nani huyo, kumbe mtoto wa sister alirudi na jirani
kimbembe mtoto kumrudisha kwao ulianzaje
 
Mbaka Sasa nawaza ulikua na mawazo gani........like na imagine

We jamaaaaaa....Leo umenitoa stress.
😂😂😂 mkuu, mda huo mi nipo nipo tu, yaani watu wanaongea mi yanapita sikio hili yanatokea sikio lingine, mda huo mie kifua kimejaa maumivu na stress kibao, kila anayeongea namuona kero mbele yangu
 
Back
Top Bottom