Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,094
- 79,491
KANUNI YA 3; USIMUAIBISHE MUNGU.
Na, Robert Heriel
ANGALIZO;
Makala hii, isomwe na mtu mwenye umri kuanzia miaka 18.
Nisihesabike sehemu ya hatia endapo mtu yeyote ambaye yupo chini ya hapo ataamua kusoma. Makala hii, kwa sehemu ndogo itatumia lugha ngumu hivyo kama hupendi kusoma lugha ngumu tafadhali naomba usisome.
Niite Taikon wa Fasihi, mwanafalsafa katika zama za utandawazi.
Ilipo fahari watu hufurahia na kukimbilia, ilipo fedheha watu huhuzunika na kupakimbia. Aibu huja pasipo hodi, aibu inamiguu elfu, ina mbio kama duma, Nani awezaye kuikimbia fedheha, kwa maana fedheha huruka kama kipanga, kwa kasi humpata mpumbavu. Basi mche Mungu ili aibu isikupate.
AIBU ni hisia mbaya inayoumiza ya udhalilishaji inayosababishwa na utambuzi wa kufanya jambo kipuuzi au la kijinga au kufanyiwa jambo la kipuuzi au la kijinga.
Hakuna ambaye hajawahi kupata aibu dunia ingalipo.
Kwenye aibu kuna kujiaibisha na Kuaibishwa.
Zipo aibu za maneno na aibu za vitendo. Hakuna aibu ya kufikiri kwani mtu ukimuwazia mambo ya kipuuzi huwezi kumuonea au hawezi kukuonea aibu kwani hajui na wewe unajua hajui. Aibu sharti ihusu watu zaidi ya mmoja au wahusika zaidi ya mmoja. Aibu ikifahamika na mtu mmoja hubaki kuwa siri.
AIBU inayozungumziwa hapa leo ni ile ya Fedheha, wala hatuzungumzii HAYA au SONI ambayo ni tabia ya mtu kuona aibu mbele za watu. Hapa tunazungumzia ile aibu inayohusu hisia mbaya inayodhalilisha mtu.
Msingi mkuu wa aibu ya mwanadamu ni Utu wake. Kikawaida kila mwanadamu hupenda kuheshimiwa, na ili uheshimiwe utahitajika mambo makuu yafuatayo;
1. Sheria za Mungu
2. Sheria za nchi
3. Maadili, miiko desturi na tamaduni ya jamii yako.
Mambo hayo makuu matatu ndio humfanya mtu aheshimike na kuyavunja hayo au kuvunjiwa hayo ndio huitwa FEDHEHA.
Kila jamii ina amini katika mungu wake, hii ni kusema kila mungu anasheria zake kulingana na jamii husika inavyoamini. Mwanajamii yoyote kwenye kinyume na sheria za mungu wake hujitia aibu yeye mwenyewe mbele ya jamii yake.
Kila nchi inasheria zake, kutofuata sheria za nchi yako ni kutafuta aibu na fedheha, ndio maana hata mafisadi licha ya kuwa na pesa nyingi lakini kwao ni Fedheha kumuita Fisadi au mhujumu uchumi.
Leo tutazungumzia mada isemayo Usimuabishe Mungu!
Kizazi cha sasa ni kizazi ambacho kwa hakika kimeamua kwa dhati yote kumuabisha Mungu wao. Ni kizazi ambacho kimekusudia kumnyoosha Mungu mpaka ajute kwa nini aliumba kizazi hiki. Kwa hakika, Mungu hawezi kuyaangalia yanayoendelea katika kizazi hiki.
Mtu anayekuabishia unamchukuliaje? Unamuonaje? Je unaweza kumtazama? Je unaweza kumpa muda wako mkapiga stori?
Kumuabisha Mungu ni kwenda kinyume na sheria zake. Kwa mfano mtu yeyote asiyetaka kazi na asiyefanya kazi huyo ni fedheha kwa Mungu wake. Anamuabisha Mungu wake. Utaishije bila kufanya kazi,
Mtu asiyewaheshimu wazazi wake, huyo anamuabisha Mungu. Utaishije bila kuwaheshimu wazazi wako, hakuna udhuru wowote wa kukufanya usiwaheshimu wazazi wako, Hata kama walikufanyia nini, sheria ni moja tuu, waheshimu Baba na mama yako, ili siku zako zipate kuwa nyingi.
