Usilishangae anguko la ndoa. Sababu ni hii

Diwani

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2014
Posts
2,825
Reaction score
3,021
Katika karne hii ya 21 kumekuwa na manung'uniko mengi sana kuhusu changamoto zinazoikumba ndoa na malalamiko ya watu ni juu ya nini kimetokea kwenye ndoa. Mbona zama hizi ndoa zinaanguka na kuna ongezeko kubwa la madai ya talaka na kudhoofika kwa taasisi hii?

Wengi wanazungumzia sababu zao kijamii, wanasahau ndoa kwa asili yake kwenye nyanja ya uchumi.

Zamani ndoa zilikuwa ni taasisi zilizoasisiwa na mfumo wa kijima; hivyo ndoa ilikuwa na lengo la kutengeneza Familia imara ambapo familia ndiyo ilikuwa chanzo cha na msingi wa nguvukazi katika maendeleo ya kiuchumi na uwepo (survival) ya jamii husika. Ebu fikiria, unajua kama kuna wakati jamii zetu zilikuwa zikiishi chini ya mfumo wa Kijima ambapo watu walihitajika wengi kwa ajili ya uzalishaji? Hii ina maana kuwa, bila familia kusingewezekana kuwepo vijiji, miji na hata majiji, na familia ilihitajika kwa ajili ya kujenga mfumo imara wa uzalishaji mali kwenye Kilimo, Ufugaji, biashara na hata usimamizi rasilimali (siasa).

Kwa kutambua jambo hili, ndoa ndiyo ilikuwa 'base" ya familia imara; ambapo mfumo mzima wa elimu na mafunzo wa wakati huo ulikuwa umelenga katika kujenga jamii yenye kuheshimu na kuthamini ndoa kwa sababu ndio msingi wa familia na bila familia kusingekuwapo na jamii yoyote iliyopo leo hii.

Kupitia jando, unyago, na kwa baadhi ya jamii kufunda; mfumo wa elimu ulizingatia ndoa na juzi mbali mbali za uzalishaji (practical skills); lengo likiwa kujenga na kuimarisha familia. Hivyo, Watoto wa kiume walifunzwa kuwa Wame/baba wa baadae, na watoto wa kike walifunzwa kuwa Wake/mama wa badae kupitia miundo hiyo ya elimu. Ndio mana waliishi chini ya muundo maalumu (defined order) ambapo baba alikuwa kiranja wa familia na aliongoza mfumo mzima wa uzalishaji.

SIKU HIZI; mambo yamekuwa tofauti, makundi ya uzalishaji si familia tena, bali Kampuni. Na hii ni baada ya kuanza kwa mfumo wa Kibepari ambapo, familia si msingi wa uzalishaji bali Mtaji. Hata hivyo, mifumo ya elimu ya zama hizi haziandai tena mtu kuwa 'Marital individual' yaani mtu anayethamini na kulinda ndoa kama taasisi nyeti ya kuanzisha familia kwa ajili ya 'community survival' kupitia uzalishaji.

Leo tunashuhudia kuwapo kwa watu, hususan wasomi ambao wanajituma zaidi kwenye ofisi zao za kazi kuliko kwenye familia zao, kwa sababu; mfumo wa uzalishaji wa zama hizi unategemea zaidi nguvukazi ya mtu binafsi (Individualism) kuliko familia kwa ujumla.

Kijamii, mfumo wa Kibepari umetengeneza watu wanaothamini zaidi nyezo walizonazo, na nafsi zao pekee na si kundi (nje ya kampuni, shirika, taasisi au kiwanda); hivyo basi hisia za ndoa, zimeanguka kwa sababu kubwa. Anguko la ndoa ndilo sababu ya anguko la familia.

Mwisho kabisa, kuna suala zima la mabadiliko ya majukumu ya kijinsia; kutokana na mabadiliko ya ki-majukumu kati ya Mwanamke na Mwanaume, ndoa imepoteza mantiki ya kuwa taasisi, bali kwa sasa ni mtindo wa maisha tu (life style).

Hivyo basi. Mfumo wa uchumi, ndio hujenga mfumo wa Kijamii. Ubepari ambao ndio mzizi wa Individualism umepunguza hitaji la ndoa kwenye uzalishaji, ila mtu binafsi tu.

Kila la heri.
 
Zamani mwanamke alikua akiamka kwanza anawasha moto, tofauti na hawa wa sasa wakiamka kwanza wanawasha data....🤥
🤣🤣🤣🤣 Wanaume walikuwa wakiamka wanawasha nini?

Ila siku hizi mtu hata kabla hajakagua miguu kama kaamka mzima au kapooza, anawasha data kwanza
 
No reform No election.we ushaona mume wa rais tz kawa kundi la wanawake wa raisi
 
Kwamba hitaji la ndoa limepungua sio kweli,hebu niambieni kila jmosi huko kwenye miji yetu hamuoni misururu ya magari barabarani yakisindikiza ndoa? ,hivi hamuoni kwenye ma pub mbalimbali vikao vya harusi?
 
Sio wake, ni wenza wa Rais na viongozi.
Ila Yule Baba aheshimiwe, kama mkewe ananyoosha watu hivi....mijanaume inalia ila akifika kwake lile jicho linalegea.
 
🤣🤣🤣🤣 Wanaume walikuwa wakiamka wanawasha nini?

Ila siku hizi mtu hata kabla hajakagua miguu kama kaamka mzima au kapooza, anawasha data kwanza
Wanaume wa zamani tuliamka saa kumi na moja alfajiri hata kama hauna ajira unaingia mtaani kutafuta kibarua.
Hawa wa skuizi ni wavivu na wakishapata degree wanaanza kulalamika hawana ajira...🤨
 
Kwamba hitaji la ndoa limepungua sio kweli,hebu niambieni kila jmosi huko kwenye miji yetu hamuoni misururu ya magari barabarani yakisindikiza ndoa? ,hivi hamuoni kwenye ma pub mbalimbali vikao vya harusi?
Jesus. Unafananisha na idadi ya watu? Au unadanganywa na hizo kelele? Hizo ndoa zinazofungwa. 47% zinaanguka kati ya miaka 2-5. 28% zina last mpaka miaka 15 na 20% mpaka miaka 25 na 5% mpaka kufikia 30-38

Usidanganywe na hizo kelele.
 
Sio wake, ni wenza wa Rais na viongozi.
Ila Yule Baba aheshimiwe, kama mkewe ananyoosha watu hivi....mijanaume inalia ila akifika kwake lile jicho linalegea.
Inaonekana una men's issues
 
Kwamba hitaji la ndoa limepungua sio kweli,hebu niambieni kila jmosi huko kwenye miji yetu hamuoni misururu ya magari barabarani yakisindikiza ndoa? ,hivi hamuoni kwenye ma pub mbalimbali vikao vya harusi?
Hizo ni harusi sio ndoa,ndoa ni maisha baada ya hiyo harusi kuisha.
Ndoa nyingi huwa zinakufa kabla ya miaka 3 kuisha.
 
Marriage is a scam. Enter at your own risk.
 
Back
Top Bottom