Erick Richard R-Madrid
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 399
- 279
Yan ulomuajiri ankuwa na lain zake za uwakala....so anazungusha biashara yako kupitia laini zake....zako zinawekwa pemben...analipwa mshahara na kamishen anapewaInakuwaje hi?
Asante sana mkuu kwa maelezo yako hakika yamenipa mwanga sana wa usimamizi wa fedha (mihamala).Muelekeze kijana wako
awe mwepesi kuwatambua matapeli haraka sana
awe mwepesi kuzitambua fedha bandia
awe mwepesi kuhudumia wateja kwa haraka ili kuepusha msongamano
awe na kauli nzuri kwa wateja
awe mwepesi kubadirika kutokana na hali ya mteja
Kuhusu miamala inayoingia na kutoka KUNA LOG BOOK atakua anaandika kila muamala
Kuhusu miamala inayoingia na kutoka utaijua kutokana na mtaji wako na commission unayopata kwa mwezi hapa (huduma kwa wateja wanaweza kukusaidia)
Unavyoenda kuchukua commission unaweza ukaomba statement ya mwezi mzima kisha ukapiga hesabu.
Yan ulomuajiri ankuwa na lain zake za uwakala....so anazungusha biashara yako kupitia laini zake....zako zinawekwa pemben...analipwa mshahara na kamishen anapewa
Asante sana mkuu kwa ushauri, ubarikiwe sanaKwa upande wa Tigo pesa
Unaweza kuangalia kila siku kiasi kilichoingia na ukapata jumla ya commission kabla ya mwisho wa mwezi.
Mwambie kijana wako asipokee simu yoyote kutoka kwenye laini ya uwakala
Asije akarudisha hela kwa mtu aliekosea namba akatuma kwake amwambie mtu aliekosea awapigie Tigo wairudishe
Simu za uwakala asiziweke kwenye meza za wateja kwani mteja tapeli anaweza akaja na simu kama yake akambadirishia
Aangalie message iliyoingia baada ya kutoa hela kwani mteja anaweza akasema nataka nitoe 50000 akatoa 5000 kwa papara zake akampa 50000
Na pia kuhusu kuibiwa na kijana wa kazi siku hizi vijana wa kazi wala hawakuibii pesa ila wanakuibia wateja, kuna wateja wengine huwa wanahitaji msaada wa kutolewa fedha, anachofanya kama mteja anataka kutoa elf 10 mteja atakatwa 1400 anachofanya ni kujitumia kwenye simu yake 11080 mteja atakatwa 320 kijana atapa 1080 ya papo kwa papo akipata watu 10 Kwa siku anapata si chini ya Tsh 7000 kwa siku akifanya kwa mwezi ana pesa nzuri pamoja na mshahahara. Anachofanya zile hela ni kuzitoa kwa pamoja jioni kabla hujafunga nae Hesabu,
Hapo nimezungumzia Tigo pesa ambayo nina uzoefu nayo
Good ila mshahara ni vema uwe fixed amount maana unaweza kuwa unamlipa haridhiki akakufanyia vitimbi Binafsi namlipa kwa asilimia yaani akipiga kamisheni analipwa 30% yakeThanks, nimeanza kwa kumwambia nitamlipa kiasi kidogo cha mshahara. Kwa kuwa ndo mwanzo ila kadri biashara itakavyo kuwa nzuri kwa juhudi zake ndo mshahara wake utapanda zaidi.
Asante
Ushauri mzuri sana mkuu nitafanyia kazi hlo, unamlipa kutokana na namna anavyofanya kazi kwa juhudiGood ila mshahara ni vema uwe fixed amount maana unaweza kuwa unamlipa haridhiki akakufanyia vitimbi
Binafsi namlipa kwa asilimia yaani akipiga kamisheni analipwa 30% yake
Japo 30% nililenga kumpiga kampani kubwa jamaa kutokana na kuona life limempindia kiasi but ni mwaminifu so ukiweza mkakubaliana 25 % sio mbaya cos wewe huhangaiki uko ni juhudi zake kupata kizuri
AiseeKuna ujanja saiv unafanyika na unaemwajiri, akiwa kazin anazungusha flot kwenye lain zake na sio zako so mwisho wa mwez anapata faida kwa kutumia pesa zako na pia mshahara unamlipa, tunasema double chance!!!!
