Usimlaumu mkeo kuwa hazai/tasa

Gerald Robert

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
337
219
Umemuacha mke wako kwa tuhuma kwamba hazai (tasa). Mwanamke huyo huyo uliyemtuhumu kwamba hazai na ukaamua kumuacha, kwasasa ni mjamzito baada ya kuolewa na mwanamume mwingine.

Je kama wewe ndiye huyo mwanamume aliye acha mke, utajisikiaje pindi utakapotambua kwamba mke uliye muacha sasa anaujauzito?
===========================

USHAURI WANGU.

Pindi wanandoa mnaposhindwa kupata watoto katika ndoa yenu si busara kabisa kumshutumu mke kwamba hazai au ni tasa.

Ni vema nyote wawili muwaone wataalamu wa afya na mfanyiwe vipimo vya afya. Kutokupata mtoto kunaweza kuwa ni tatizo kwa upande wa mwanamke au mwanamume, au nyote wawili.

Tatizo laweza kuwa ni mbegu za kiume (kwa mwanamume) au via vya uzazi kwa mwanamke, nk kwahiyo ni vema sana nyote wawili kufanyiwa vipo vya afya vya kitaalamu. Damu (Blood) kwakawaida huwa katika makundi (Blood group)

Haya makundi ya damu pia husababisha wanandoa kutopata watoto, kuna baadhi ya blood group zikitofautiana baina ya mume na mke, wawili hawataweza kupata watoto kabisa (isipokuwa ni kwa neema tu)

Kwahiyo kwa wale ambao bado hawajaoana ni vyema sana kuwaona wataalamu wa afya ili kuangalia makundi ya damu zao kama zitawawezesha kupata watoto pindi watakapo oana.

Kama kila kitu kiko sawasawa na hampati watoto, hapo ndipo mnapaswa kumuuliza Mungu kwa njia ya maombi.

NOTE: Unaweza ukawa na nguvu za kiume za kutosha kabisa kushiriki tendo la ndoa kikamilifu, lakini mbegu zako za kiume zikawa hazina uwezo wa kumfanya mwanamke apate ujauzito (mimba)

By Mtumishi Gerald Robert
 
Dah..asante mkuuu..yupo Rafiki yangu hajabahatika kupata Mtoto mwaka wa 12 ...lakini yupo na mkewe wanakaa vizuri Sana .na ukiwaona utafikiri wame owana Jana ...jinnsi wanavyo pendana..wamepima na kagundulikana mwanamke..mirija imeziba. Vibaya sana.na hatoweza kuzaa labda kwa kufanya ivf
.but mapenzi yako..utayaonea gere .
 
Waaambie wanitafute
 
Kama uko siriaz waambie wanitafute facebook kwa jina la Mtumishi Gerald Robert. Tutashauriana vema sana. Ahsante
 
Back
Top Bottom