Huoni tatizo hapo
Yaani mwalimu anakuwa kwenye Box la kujifunza kuanzisha shule yake tu.
Lakini Carrier kama muhasibu anaweza ajiriwa kampuni yeyote ile ya Logistics, Mining, Heath, Technology...Hana Box anapata Knowledge ya kuanzisha any kind of Company inayodili na chochote kile na kuwa na knowledge pana jinsi ya kuwa manage Officers mbalimbali HR, Wahasibu, Marketing department nk nk kwasababu hivi ni vitu common kwenye masuala ya kampuni ambapo most Accountant wanakula shavu huko.
sasa huyu mwalimu yeye shavu lake anakula Mtombo Sec kibaha buyuni huko hawi experienced na shughuri zozote za kikampuni HR, Marketing team nk Shule nyingi hazina hizi ishu.
Sijui umenielewa ila kimsingi Carrier kama uwalimu changamoto sana.
Mkuu usiwafunge waalimu, nao wana fursa kama ilivyo kwenye field zingine.
Unapojifunza kitu tunategemea ukatumie knowledge yako sasa kutegemeana na kile ulichojifunza ili kupata unachokitaka.
Unaposoma kitabu na kukimaliza kitabu hucho huwa hakihitajiki tena na kinachobaki kichwani ndiyo kinachohitajika (knowledge) ili kuingia katika utendaji.
Sikuwa na maana kuwa ni lazima ukaanzishe aina ya kampuni uliyopo kwasababu umejifunza namna ya utendaji kupitia kampuni hiyo.
Knowledge unayoipata unaweza kuitumia kuanzisha chochote kile ilimradi uwe na nia ya dhati kufanya hicho unachotaka kukifanya. Pia kumbuka huwezi jifunza kupitia kampuni moja na ukafanikiwa kila kitu.
Lazima ujue unataka nini? Na kwenye kampuni hii nitapata nini? Lakini pia ujue nini utahitaji na hakipatikani katika kampuni hii? Na lazima ujue wapi au kwa nani naweza kupata kitu hicho?
Mwalimu kupitia ofisi yake kuna taratibu za jumla ambazo anaweza kuelewa na ikamsaidia, kwa mfano uelewa juu ya taratibu za ulipaji mshahara kwa wafanyakazi, sheria zinazotumika kuanzisha taasisi binafsi hasa shule, haki za msingi za mfanyakazi na mengine pia.
Turudi kwenye suala la mwalimu kutokuwa na uwezo wa kuanzisha kampuni zingine tofauti na shule, hili jambo siyo kweli.
Engineer anaweza Fanya kazi kwenye kampuni ya magari na yeye siyo kwamba kile atakachojifunza pale ndicho atakachohitaji ili kuanzisha kampuni yake. Kuna masuala ya sheria hili halichagui mwalimu wala doctor ni lazima kufuata sheria hitajika ili uweze kufanya shughuli husika.
Hivyo niseme tu, kila mmoja katika kampuni husika ana nafasi ya kujifunza namna ya uendeshaji na background ya kampuni husika SIYO kwa lengo la kuandaa kampuni kama hiyo, hapana. Ila kwa lengo la kupata uelewa wa namna jinsi watu wanavyoanza mpaka kufanikiwa sasa kuanzia hapo unaweza amua nianzishe kampuni kama hiyo au nyingine tofauti.
Lakini faida inakuja kiujumla kuwa unayo basic knowledge ya uendeshaji wa biashara, tahisisi au kampuni ya aina fulani kwasababu umekuwa sehemu ya kampuni hiyo na umeshuhudia na kujifunza.
Dhana ya waalimu kuwa na uwanja mdogo siyo kweli. Wapo watu kama akina MSUKUMA wanamiliki kampuni za mabasi na ni darasa la saba, inakuaje wewe mtu was degree unalalamikia field yako?
Hapo ndipo nguvu ya mtazamo inapokuja kuwa na athari katika maisha yako kiujumla na kujitengenezea dhana kuwa haiwezekani na kweli haitowezekana.