^^Mlevi alipanda daladala.
Konda akamuambia, tabia yako ya ulevi huwezi kufika mbinguni.
Mlevi akajibu, "kumbe mnaenda mbinguni, nishusheni. Mimi naenda BUGURUNI.....!
^^Bibi alikuwa anafua nguo za mjukuu wake aliyekufa kwa Ukimwi.
Katika kufua akakutana na bikini.
Bibi akasema "Ugonjwa huu mbaya, unakondesha hadi chupi! Ewe Mungu Tunusuru".
^^Jamaa alikuwa ana tabia ya kukojoa kitandani baadhi ya siku.
Akafikia kuoa. Katika ya siku za mwanzo baada ya harusi, siku moja kama kawaida yake alijikojolea.
Akapiga kelele "Mungu wangu eee".
Mke wake akashtuka, akamuuliza: Vipi mume wangu?
Mume: Hivi mke wangu ungeota unataka kuliwa na mamba, chuwi na simba kwa wakati mmoja ungefanyaje?
Mke: Ningezimia kabisa. Mume: Basi mwenzio sijazimia nimejikojolea.
^^Waumini waliambiwa watoe michango ili wazungushie ukuta eneo la makaburi.
Mchungaji akauliza kuna mtu ana swali?
Mlevi akauliza "je kuna Marehemu yoyote aliyewahi kutoroka? Kama hakuna, ukuta wa nini sasa?
Au ndixn ufisadi hadi kwenye makaburi...?
Mchungaji kimyaaaaa!
^^Uswazi kuna Vituko.
Mtu mmoja alinyimwa chakula msibani, kwa hasira akaaga akisema
"HAMNA NOMA... NA MIE NITAFILIWA TU. Mungu yupo..!!