Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,038
“Si kila anayeitwa ndugu ni wa kweli , wengine ni jina tu kwenye ukoo, lakini moyoni hawapo.”
Undugu wa kweli haupimwi kwa damu, bali kwa moyo.
Wapo watu wanaweza kukusaidia wakati wa jua, lakini wakakusahau ukianza kunyeshewa na mvua.
Hii ni hali halisi ya maisha usikate tamaa, bali jifunze kutegemea MUNGU na wewe mwenyewe.
“Si kila anayekuambia yuko na wewe, yuko nawe kwa dhati.”
Dunia ni pana, lakini maisha ni mafupi sana.
Chagua kuishi kwa hekima na kuwa na woga kwa Muumba aliyeweka pumzi ndani yako.
Kumbuka, ardhi ni kama tumbo la mla rushwa ,halitosheki.
Daima huendelea kumeza hata waliotenda mema, sembuse waliokupuuza?.
“Maisha ni safari ya ndani , usiyapoteze ukijitahidi kupendeza machoni pa watu.”
“Usidanganyike na tabasamu, wengine wanatabasamu ili kuficha makucha.”
Kuna watu hawasemi mabaya yako kwa sauti, lakini mioyoni mwao wameshaandika hukumu yako. Wanasubiri tu uanguke, ili waseme, “Nilijua tu.”
Lakini usiogope. Hata Yesu alisalitiwa na mmoja wa wake. Uaminifu hauko kwa jina wala damu , uko kwa moyo uliojaa heshima, imani na upendo wa kweli.
“Kuna waliokuchekea kesho yao ikiwa nzuri, lakini wakakusahau ulipohitaji hata nusu ya tabasamu lao.”
Maisha haya ni shule na kila siku ni darasa jipya. Walio leo ni marafiki, kesho wanaweza kuwa mashahidi wa anguko lako.
Lakini usilolijua ni kuwa,Kila anguko linafundisha, na kila kidonda kina hadithi.
“Usiogope kutembea peke yako, wakati wote wa kweli hawapatikani kwa wingi.”
Walioko kwa ajili ya moyo wako watabaki hata mvua ikinyesha na paa zikivuja.
Nao ndio familia ya kweli , si kwa damu, bali kwa roho.
Mwisho wa siku, amani ya kweli haiji kwa kuzungukwa na wengi, bali kwa kujua kuwa unaishi kwa ukweli, kwa kusudi, na kwa Mungu.
~Chavalikungu