Usimamizi wa biashara za kifedha

Erick Richard R-Madrid

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
399
279
Narudi kwenu wana jukwaa la Biashara, jukwaa lenye watu watashi wa kibiashara.

Nategemea kupata Line zangu za uwakala wa biashara za MPESA, TIGO PESA, AIRTEL mwishoni mwa mwezi huu wa 8, nimeshapata mtu wa kumuajiri tayari kuanza kazi kwa muda huo, pia eneo la biashara nishapata tayari kujenga fremu yangu ndogo.

Naomba kufahamu wenzangu (wana jukwaa) ambao wanafanya biashara hii na wameajiri watu wengine huwa wanafanyaje kujua na kuelewa mihamala inayoingia na kutoka (kwa usahihi).

Waweza pia kunipa mbinu na changamoto mbalimbali za kufanya biashara hii ili iweze kutusaidia wote na kuweza kuielewa na kutupatia faida sote pindi tutakapoianza.
Asanteni sana.

Pia kwa aliyena uzoefu wa hii biashara ya mihamala aweze kutupa mrejesho wa namna ambavyo commission zinapatikana, na namna ambavyo mtu anaweza kujua commission (kufanya mahesabu ya commissions) yake kabla ya muda wa malipo kufika.[/B]
 
Muelekeze kijana wako
awe mwepesi kuwatambua matapeli haraka sana
awe mwepesi kuzitambua fedha bandia
awe mwepesi kuhudumia wateja kwa haraka ili kuepusha msongamano
awe na kauli nzuri kwa wateja
awe mwepesi kubadirika kutokana na hali ya mteja

Kuhusu miamala inayoingia na kutoka KUNA LOG BOOK atakua anaandika kila muamala
Kuhusu miamala inayoingia na kutoka utaijua kutokana na mtaji wako na commission unayopata kwa mwezi hapa (huduma kwa wateja wanaweza kukusaidia)
Unavyoenda kuchukua commission unaweza ukaomba statement ya mwezi mzima kisha ukapiga hesabu.
 
Asante sana mkuu kwa maelezo yako hakika yamenipa mwanga sana wa usimamizi wa fedha (mihamala).

Sikuwa nafahamu kuwa naweza kupata msaada kupitia mtandao husika.

Asante.
 
Kwa upande wa Tigo pesa

Unaweza kuangalia kila siku kiasi kilichoingia na ukapata jumla ya commission kabla ya mwisho wa mwezi.

Mwambie kijana wako asipokee simu yoyote kutoka kwenye laini ya uwakala

Asije akarudisha hela kwa mtu aliekosea namba akatuma kwake amwambie mtu aliekosea awapigie Tigo wairudishe

Simu za uwakala asiziweke kwenye meza za wateja kwani mteja tapeli anaweza akaja na simu kama yake akambadirishia

Aangalie message iliyoingia baada ya kutoa hela kwani mteja anaweza akasema nataka nitoe 50000 akatoa 5000 kwa papara zake akampa 50000

Na pia kuhusu kuibiwa na kijana wa kazi siku hizi vijana wa kazi wala hawakuibii pesa ila wanakuibia wateja, kuna wateja wengine huwa wanahitaji msaada wa kutolewa fedha, anachofanya kama mteja anataka kutoa elf 10 mteja atakatwa 1400 anachofanya ni kujitumia kwenye simu yake 11080 mteja atakatwa 320 kijana atapa 1080 ya papo kwa papo akipata watu 10 Kwa siku anapata si chini ya Tsh 7000 kwa siku akifanya kwa mwezi ana pesa nzuri pamoja na mshahahara. Anachofanya zile hela ni kuzitoa kwa pamoja jioni kabla hujafunga nae Hesabu,

Hapo nimezungumzia Tigo pesa ambayo nina uzoefu nayo
 
1 Kwanza mwombe Mungu maana biashara ya fedha ndiyo biashara ambayo kama huisimamii wewe mwenyewe au kuwa makini sana kwa msaada wa Mungu unaweza kulala tajiri ukaamka maskini kabisa.

2 Nakushauri umpe mkataba kabisa wala usimtazame usoni na hakikisha ana wadhamini ambao ni vema wawe ndugu zake wa damu hasa mama au baba maana pesa ina vituko sana hasa unapomwajiri mtu kwa kuchekacheka ati nimwaminifu.Imewahi kunitokea , mtu nimepigania katoka jela nikaamua kumpa kazi ili aweze kuendesha familia akaishia kubeti na kusepa na pesa zangu na sikuwa na namna ya kumdai kabisa.

3 Mfanyakazi akipoteza pesa mwambie azilipe papo hapo na kama unaweza hilo liwe ndani ya mkataba kabisa.Biashara hii ukichekacheka unapoteza pesa , mtu atakwambia hesabu haipo sawa kumbe katia mfukoni na tabia ikizidi anatoroka na milions of money au anakwambia kapata loss hata ya milion 4

4 Hakikisha una mtaji wa ziada wa kuweka katika biashara yako ili ikitokea umetapeliwa au imepotea kuasi unacover kusudi wateja wasikukimbie maana wanapenda uhakika wa pesa

5.Commission usipende kuiingiza kwenye mtaji .Watu wengi wanaanza na sh 1000000 , akiona anapata laki 4 kwa mwezi anaona heri awe anaiweka commision ndani ya mtaji ili iwe kubwa zaidi apate kamusheni bomba zaidi sasa ikitokea dharula unajikuta ushakuwa maskini na kijiwe kinakufa rasmi.

6 Mshahara anza na wa kawaida ila mfanyakazi akikuingizia pesa nzuri ya kupanda kila mwezi mwongeze bonus azidi kupiga kazi zaidi.Wengine wanasikia fulani anamlipa mfanyakazi wake Laki moja na wao wanawatamkia wa kwao kuwa ni laki moja kumbe mwenzako alishajua faida ya eneo lake labda ni laki 5 kupanda juu sasa wewe unamlipa laki moja na commission imeingia laki na nusu hapo ni taabu tu .

Ni hayo tu
 
Asante sana mkuu kwa ushauri, ubarikiwe sana
 
Thanks, nimeanza kwa kumwambia nitamlipa kiasi kidogo cha mshahara. Kwa kuwa ndo mwanzo ila kadri biashara itakavyo kuwa nzuri kwa juhudi zake ndo mshahara wake utapanda zaidi.

Asante
Good ila mshahara ni vema uwe fixed amount maana unaweza kuwa unamlipa haridhiki akakufanyia vitimbi Binafsi namlipa kwa asilimia yaani akipiga kamisheni analipwa 30% yake
Japo 30% nililenga kumpiga kampani kubwa jamaa kutokana na kuona life limempindia kiasi but ni mwaminifu so ukiweza mkakubaliana 25 % sio mbaya cos wewe huhangaiki uko ni juhudi zake kupata kizuri
 
Good ila mshahara ni vema uwe fixed amount maana unaweza kuwa unamlipa haridhiki akakufanyia vitimbi
Binafsi namlipa kwa asilimia yaani akipiga kamisheni analipwa 30% yake
Japo 30% nililenga kumpiga kampani kubwa jamaa kutokana na kuona life limempindia kiasi but ni mwaminifu so ukiweza mkakubaliana 25 % sio mbaya cos wewe huhangaiki uko ni juhudi zake kupata kizuri
Ushauri mzuri sana mkuu nitafanyia kazi hlo, unamlipa kutokana na namna anavyofanya kazi kwa juhudi

Asante mkuu kwa ushauri
 
1 Kwanza mwombe Mungu maana biashara ya fedha ndiyo biashara ambayo kama huisimamii wewe mwenyewe au kuwa makini sana kwa msaada wa Mungu unaweza kulala tajiri ukaamka maskini kabisa.

2 Nakushauri umpe mkataba kabisa wala usimtazame usoni na hakikisha ana wadhamini ambao ni vema wawe ndugu zake wa damu hasa mama au baba maana pesa ina vituko sana hasa unapomwajiri mtu kwa kuchekacheka ati nimwaminifu.Imewahi kunitokea , mtu nimepigania katoka jela nikaamua kumpa kazi ili aweze kuendesha familia akaishia kubeti na kusepa na pesa zangu na sikuwa na namna ya kumdai kabisa.

3 Mfanyakazi akipoteza pesa mwambie azilipe papo hapo na kama unaweza hilo liwe ndani ya mkataba kabisa.Biashara hii ukichekacheka unapoteza pesa , mtu atakwambia hesabu haipo sawa kumbe katia mfukoni na tabia ikizidi anatoroka na milions of money au anakwambia kapata loss hata ya milion 4

4 Hakikisha una mtaji wa ziada wa kuweka katika biashara yako ili ikitokea umetapeliwa au imepotea kuasi unacover kusudi wateja wasikukimbie maana wanapenda uhakika wa pesa

5.Commission usipende kuiingiza kwenye mtaji .Watu wengi wanaanza na sh 1000000 , akiona anapata laki 4 kwa mwezi anaona heri awe anaiweka commision ndani ya mtaji ili iwe kubwa zaidi apate kamusheni bomba zaidi sasa ikitokea dharula unajikuta ushakuwa maskini na kijiwe kinakufa rasmi.

6 Mshahara anza na wa kawaida ila mfanyakazi akikuingizia pesa nzuri ya kupanda kila mwezi mwongeze bonus azidi kupiga kazi zaidi.Wengine wanasikia fulani anamlipa mfanyakazi wake Laki moja na wao wanawatamkia wa kwao kuwa ni laki moja kumbe mwenzako alishajua faida ya eneo lake labda ni laki 5 kupanda juu sasa wewe unamlipa laki moja na commission imeingia laki na nusu hapo ni taabu tu .

Ni hayo tu
Nimependa jinsi ulivyoelezea, yani points zimeshiba.
Be Blessed mkuu🤝
 
Sorry jaribu kupeleleza kiasi cha commision kwa kila muamala kabla ya kuanza hii biashara.....mwaka jana nmefanya mpesa lakn nkawa najikuta mwisho wa mwez nna commision ya 7000 nkaachana nayo....so n vema ukajua faida zake kwanza
 
sorry jaribu kupeleleza kiasi cha commision kwa kila muamala kabla ya kuanza hii biashara.....mwaka jana nmefanya mpesa lakn nkawa najikuta mwisho wa mwez nna commision ya 7000 nkaachana nayo....so n vema ukajua faida zake kwanza
Mm pia ninahitaji sana kujua njisi ya kupata commision , kwa wenye ufahamu tupatieni elimu jamani.
 
sorry jaribu kupeleleza kiasi cha commision kwa kila muamala kabla ya kuanza hii biashara.....mwaka jana nmefanya mpesa lakn nkawa najikuta mwisho wa mwez nna commision ya 7000 nkaachana nayo....so n vema ukajua faida zake kwanza
Asante kaka kwa ushauri, japo ungetupa mwanga kidogo namna ambavyo commission inapatikana angalau kwa mtandao mmoja wapo hapo juu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom