Mwakaboko King
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 1,099
- 207
Habari za majukumu wanabodi, naamini tumekuwa pamoja katika mada mbalimbali za maswala yahusuyo Chaguzi nchini Tanzania. Nikiwa mmoja wa wafuatiliaji wa Siasa za Tanzania na hasa chaguzi mbalimbali naomba tujikumbushe kuhusu MCHAKATO WA UCHAGUZI NCHINI TANZANIA.
Kama tujuavyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania ndiyo yenye Mamlaka ya kusimamia na kuendesha chaguzi za Urais, Ubunge na Udiwani kwa Tanzania Bara. Vilevile ina jukumu la Kusimamia Sheria za Uchaguzi, Uandikishaji wa Wapiga Kura pamoja na Uboreshaji wa wa Daftari la Wapiga Kura.
Katika kuendesha chaguzi hizo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) huteua watu kwa nyadhifa zao na sifa zinazotakiwa ili waweze kusimamia Uchaguzi katika maeneo yao, watu hawa ni pamoja na Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mtumishi wa Umma ambaye husimamia shughuli zote za Uchaguzi katika ngazi za majimbo. Wengine ni Wasimamizi wasaidizi na wasimamizi wa Vituo vya kupigia Kura ambao husimamia upigaji wa Kura katika Kata zao na katika vituo vya kupigia Kura.
Tuangalie mambo mbalimbali ambayo hufanyika kwenye Mchakato wa Uchaguzi;-
Uandikishaji wa Wapiga Kura - Kama tunavyojua uchaguzi ulio Huru ni lazima utoe fursa kwa kila mwananchi kujiandikisha ili aweze kupiga kura. Kama mnakumbuka Tanzania ilifanya zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hili lilikua zoezi muhimu sana katika kufanikisha uchaguzi ulio Huru na wa Haki, ipo mifano mingi ya baadhi ya nchi ambazo hazikufanya vizuri katika chaguzi au zimeshindwa kufanya chaguzi kwa sababu tu wananchi wa nchi hizo hawakuandikishwa.
Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura, Uboreshaji wa Daftari la Wapiga hufanyika ili kuondoa wananchi waliofariki, kufanya marekebisho kwa wananchi waliohama kutoka eneo moja kwenda jingine, Wananchi waliokosa sifa au kupoteza Kadi zao za kupigia Kura kupatiwa kadi nyingine kuwawezesha kupiga Kura wakati wa Uchaguzi. Hivyo kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 kutakuwa na Uboreshaji wa Daftari hilo ili kutoa fursa kwa wananchi wenye sifa ambao hawakujiandikisha au kupiga Kura mwaka 2015 waweze kupiga Kura katika uchaguzi ujao.
Jambo la msingi hapa ni kwamba mara baada ya uboreshaji, Daftari hilo hupelekwa kwenye Majimbo na Kata kwa ajili ya kuwekwa wazi ili wananchi wakague kama taarifa walizotoa ni sahihi na zimeingizwa kama walivyojieleza.
Uteuzi wa Wagombea, Kazi ya uteuzi wa wagombea hufanywa ndani ya Vyama vya Siasa, kwa mujibu wa Sheria vyama vya Siasa vilivyopata Usajili wa kudumu vinaweza kuwasilisha jina la mgombea Urais na Makamu wa Rais kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na jina la mgombea Ubunge na Udiwani kwa Msimamizi na Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi kulingana na siku au muda uliotangazwa na Tume.
Kwa leo naomba tuishie hapa mada hii itaendelea,
Nawasilisha.