Binti Magufuli
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 7,479
- 5,160
Natumaini weekend yenu iko njema. Kwangu mimi; Weekend hii hata siielewi elewi, mchana nilijua ni njaa so nilienda kutafuta ndizi ili nipike machalari yangu nile hali itulie. Tofauti na matarajio yangu hata baada ya kula machalari yangu bado naiona haileweki. Nashukuru Mungu inaishia hivyo.
Leo nimeguswa na swala moja; Unamkuta mtu amefulia, hana uelekeo, anaishi kama hayupo vile...basi huruma inakujia unaanza kuumiza kichwa kuhusu namna ya kumsaidia huyu binadamu mwenzako kiroho safi kabisa. Huku na kule kweli unampatia dili na unamsaidia mwanzo mwisho namna ya kuligrab hilo dili hadi linatua mikononi mwake na maisha ya jamaa ghafla bin vup yanabadilka anaanza kupiga mahesabu ya madolari ya uhakika. Jamaa mambo yakishamuendea ndo kwaanza hata hakutambui tena, hata uwe na shida ya namna gani hawezi kukutoa tena (hata kama iko ndani ya uwezo wake), au akiamua kukusaidia basi atakuwekea masharti weeeee hadi unaamua kusarenda mwenyewe, hiyo haitoshi anadiriki kukaa kwenye makundi na kukuambukiza ubaya na kukuchafua. Hivi sisi binadamu tukoje lakini? inakuwa ngumu sana kukumbuka tulikotoka, tulipo na tumefikaje hapo? hivi ulisikia shida za dunia ndio zimefikia tamati?
Tunapaswa kutambua kuwa dunia ni duara na si kwamba tu inalizunguka jua na mhimili wake bali hata na mambo ya maisha yanazunguka, kesho hujui unakutana na nani, wapi na kwa namna gani.....tenda mema usikumbuke kulipwa, lakini pia na wewe uliyetendewa jema kumbuka walau kuonesha heshima na shukrani kwa mtu aliyetumia muda na akili yake kukusaidia, unajifanya jogoo kwa kuwa alishakusaidia ila kumbuka kuna watu ambao kwa asili Mungu amewaumba na bahati , kama ambavyo alikuonesha dili flani ndivyo hivyo yatapatikana mengi kupitia mtu huyo.........
Pamoja na ukweli kwamba binadamu hawabebeki siwezi toa ushauri wa fadhila mfadhili mbuzi umnywe mchuzi, ila naweza sema tenda wema bila kuchoka ila malipo si lazima (iwe kwa Mungu au kwa huyo ulomtendea wema). Waweza mtendea mtu wema na akakulipa mabaya vile vile, hii ndio dunia kama ulikuwa hujaijua.
Basi sawaaa, yangu ndio hayo.