Ushuru wa maegesho ni uonevu

Marumeso

JF-Expert Member
Oct 3, 2009
1,410
1,322
Sasa hivi miji na majiji mbalimbali zimebuni utaratibu wa kukusanya ushuru wa maegesho. Kila utakapopita utakuta vijana wamewekwa kwa shughuli ya kuchukua pesa kwa mtu anaepaki gari yake hapo. Tena bila kujali unapaki kwa muda gani watakudai chao. Ukipita kulia hawa hapa, kata kushoto hawa, ingia huku wapo kata hapa wapo!!

Haya...kinachosumbua zaidi mengi ya maeneo haya yaliyopewa jina la maegesho hayajaongezwa thamani kwa kufanyiwa uwekezaji wowote. Kwa lugha nyingine hakuna maeneo yaliyoandaliwa rasmi kama maegesho. Unakuta sehemu ya hovyohovyo tu haina lolote wala chochote ilimradi gari inasimama kuna mtoza ushuru kawekwa hapo akusanye ushuru, jamani.
Mwogopeni mungu!!

Na mara nyingi vijana wanaowekwa hapo ni kama wapo hapo kukusanya pesa tu wala hawana habari na uangalizi wa hayo magari yenyewe. Unakuta kijana akishachomeka risiti anatokomea anakokujua, atarudi mbio pindi ataposikia umewasha gari unataka kuondoka au hadi umwite.

Jamani pesa zinatafutwa kiugumu na tena kwa jasho. Msipende pesa za bure bure namna hii na kama ni lazima mchukue pesa zetu mtendee haki kwa kutengeneza hayo maegesho vinginevyo huu ni wizi tena wa mchana kweupe.
 
Back
Top Bottom