Usilolijua kuhusu wawindaji haramu

kambagasa

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
2,261
1,785
Ni leo jumapili nimemtembelea rafiki yangu (ananizidi umri ila huwa tunabadirishana mawazo hasa mambo ya bustani). Nilifika nikamkuta pekee yake wife wake akiwa ameenda kwao Kigoma. Namuuliza ulimpataje shemu huko Kigoma wakati wewe ukiwa Msukuma wa Kahama? Ananijibu alimfuata baba yake ambaye alimfuata mke wa pili mwenyeji wa huko na akajiingiza katika uwindaji haramu miaka ya 1996 kipindi cha Mkapa.
MAHITAJI YA KUCHUKUA:
Chakula hasa unga,chumvi,vyombo,panga,shoka,visu na bunduki aina ya rifle,shotgun hawakuwa wanaitumia sababu haina nguvu za kumuweza tembo.

NAMNA YA KUWINDA TEMBO
Walikuwa wanavizia muda wa asubuhi kwenye mabwawa natural yaliyoko hifadhini. Pia hufuatilia sauti na kukwepa ulelekeo wa upepo kwa kuwa ukisimama upande unakotokea upepo tembo hunasa harufu na hivyo kuaza kujihami. Baada ya kuua tembo ndipo harakati za kung'oa meno huanza kwa kukata nyama iliyopo kwenye maungio na kutumia shoka imara. Kipindi hicho cha Mkapa walikuwa huru sana kwani walikuwa wakiua na kutoa meno kazi kubwa ilikuwa kutoka hifadhini na ukivuka tu mpaka upande wa Burundi unakuwa salama kiasi kwamba mnaweza kulibeba mabegani pasipo wasiwasi wowote na kuwakuta matajiri wakisubiri na kuyasafirisha Congo.
KUSALITIANA
Hatari iliyokuwa inawakumba hawa majangiri (jangiri mstaafu) ni makundi ya wawindaji haramu kuvamiana kwa lengo la kunyang'anyana meno hasa kama hamfahamiani na kama hilo kundi limekosa tembo na lina order ya pesa nyingi. Hapo kupigwa risasi na kufa ni jambo la kawaida sawa na wafanyabiashara wa dhahabu,Tanzanite na Almasi.

FAIDA ALIYOPATA:
Hajaona faida yoyote zaidi ya nyama,pombe na wanawake
 
Back
Top Bottom