Kuna zoezi linaloendelea kwa ajili ya uandikishaji wa daftari la wapiga kura wa Serikali za Mitaa.
Kila mahali kuna malalamiko dhidi ya waandikishaji wa zoezi hili wakikipendelea Chama fulani.
Malalmiko ya Dodoma Jiji ndiyo funga kazi. Kuna vijiwe vinaandikisha watu hewa na hakuna kinachofanyika.
Kuna mwandikishaji anaandika wapiga kura na anaacha nafasi katikati kwa ajili ya kujaza wapiga kura anaowajua na hakuna kinachofanyika. Kinachotakiwa haki itendeke na mambo ya hila hayatakiwi katika zoezi hili.
Jana nimemuona Mzee Butiku katika kipindi cha dakika 45 alisisitiza kuwa viongozi wapatikane kwa njia ya haki na siyo kwa njia ya mlango wa nyuma.
Zoezi hili limegubikwa na kasoro kubwa kwa ajili ya kuipendelea Chama fulani.
Kwanini wapiga kura wasingetumia tu kadi zao za kupigia kura na kama kuna vijana waliotimiza miaka 18 basi wakati wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura wangepewa kadi zao za kupigia kura ili nao waje kutumia kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa.
Inasikitisha sana kama Serikali inaona mambo haya na haichukui hatua.