Usije juta kupitia makosa haya

Machmadem

JF-Expert Member
Jul 9, 2017
758
933
Habar za weekend zangu JF

Kwa jinsi maisha yanavyokwenda kasi zaid ya ile ya mwanga haya ni baadhi ya mambo ambayo hutakiwi kupitia na kama umepitia basi hakikisha hurudii.

1. Matumizi mabaya ya pesa
2. Kusoma ndio maisha
3. Kukata tamaa bila kujaribu
4. Kukubali kila unachosikia/ambiwa
5. Kuwekeza bila utafiti
6. Kutaka/kufanya Mambo mengi kwa wkt mmoja
7.Kutokuchagua mtu sahihi ktk mahusiano yako.

Karibuni kuchangia pamoja tupeane madini kuna watu walisha experience ayo mambo unaweza kuongezea nyama.
 
1. Fafanua zaidi, yapi ni matumizi mabaya na kwa watu wa aina gani? Mf: mimi mwenye kipato cha laki moja kwa mwezi, nikihonga 20k kwa mwezi ni matumizi mabaya? Yule mwenye bilioni akahonga Lexus zero kilomita, ni matumizi mabaya?

2. Ingawa sio sana ila akiba haiozi na hasa kwa hizi nchi zetu za kiafrika na masikini, kusoma ndio maisha...kwamba hata kuwe na ukame wa miaka 10, siku ikinyesha hata nchi jirani, ikabidi maji yatiririke kwenda baharini, basi yatafuata mkondo/njia yake tu. Kila mtu anaweza kusoma, ila kuna mambo sio kila mtu anaweza kufanya au kupata, kama una nafasi, usiache kusoma, wenyewe wanasema ni "an added advantage". Baada ya uhuru, hakuna aliyewahi kusaini mikataba mibovu kwa niaba ya nchi ambaye sio msomi, tena wengine ni wa vyuo vikubwa na heshima lukuki.

3. Hii ni tabia ya wasomi wa kikwetu, na ni wazuri sana kwenye kutengeneza mifumo ya uharibifu kuliko kujenga. Wanakata tamaa kama hakuna mianya ya ujanja ujanja.

4. Qnet, Deci, Forever n.k

5. Kwa lugha nyepesi, ni kutakatisha pesa. Huitaji utafiti kufanya biashara ya maandazi. Ila Afisa wa TRA anayechukua milioni 100 kwa kuchezesha mambo, hawezi iweka benki, akikaa nayo ndani inaweza kumuua, anaenda kufungua Bar classic, na kwakuwa zile mambo zinamtembelea bado, basi uhalali wa pesa zake unaonekana ukitokea hapo. Siku kazi imekufa, unagundua kumbe yeye ndo alikuwa akihudumia biashara.

6. Kwa ngazi za akina Mo na wenzie, hakuna shida. Kama ulianza maisha kwa kujinunulia godoro la kulalia, mshahara unakatwa 15% ya bodi na huna jinsi ya kugusa pesa za angani zipitazo ufanyiapo kazi, huwezi kufanya mengi kwa wakati mmoja na ukifanya tamaa sana, Qnet watakubeba pia.

7. Hili ni zito, ama uchague UPENDO wa kweli bila kujali chochote kingine ukiamini na kumtegemea Mungu, kwamba upendo utadumu na kunyoosha mengine AU uchague fahari upambane na hali yako.
 
Hapo kwenye mahusiano pagumu kiongozi wewe unaweza kumwona sahihi kumbe kwako kaja baada ya kutoswa na abdalah siku mktibuana kidogo tu anaondoka,
mahusiano Siku hizi yamefikia pabaya sana wengi tunaogopana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom