Swali?
Walijifunza saa ngapi uwanajeshi na ili kudhibitisha kwamba ni Mwanajeshi Mungu anamtuma kwa Mwanamme akamlinde.
Yeremia 31:22 .... Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya Duniani; Mwanamke atamlinda Mwanamume.
KUMBUKA HILI MWANAUME MWENZANGU.
●Mtu wa Kwanza kukutana na SHETANI live ni Mwanamke pamoja na kwamba walizungumza mengi na kula tunda kiukweli hatujui mengine waliozungumza mbali na kula tunda.
●MWANAMKE aliumbwa ukiwa usingizini wewe MWANAUME hujui ni kitu gani walichozungumza na Mungu kabla ya wewe kuzinduka.
●MWANAMKE ndiye aliyemwelewa Mungu alipoambiwa ana mimba ya Roho Mtakatifu wewe MWANAUME ulitaka kumkimbia badala ya kukabiliana na changamoto hiyo.
●MWANAMKE ndiye Mtu wa kwanza kwenda kuhakikisha kama kweli Yesu amefufuka na kusambaza habari.
●MWANAMKE ndiye anayeongoza kwa ushawishi mkubwa, Mwanaume huna ujanja mfano. ■Eva kwa Adamu ■Delila kwa Samson ■Ester kwa Ahasuero ■Raheli kwa Labani n.k
Usimuudhi Mke wako ana Siri kubwa sana usione kakaa na wewe anakuvumilia pamoja na ukatili wako.
Toka nje ya box mkuu, wanaume tuna siri nyingi zaidi za wake zetu. Usifungwe na vifungu vichache vinavyozungumzia nguvu za mwanamke ukaacha vifungu lukuki vinavyozungumzia nguvu ya mwanaume.
Toka nje ya box mkuu, wanaume tuna siri nyingi zaidi za wake zetu. Usifungwe na vifungu vichache vinavyozungumzia nguvu za mwanamke ukaacha vifungu lukuki vinavyozungumzia nguvu ya mwanaume.
Hapo kwenye kuvumilia ukatili wako ni kwa sababu wanaamini utakufa mapema tu kabla yake, hasira hukaa kifuani mwa mtu mpumbavu... hivyo atakuhesabia tu udondoke.