Usicheze na Vyombo vya Habari

muzi

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
1,039
1,453
Kimsingi vyombo vya habari vina nafasi kubwa sana kukupandisha na kukuangamizi. Ulimwenguni pote ni dhahiri kuwa MEDIA zina nafasi kubwa sana kukufanya kuwa MAARUFU kwa PROMOTION ya kazi na matendo yako.

Ukiwa karibu na media wayasemea POSITIVE achievements, plans, deliverable na yote ambayo yatakufanya kuwa ABOVE THE EDGE. Lakini pale unapokwenda negatively na media watayasemea mengi mabaya unayofanya na mwishowe kukuangamizi. Hata ukiwa na pesa nyingi lakini cheza vizuri na media.

Sasa hivi mtaani watu wanapiga mayowe na taarifa za MVAMIZI hazionekani tena, labda kwenye vile vyombo vya vinavyomilikiwa na wenye nchi. Lakini hata hivyo TV, magazeti yao watu wanaongalia/kununua ni wachache sana.
Hili ni somo zuri kwa wakuu wa nchi na wote wanopenda kujulikana na jamii
PLAY SAFELY WITH MEDIA
 
Unatafuta ngumi za usoni eeehhhh............
 
Mnatamani kumuandika ila mnaogopa kuonekana wasaliti. Kubalini ukweli mlimpa kiki akawapa mauzo makubwa ya magazeti yenu,mmempumzisha na mauzo yameshuka
 
Vyombo vya Habari=Vyombo vya Uongo/Hatari.

Vyombo vya hatari/Uongo ni chombo cha maangamizi chenye kuweza kuishambulia dunia kwa muda mfupi sana na kuleta matokeo mabovu/hasi.Vyombo vya hatari/uongo huishambulia akili ya mtu asiweze Kufikiri, Kuhoji, Kudadisi, Kusaili nk.

Kusaili ni kuuliza maswali ya msingi juu ya Kile unachokiona, Unachokisoma, Unachokishika nk.There after Mind yako inakuwa FREE.Hivyo ndivyo walivyofanya kina Copernicus,Pythagoras,Anaximander,Socrate,Plato nk.Hawakuwahi ku-STRUGGLE FOR LESS.

Kuna watu leo wanawachukia Waarabu,Wamarekani,Wasomali nk eti tu kwasababu hivi vyombo vya Uongo vimeandika, Vimesema nk.Ni hatari mno.Twende extra mile,tusaili kila jambo kwa mapana yake.

Leo hii kuna watu wanaishi maisha fulani,Wankula vyakula fulani,Wanavaa katika namna fulani nk eti tu kwa sababu vyombo vya uongo vimesema.Hii si sawa kabisa,We need to reason everything.

Hii ndiyo kazi ya ubongo wa Mwanadamu.Kazi ya ubongo wa Kondoo ni kuliwa.
 
Back
Top Bottom