Usijipe tabu ya kutoa matusi kwa comments kwenye mitandao, kama hupendi post za mtu usimfollow, unfollow

askarikambi

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
246
263
Kuna kitu huwa kinanishangaza sana nikipitaga Instagram.
Kuna watu utakuta wamemfollow mtu/msanii, kuonyesha kuwa wanataka kupata habari juu ya msanii au mtu yule. Hii ni kuonyesha kuwa "wanavutiwa" naye.
Sasa mshangao wangu, ni jinsi wale followers wanavyo comments vibaya kwenye picha au video anazotuma yule msanii.
Wengine wakilaumu kuwa anachofanya kinawachefua, wengine wanadai hapendezi, wengine eti unauza, kauze mbele, n.k.
Huwa najiuliza, na labda mnisaidie, hivi utawezaje kuona page ya mtu hadi uchefukwe na kurusha matusi pasipo kumfollow?
Kwann uingie kwenye page ya mtu ambaye hupendi vitu anavyopost hadi ukerekwe na vilivyomo upate tabu ya kurusha matusi?
Kama uliingia kimakosa, kwann usi-unfollow?
Najua wengine mko humu JF, kwann mteseke?
Au inawezekana kwa page ya mtu kuja tu pasipo kumfollow?
Acha nishauri wale waliomo humu.
Usijipe tabu ya kutoa matusi kwa comments kwenye mitandao, kama hupendi post za mtu usimfollow, unfollow.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom