Mitchell
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 944
- 1,103
Mama mmoja mcha Mungu alikuwa na jirani yake mwenye roho mbaya kupita kiasi, siku moja akafungulia mabata yake ili yakajitafutie chakula. Bahati mbaya yakaenda kwa jirani yake, jirani kuyaona akayapiga mabata yote matano na kuyajeruhi vibaya sana. Yakajikokota yakarudi nyumbani yakiwa hoi sana mama mcha Mungu kuona vile akaona ni vema ayachinje ili yasije kufa. Basi baada ya kuyachinja akayatengeneza, akayaweka kwenye friji kisha akachukua mabata mawili akayafunga vizuri na kumpelekea jirani : Jirani haya mabata yamepigwa huko mtaani bila huruma na yaliumia vibaya hivyo nimeona niyachinje ila yalikuwa mengi hivyo na wewe chukua haya upate kitoweo jirani yangu.