Unafanya uzinzi kila kukicha, umejigeuza mbwa kila dume unataka likupande, na mwanaume umejigeuza Fisi kama sio jogoo kila jike unataka kulipanda, acha kujiabisha, acha kumuabisha Mungu.
Huwezi furahia maisha kwa kumuabisha Mungu aliyekuumba. Yaani kugonga wanawake na malaya ndio iwe furaha yako? Huoni una shida mahali? Yaani kuvunja sheria za Mungu kwako ndio starehe huoni unamatatizo, huoni kuna hatari inakuvuta kwa nguvu. Acha kugonga wake za watu, acha kuiba waume za watu.
Unakuta kijana anajivunia kumuabisha Mungu, anasema; Nimeshalala na wanawake hamsini, mimi ni Rijali" Wewe ni Rijali wa kumuabisha Mungu wako. Yule aliyesema usizini na usitamani mke wa jirani yako, wewe ndiye unajifanya mjanja kumuabisha.
Ikiwa wewe hupendi kuabishwa, unafikiri Mungu ndio anapenda?
Unafanya wizi alafu unachekelea kuendesha magari mazuri ya kifahari ya wizi, unajenga mijengo kwa pesa za wizi ulioiba kwenye mali za watu masikini, unasema umetusua kama sio kutoboa maisha. Kumuabisha Mungu ndio kutoboa, hahahah!
Wewe ni mwehu sana. Hakuna aliyewahi kusifiwa kwa kumuabisha Mungu, hakuna na hatakuwepo. Hakuna atakayekusifia kwa kuiba na kudhulumu pesa za watu masikini, hata wewe mwenyewe hutajisifu bali utakuwa unajidanganya kuwa umepata raha.
Kwenye maisha ogopa kumuabisha Mungu, hilo ukilimudu basi maisha yako bwerere. Sio lazima upate hela, sio lazima ujenge, sio lazima upate magari mazuri, kwenye maisha hakuna jambo la lazima isipokuwa Mungu. Mungu ndiye wa lazima, ukishalijua jambo hili itakusaidia sana hasa siku za hatari na zisizo na msaada.
Utakapofanya jambo fulani kuwa la lazima upo kwenye hatari ya kumuabisha Mungu wako. Mungu ndio walazimi na yeye ndiye anajua kwako kipi ni chalazima.
Watu wengi walidhani elimu ni yalazima, wakasahau kuwa hakuna kilicho cha lazima isipokuwa Mungu. Wamemaliza sasa, wanajikuta wanaelimu lakini haina ulazima wowote huku mtaani. Wanalaumu na kulalamika. Mtu ageuzaye kitu kuwa cha lazima hutafuta kulalamika.
Wapo waliofikiri pesa ni yalazima, wameitafuta na wameipata lakini wanakuja kugundua kuwa pesa sio ya lazima, wenye pesa wanaelewa kile nikisemacho, pesa haikuongezeo chochote ndani ya moyo, akili, ubongo, hisia pesa huongeza mambo ya nje kama nyumba, magari, mavazi, simu kali, n.k
Pesa inakuwa tamu pale unapokuwa na Mungu.
Hapo utakuwa unasaidia watu, utakuwa unatoa sadaka kwa wahitaji, utakuwa unawalipa wafanyakazi wako vizuri, Mke wako ataenjoi na watoto.
Lakini pesa inakuwa chungu pale Mungu usipokuwa naye.
Utakuwa unadhulumu watu ili uzidi kuwa tajiri. Utawalipa wafanyakazi wako kidunchu kama misukule yako, hawatakuwa na furaha bali watakuwa kama watumwa wako, Utakuwa unagongea wanawake wengine hivyo utamsononesha Mke wako, utaleta ugomvi baina ya watoto kwani utakuwa umezaa watoto kwa mama tofauti tofauti, familia haitakuwa na amani. Utaanza kuumwa na maradhi kwani utakuwa unakula chochote hata kama ni haramu kwa sababu hauna Mungu.
Usimuaibishe Mungu. Mungu akikupa zawadi au baraka itumie ipasavyo. Kuitumia ipasavyo ndio namna pekee ya kumshukutu Mungu na kumfanya ajionee fahari nawe.
Ukipewa Mke, mpe penzi la moto acha kuzubaa zubaa. Mridhishe kitandani kwa mikwaju na slow motion za uhakika. Mwanamke atosheke mpaka asema basi. Kumridhisha mwanamke kitandani ni kumpa utukufu Mungu wako. Ni kuonyesha uwezo wa kutumia uume wako, akili, na ufundi wa kila namna.
