Gospel Preacher
JF-Expert Member
- Jan 17, 2018
- 233
- 264
Habari zenu ndugu zangu na watu wa Mungu mliopo humu JF, Kwa uweza wa Roho Mtakatifu Leo ninevuviwa kuleta ONYO hili kwenu na kwa watu wanaosababisha watu kutokwa Roho, kwa kuwapiga risasi,kutoa mimba,kuwateka na kuwatesa mpaka kufa au namna yoyote ile.
Napenda kuanza na tafasiri halisi:
Mtu ni Roho yenye nafsi hai inyoishi ndani ya jumba lake na hilo jumba lake ndio tunaiitwa mwili. Hivyo mtu kama ilivyo kawaida mwananchi anae kaa ndani ya nyumba anaweza kutoka na kwenda sokoni na kurudi nyumbani mwake na hii ndio ilivyotafasiri ya mtu, yaani anaweza kutoka ndani ya jumba lake(mwili wake) na kuingia ndani kwa sababu za kiroho (isipokuwa mtu mwenyewe hawezi kujitoa ndani mpaka kuwe na external force-nguvu ya nje ya rohoni ndio itakayo mtoa)
2 WAKORINTHO 12:2-4
2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua);
4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.
Tumeona ushahidi hapo kuwa Mtu anaweza kuwa nje ya mwili au ndani ya mwili lakini sio kwa kutaka kwake isipokuwa ni nguvu ya nje yaani nguvu hii inaweza kuwa ya Mungu-Roho Mtakatifu au Shetani-pepo la mauti(kama mtu mwenyewe hana Mungu wala haamini ktk Mungu na mwanae Yesu Kristo).
Hivyo mtu unafanya kazi ya kupewa au kujiamulia kuua/kumteka/kumchinja /kutoka mimba/au kunwaga damu ya mtu, tambua kuwa unamsaidia shetani kufanya hivyo, na kila Damu ya mtu ulioimwaga ina sauti na inaweza kuzungumza( kwa asili uhai wa mtu upo ktk damu ,damu ni uhai na unaweza kuongea)
Mwanzo 9:4
Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.
Mwanzo 9:5
Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.
Mwanzo 9:6
Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.
Unaona ushahidi wa kibibilia kuwa damu inaongea na inasauti maana ni Uhai, Kaini alimuua mwenzake Habili katika Uwanda na Mungu akamwambia sauti ya Damu ya nduguyo inanililia, hivyo kama umeshiriki kumwaga damu ya mtu au kuua jua kwamba uhai wa mtu unakulilia Siku siku zote, na Mungu anakupa nafasi ya kutubu na kuacha Mara moja na ndio maana Leo umekutana na Thread hii.
Kumwaga damu ya mtu ni DHAMBI inayoongea mbele za Mungu, bila kujali aliyekutuma kufanya hivyo na kwa Mshahara gani unaopewa ni DHAMBI inayoongea muda wote.
Unapoa toa uhai wa mtu ambaye ni Roho ,kwa kawaida Roho huwa zinaishi mpaka mauti ya pili itakapofika (yaani siku ya kiama kwa maana Roho huwa hazifi, na hata maandiko yanaposema kuwa "Roho itendayo DHAMBI ndio itakayokufa" inamaana kwa habari ya mauti ya pili),isipokuwa inabaki ikirandaranda katika ulimwengu wa Roho ni kwasababu nyumba yake ambao ni mwili umeharibika hivyo hauwezi kukaaa, ndio hawa badae shetani anawatumia vibaya kuangamiza wanadamu wenzao na kuwageuza kwa namna ya Giza na wanakuwa jeshi la wafu.
LAKINI.......Mungu wetu aliyeziumba mbingu na nchi ni wa rehema sana ameufungua mlango wa toba kwako tena, kama umefanya hivyo hauna haja ya kutubu na kumwambia mtu yyte(kwa usalama wako) wewe omba msamaha kwa kumaanisha na Mungu aonae sirini atakusamehe na utafute kanisa lolote la wanao mwamini Yesu Kristo kama mwana wa Mungu na Roho Mtakatifu kama msaidizi wako na yeye atakusaidia saaaana na utaepukana na Mauti ya pili yaani hilo ziwa la moto.
NB: ACHA KUMWAGA DAMU ZA WATU NA KUTOA UHAI WA WATU.NI CHUKIZO MBELE ZA MUNGU.
Ukiwa mtu unatoa Roho za watu, unakuwa karibu sana na shetani maan a ndio kazi anayoipenda ,Bibilia inasema "mwizi haji ili aibe,kumchinja na kuua lakini Mimi ninekuja ili muwe na uzima kisha muwe nao tele". (Maneno ya Yesu Kristo )
FUATA SALA HII KWA UFUPI.
BABA MUNGU KATIKA JINA LA YESU, NAKUJA MBELE ZAKO MIMI..........(JINA LAKO) MWENYE DHAMBI, NILISHIRIKI KUMWAGA DAMU NA KUTOA UHAI WA WATU KWA NAMNA MBALIMBALI ,NAOMBA MSAMAHA LEO KWA JINA LA YESU. NAKUPOKEA YESU UWE BWANA NA MWOKOZI WANGU BINAFSI WA MAISHA NIPE ROHO WAKO MTAKATIFU ANISAIDIE. KUANZIA SASA NAKUPOKEA RASMI EE YESU KRISTO NA ASANTE KWA KUNIOKOA.
AMEN.
By
Gospel Preacher
The Gospel of Salvation (injili ya wokovu)