Nimependa jinsi ulivyoelezea, yani points zimeshiba.1 Kwanza mwombe Mungu maana biashara ya fedha ndiyo biashara ambayo kama huisimamii wewe mwenyewe au kuwa makini sana kwa msaada wa Mungu unaweza kulala tajiri ukaamka maskini kabisa.
2 Nakushauri umpe mkataba kabisa wala usimtazame usoni na hakikisha ana wadhamini ambao ni vema wawe ndugu zake wa damu hasa mama au baba maana pesa ina vituko sana hasa unapomwajiri mtu kwa kuchekacheka ati nimwaminifu.Imewahi kunitokea , mtu nimepigania katoka jela nikaamua kumpa kazi ili aweze kuendesha familia akaishia kubeti na kusepa na pesa zangu na sikuwa na namna ya kumdai kabisa.
3 Mfanyakazi akipoteza pesa mwambie azilipe papo hapo na kama unaweza hilo liwe ndani ya mkataba kabisa.Biashara hii ukichekacheka unapoteza pesa , mtu atakwambia hesabu haipo sawa kumbe katia mfukoni na tabia ikizidi anatoroka na milions of money au anakwambia kapata loss hata ya milion 4
4 Hakikisha una mtaji wa ziada wa kuweka katika biashara yako ili ikitokea umetapeliwa au imepotea kuasi unacover kusudi wateja wasikukimbie maana wanapenda uhakika wa pesa
5.Commission usipende kuiingiza kwenye mtaji .Watu wengi wanaanza na sh 1000000 , akiona anapata laki 4 kwa mwezi anaona heri awe anaiweka commision ndani ya mtaji ili iwe kubwa zaidi apate kamusheni bomba zaidi sasa ikitokea dharula unajikuta ushakuwa maskini na kijiwe kinakufa rasmi.
6 Mshahara anza na wa kawaida ila mfanyakazi akikuingizia pesa nzuri ya kupanda kila mwezi mwongeze bonus azidi kupiga kazi zaidi.Wengine wanasikia fulani anamlipa mfanyakazi wake Laki moja na wao wanawatamkia wa kwao kuwa ni laki moja kumbe mwenzako alishajua faida ya eneo lake labda ni laki 5 kupanda juu sasa wewe unamlipa laki moja na commission imeingia laki na nusu hapo ni taabu tu .
Ni hayo tu
Mzuri mno, tuendelee kuchota maarifa hapaUzi mzuri sana huu wazoefu endeleeni kushusha nondo
Wengine walete nondo basi na wengine wafaidikeMzuri mno, tuendelee kuchota maarifa hapa
Mm pia ninahitaji sana kujua njisi ya kupata commision , kwa wenye ufahamu tupatieni elimu jamani.sorry jaribu kupeleleza kiasi cha commision kwa kila muamala kabla ya kuanza hii biashara.....mwaka jana nmefanya mpesa lakn nkawa najikuta mwisho wa mwez nna commision ya 7000 nkaachana nayo....so n vema ukajua faida zake kwanza
Asante kaka kwa ushauri, japo ungetupa mwanga kidogo namna ambavyo commission inapatikana angalau kwa mtandao mmoja wapo hapo juu.sorry jaribu kupeleleza kiasi cha commision kwa kila muamala kabla ya kuanza hii biashara.....mwaka jana nmefanya mpesa lakn nkawa najikuta mwisho wa mwez nna commision ya 7000 nkaachana nayo....so n vema ukajua faida zake kwanza