Usiipuzie Sauti ya Mungu

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
367
Reaction score
731
Hellow habari, samahani naomba tuonane pale pa siku zote nina ujumbe wako, nisimu ambayo niliwasiliana na binti ambaye kwa kipindi kile nilitamani kuanzisha maisha naye ya pamoja

Miakaa kadhaa nyuma wakati , nimemaliza shule na kufanikiwa kuingia katika soko la ajira, nilianza mchakato wa kupata mke.

Mchakato huo nilifanya nikiwa kanisani mahali ambapo tuna muabudu Mungu. Nikiwa kanisani kuna binti tulikuwa naye katika kwaya.

Yule binti alikuwa ni miongoni mwa wanakwaya ambao wamempa Yesu maisha yao kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yao.

Binafsi nilifanikiwa kumfahamu kwa kitabu kidogo tangu nimerudi nyumbani kwa jinsi ya nje alikuwa ni mrembo na anajipenda kwa kweli

Nikiwa kwenywe kwaya moyoni, nilifanikiwa kufatilia maisha ya yule binti ya kanisani mambo ya nje tu, marafiki zake, ndugu zake , anavyosomo nk

Biblia inasema Mungu aangalia nje, Mungu anaangalia ndani ila Wanadamu tunaangalia nje.

Moyoni mwangu nilikuwa nataka kujua maisha yake ya nje na ya ndani yako sawa.

Nikiwa na endelea na upelelezi wangu wa kimya kimya, kaka yangu wa kiroho akaniuliza umemona flani? Unaonaje akiwa mke wako?

Nilimjibu majibu ya kawaida sana kwamba ni mrembo na yuko vizuri kwa jinsi ya nje ila kwa ndani moyo wangu umegoma kuwa naye kama mama wa watoto wangu.

Kaka yangu kiroho alinicheka akasema labda hana elimu kubwq kama ya kwangu ndio maana umehamua hivyo, binafsi haikuwa swala la elimu maana maisha ni zaidi ya elimu ilikuwa moyoni mwake yuko nani ambaye anaweza kuwa msaada wa maisha yetu.

Biblia inasema apataye mke amepata kitu chema, kwa hiyo kitu chema sio sura na vitu vya nje tu ingawa muhimu pia kuwa mtu unayempenda ila zaidi ilikuwa moyoni mwake kuna nini?

Maneno yalikuwa mengi na ushauri ulikuwa mwingi mwisho nikakubali ushauri wao.

Uzuri yule binti tulikuwa tuna mahusiano naye mazuri tu kama watumishi wa Mungu, nikamwomba kuonana naye, mazungumzo yakawa mazuri.

Miezi ikasogea mahusiano yakawa yamenonga, siku moja nikawa nimepanga kutangaza ndoa na taratibu za kuanza

Jioni moja tulikutana katika eneo ambalo tulikuwa tunakutana mara kwa mara nilimwita yule binti na kumweleza yale ya moyoni, binafsi yule binti alifurahi sana na tukaendelea na maongenzi mengine na baadae tukaagana.

Nikiwa njiani narudi nyumbani moyoni mwangu nilikosa Amani kabsa, nikama nimepokea taarifa mbaya, nilijiskia huzuni, kadri nilivyokuwa nawazo mipango ya kufunga ndoa na yule binti moyo ulikiwa na uzuni.

Kipindi kile sikujua maana ya uzuni ya Mungu ndani yangu maana yake nini? Nikampigia simu kaka yangu wa kiroho nikamweleza nataka kumwoa yule binti lakini moyoni kuna goma naskia uzito, naomba unisaidie kufanya upelelezi juu ya yule binti maana ndani yangu hakuko sawa, nashukuru kaka yangu wa kiroho kwakuwa yule binti alikuwa anafahamia naye kwa ukaribu sana alifanya kazi hiyo kwa moyo mkuu

Mara baada ya upelelezi kukamilika kaka yangu alikuja na taarifa ambayo haikuwa nzuri, sasa changamoto ikawa juu ya kanisa na marafiki ambao walikuwa wanajua nini kinaendelea , tukaomba tufanye maombi ili Mungu atupe hekima ya kumaliza jambo ili kwa wema

Namshukuru Mungu, Mungu alitufanyia njia pasipo na njia na tukavuka salama, kila mmoja akaendelea na maisha yake

Siku zote usidharau sauti ya Mungu ndani yako, Mungu anasema na sisi kwa njia nyingi tu lakini kwa sababu hatujuia ansemaje tunaingia kwenye matatatizo.

Usidharau sauti ya Mungu ndugu yangu sio kila Mwanamke/ Mume anaweza kuwa Mume/mkeo yuko yule Mungu ambaye amemweka kwa ajili ya kutimiza kusudi lake, ndio maana ni muhimu sana kumsikiliza Mungu wakati unafanya maamuzi juu ya maisha yako.

Pauli anasema kuishi hapa duniani ni kwa ajiki ya Kristo hivyo usifanye maamuzi ya maisha yako kama ni ya kwako pekee yako, hapana maisha pia ni ya Mungu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…