Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,232
- 1,741
Yer 40:16 SUV
[16] Lakini Gedalia, mwana wa Ahikamu, akamwambia Yohana, mwana wa Karea, Usilitende jambo hili, maana unamsingizia Ishmaeli.
Gedalia alikuwa kiongozi mzuri tu, aliletewa onyo la tahadhari ya kutaka kuuwawa kwake, lakini akalipuuza onyo hilo na kuona ni uzushi tu unaovumishwa na watu, lakini baadaye aliuawawa.
Kifo chake kilileta maumivu makubwa kwa watu wa Mungu, maana lilikuwa ni tukio baya la kupoteza kiongozi wao, jambo ambalo angeweza kuchukua tahadhari asingekufa.
Huyu Gedalia alikuwa ni mtawala au kiongozi aliyewekwa na Wababeli baada ya kuanguka Yerusalemu, katika uongozi wake alipokea taarifa kutoka kwa Yohana mwana wa Karea kuwa Ishmaeli alikuwa anapanga njama za kumuua.
Kama nilivyotangulia kusema taarifa hii Gedalia hakuizingatia sana zaidi aliona ni uzushi tu wa watu, lakini haikuwa hivyo maana tunaona katika sura inayofuata aliuwawa kweli.
Yer 41:1-2 SUV
[1] Basi ikawa katika mwezi wa saba, Ishmaeli, mwana wa Nethania, mwana wa Elishama, mmoja wa wazao wa kifalme, tena ni mmoja wa majemadari wa mfalme, na watu kumi pamoja naye, wakamwendea Gedalia, mwana wa Ahikamu, huko Mizpa; nao walikula chakula pamoja huko Mizpa. [2] Akaondoka huyo Ishmaeli, mwana wa Nethania, na watu wale kumi waliokuwa pamoja naye, wakampiga Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, kwa upanga, wakamwua; yeye ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa liwali wa nchi.
Badala ya Gedalia kuwa kiongozi mwema kwa yale mabaki ya watu waliobakia, kwa kukosa kwake tahadhari aliyopewa, aliwaacha watu wake katika hali mbaya ya huzuni baada ya kifo chake.
Tunapaswa kusikiliza mashauri au tahadhari tunazopewa na watu, kweli tunaweza kukutana na taarifa za uzushi, lakini haipaswi kutufanya tupuuze kila taarifa. Zipo tahadhari zinatufikia kwa nia ya kutusaidia, hatupaswi kuzichukulia kawaida.
Kosa alilolifanya Gedalia, ndio kosa linalofanywa leo na viongozi wengi, hupuuza sauti ya MUNGU zinazowajia kupitia watumishi wengine wa Mungu.
Gedalia ni mfano halisi wa kiongozi wa leo asiye na utambuzi wa kiroho, anaweza akawa kiongozi mzuri sana ila akakosa kutambua taarifa muhimu anazopata kupitia kwa watumishi wa Mungu au kwa watu wanaomcha Mungu katika roho na kweli.
Tunaaswa na neno la Mungu kuzijaribu kila roho, zipo tahadhari zinaweza zikawa na nia mbaya za kututia hofu ila hazina ukweli wowote. Tunapaswa kuelewa pia zipo tahadhari zinaweza zikawa na ukweli, ila tukazipuuza.
1 Yoh 4:1 SUV
[1] Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
Hapa tunapata tahadhari za kuzipima nabii au taarifa au tahadhari tunazopewa, ila hapa tunajifunza kutotambua tadhahari au onyo juu ya hatari iliopo mbele yetu ilivyo na madhara makubwa kwetu.
Tunaweza kupata watu wetu wa karibu na kujionyesha kwetu ni marafiki wa kweli kama alivyofanya Ishmaeli, lakini wakawa na nia ovu juu yetu na wakatuangamiza kama walivyofanya kwa Gedalia.
Sio kila rafiki anayejifanya ni rafiki yako wa kweli anaweza akawa hivyo kweli, unahitaji hekima ya ki-Mungu uweze kutambua rafiki uliyenaye sio sahihi au ni sahihi. Na unapopewa tahadhari juu ya rafiki yako usichukulie wakati wote ni uzushi.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana