• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Usia muhimu wa wazazi!!!

Ngongoseke

Ngongoseke

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2012
Messages
3,209
Points
1,225
Ngongoseke

Ngongoseke

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2012
3,209 1,225
Hakika...maneno yanatoa machozi

"Mama anaongea na mwanawe na kumpa usia"

Mwanangu mpenzi:

Kuna siku utanikuta uzee,sitafanya mambo yangu kwa akili; yakitokea hayo nakuomba tafadhali nipe muda na subira ili unifahamu !!

Pale mikono yangu itakapotetemeka,na chakula changu kikaangukia kifuani pangu,na nisipoweza kuvaa nguo zangu; jifunge na kusubiria, na kumbuka miaka imepita nilikuwa nakufunza ambayo leo siwezi kuyafanya!!

Ikiwa leo si maridadi na sina harufu nzuri; usinilaumu..kumbuka udogoni kwako nikijitahidi sana nikufanye uwe maridadi mwenye harufu nzuri!!

Usinicheke utakapoona ujinga wangu na
kutofahamu mambo ya wakati wenu huu, lakini wewe kuwa jicho na akili yangu ili niyapate niliyoyakosa!!

Mimi ndiye niliyekufunza adabu na mimi ndiye niliyekufunza vipi ukabiliane na maisha; sasa inakuaje leo unanifundisha yaliyo wajibu na yasiyo wajibu?

Usinichoke kwa udhaifu wa kumbu kumbu yangu,na uchelewaji wa maneno yangu na fikra zangu wakati ninapozungumza nawe, kwani furaha yangu wakati huu ni kuwa pamoja nawe tu!!

Wewe nisaidie tu kupata ninachohitaji; kwani bado najua ninachotaka!!

Miguu yangu ikikataa kunipeleka sehemu ninayotaka kwenda; nihurumie na kumbuka kwamba mimi nilikushika sana mkono ili uweze kutembea!!

Usione haya abadan kunishika mkono wangu leo; kwani kesho utatafuta wa kukushika mkono wako!!

Katika umri wangu huu; elewa kuwa mimi siyaelekei maisha kama wewe; lakini kwa ufupi nangojea mauti; kwa hiyo kuwa pamoja nami wala usinitupe!!

Pale ukikumbuka makosa yangu; jua kuwa mimi nilikuwa sitaki ila maslahi yako!!

Na mimi napenda sana unayonifanyia hivi sasa kwa kunisamehe matelezo yangu na kusitiri aibu zangu..Nawe Mola akughufirie na akusitiri!!

Bado vicheko na tabasamu zako vinanipa furaha kama ulivyokua mdogo... kwa hiyo usininyime suhuba yako!!

Nilikuwa nawe wakati unazaliwa; kuwa nami pale nitakapofariki!!

🔺Maneno bora yaliyopitia katika maisha yangu,na hata nikiyarudia mara elfu moja sichoki kuyasoma..
"Mola wangu warehemu kama walivyonilea nilipokua mdogo"

🌰TUAMRISHANE🌰
🌰MEMA🌰
 

Forum statistics

Threads 1,404,414
Members 531,595
Posts 34,453,031
Top