Sio unamuabisha Mungu, ukiwa na Mke wako, unambwela mbwela kama boyapori. Kimoja kama cha jogoo unalala kama mpuuzi, wewe ni mwanaume, fanya kama mwanaume. Tumia akili na wakati mwingine nguvu.
Mungu amekupa Mke mzuri unashindwa kazi, wewe ni fala, kazi kujilia mavyakula kama mpuuzi tuu. Wakati Mungu akikupa maelekezo ya vyakula gani utumie ulimuona Fala sana. Sasa unaposhindwa kumchezesha mkeo unaanza kutafuta mchawi. Mpuuzi wewe. Kazi kujiabisha huko kwa kutafuta waganga na waganguzi, acha kumuabisha Mungu. Piga mzigo.
Mwanamke umepewa Mume mzuri unazubaa zubaa tuu. Mzigo hutoi kwa wakati, na ukitoa umalala kama maiti inayooshwa. Acha kumtia Mungu aibu. Umepewa sauti nzuri, itumie, umepewa umbo nzuri litumie, umepewa ngozi laini itumie, umepewa macho mazuri yatumie. Sio umezubaa zubaa kama kikaragosi. Acha kumtia Mungu aibu.
Maandiko yanasema; kwa maana katika zama hizi waovu wamekuwa na busa na hekima kuliko wana wa nuru.
Usimuabishe Mungu kwa kushindwa kumridhisha mkeo au mumeo. Kazi kukuza kitambi kama Boya, Vyakula vinavyoleta kitambi kiasili ni haramu, vyakula vinavyoharibu nguvu za kiume kiasili ni haramu. Sema watu hilo hawalijui wanachojua ni kula kula kama nguruwe. Mwishowe wake zao wakiliwa huanza kupiga mayowe.
Mwanamke jisitiri, acha kutemba mwili ukiwa uchi, acha kutuonyesha chupi iliyojichora makalioni, acha kumuabisha Mungu wako. Hakuna ambaye anataka kuona uzuri wako, muonyeshe mumeo ukiwa ndani ya nyumba. Hiyo itakupa thawabu.
Ni dhambi na aibu kwa Mungu mwanamke kujipendezesha na kuacha Maungo yake mbele za watu. Mwanamke anapaswa ajirembe na kuonyesha maungo yake kwa Mumewe tuu wakiwa nyumbani tuu. Akitoka nje, anapaswa kujitanda na kujistiri haswa.
Kuna majianaume majinga hayataelewa, huwezi lia mkeo akigongwa nje wakati hukumkataza kuvaa vimini, huwezi lia mkeo ni malaya wakati wewe ndio umemfundisha umalaya. Mungu aliposema mwanamke avae za kujisitiri ulimuona fala sana. Ukashindwa kumkazania mkeo kuwa asivae upuuzi, sasa ukimkuta amebananishwa na kukunjwa popo kanyea mbingu unaanza kulia lia, hahaha! Wengine wanataka kuua, wengine kunywa sumu, hahaha! Ukimuabisha Mungu mbona sumu utazinywa sana.
Lazima ujue kuwa Mungu anaakili kukuzidi wewe mara elfu elfu. Akikukataza jambo fulani anamaana zake.
Unaambiwa usifanye zinaa, tunza bikra yako mpaka utakapoolewa. Unamuona Mungu Fala sana. Unajichetua, unatoa, mwishowe mimba, unaanza kulia lia, mimba umeachiwa, unaamua kutoa, au kuilea, mwanaume nduki kakimbia. Hahahaha! Unaanza kusema wanaume wabaya, kwani wewe mzuri, kama ungeitunza hiyo bikra yako hiyo Mimba ingeingia kwa wireless kama bikra maria.
Mwishowe unaanza kuona wanaume vibamia. loooh!
Wanaume nao wanajifanya wanaakili kumshinda Mungu, unataka kuoa, unaambiwa oa mwanamke bikra, unasema ooho naenda na wakati, haya nenda nao, ukifika huko mbele unaanza kulia ooh sisikii raha kwa mke wangu, Mkeo naye anakuona huna lolote. Yaani kuvuragana. Acha kumtia Mungu aibu.
Taikon nimemaliza mwenye swali karibu kuuliza.
Ulikuwa nami;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro