Ushuri wenu tafadhali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushuri wenu tafadhali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by binywa, Jun 28, 2012.

 1. binywa

  binywa Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Habari zenu ndugu zangu popote mlipo.
  Mimi ni mgeni ktk forum hii na nimekuwa nikivutiwa sana na hoja mbalimbali hapa jamvini.
  Kuna jambo nahitaji ushauri wenu. Mimi ni kijana (male)wa miaka 28 nina mchumba ambae ana miaka 22, na tumekubaliana kufunga ndoa kwani tayari nimekwisha jitambulisha kwao. Wiki iliyopita nimesikia kuwa mchumba wangu anasema (kwa watu wengine) kuwa alinikubali kwa sababu tu mimi ninafanya kazi na ninajimudu maisha yangu lakini kutoka moyoni hanipendi bali anampenda kijana mwingine ambae aliwahi kumchumbia ila binti alimkataa eti kwa sababu anafanya kazi ya ulinzi na hali yake ni duni kifedha, na ana wasiwasi na uaminifu wangu kwake kwa sababu anahisi bado nina mahusiano na girlfriend wangu wa zamani so haamini kama kweli yule nimemwacha yeye anaona bado tunaendelea na mahusiano. Anasema hivo kwa sababu kuna harusi fulani nilialikwa na nilitakiwa kwenda na mchumba wangu ila mchumba wangu alichelewa kufika na bila kupanga au kujua huyo girl friend wangu wa zamani nae alikuwa amealikwa kwenye harusi hiyo na alikuja na boyfriend wake mpya so tukakaa meza moja. Mchumba wangu alivyoingia ukumbini aliona nimekaa meza moja na huyo Ex girlfriend wangu na mimi sikujua kama mchumba wangu amefika kwani nilikua napiga simu na haikupokelewa kwa zaidi ya saa nzima na alivyokuja alikaa meza nyingine, so wakati wa chakula ulipofika tulinyanyuka mimi, my ex girlfriend, na boyfriend wa my ex girl friend. kumbe mchumba wangu alikuwa anatuona lakini ilipofika zamu ya mchumba wangu kuchukua chakula ndipo nikamwona na nikamfuata tukakaa meza moja. baada ya harusi mchumba wangu aliniuliza eti kwa nini nilimuumiza roho kwa kuingia na my ex girlfriend na alidai kuwa mimi ndiye nilimwambia huyo msichana aje baada ya kuona yeye amechelewa, nilimwelewesha na akaonekana kuelewa lakini cha ajabu mchumba wangu alienda kuongea habari kwa watu wengine kama watatu na kusema kua hajui afanye nini kwa kua mimi si mwaminifu kwake.
  Mimi kwa upande wangu sina mahusiano tena na huyo ex girl friend wangu japo mchumba wangu haamini ninapomwambia hivo.
  Naombeni mnipe ushauri nifanye nini kwani suala la mchumba wangu kuniuliza habari za ex girlfriend wangu huwa inajirudia mara kwa mara na anaonesha dalili zote kuwa yeye haniamini sana. Lakini pia ni jambo hili lililozuka kuhusu huyu kijana mwingine kua yeye anampenda japo sijasikia direct toka kwa mchumba wangu ila nimesikia toka kwa mtu mwingine ambae aliombwa ushauri na mchumba wangu. Nafikiria nimuulize mchumba wangu kuhusu jambo hili kwani naona ni jambo ambalo ni serious.
  Tafadhali nisaidieni nifanye nini na ni nifanyeje
  Nimefuatilia kwa muda nimepata yafuatayo....... Nisaidieni jamani
  Nimejaribu kufuatilia kwa muda mfupi huu ninahisi kuna kitu kinaendelea kati ya huyu mchumba wangu na huyo jamaa mlinzi kwani kuna siku moja (msichana) alikuja nyumbani kwangu tukiwa tunaongea simu ikaita kumbe ni ya yule jamaa mlinzi nilipomwambia apokee alisema kuwa haina haja kwani jamaa hana jipya nilimlazimisha sana lakini bado hakukubali, mimi nikaamua kuacha lakini huyu msichana alipoondoka wakati wa usiku nilimpigia simu msichana kanimtega tu kama jamaa alimpigia akakubali hapo pia wasiwasi ukaongezeka
  Na siku nyingine tukiwa tumetulia nilikuwa nachezea simu yangu kumbe msichana alikuwa ananiangalia kwa jicho la kuibia ktk inbox yangu kulikua n sms toka kwa huyo kijana mlinzi alipoona jina la yule jamaa aliongea kwa mshituko akitaka kusoma sms ya huyo kijana huku mapigo ya moyo wake yakienda kasi zaidi na aliposoma alikua km mtu aleetua mzigo mzito uliomlemea......
  Kwa taarifa nilizozipata toka kwa rafiki wa karibu wa mlinzi ni kuwa huyu binti ndo alionesha dalili za kumpenda huyu kijana lakini nilipomuuliza binti alisema kua yule kijana alitaka kumwoa ila yeye akakataa...... utata unaendelea kuongezeka
  Ndugu zangu kwa kweli kazi bado ni kubwa ila bado naendelea namini nitaupata ukweli ulipo ila naomba ndugu zangu msinichoke kwa kuwaomba ushauri katika hili naamini ushauri wenu ni wa muhimu katika jambo hili

  Asanteni
   
 2. K

  Kigali Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Pole sana kijana hizo ndo changamoto za kuchovya huku na kule........ kwanini sasa hukumwoa ex gf wako......
  ona sasa unapata kesi ambayo hata huijui km ya Lulu kumuua Kanumba....
   
 3. Root

  Root JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,189
  Likes Received: 12,906
  Trophy Points: 280
  Kaka hapo huna mtu ye anataka pesa tu siku ukiwa kwenye hali kama ya huyo mlinzi atakutema hivyo kuwa mjanja usije kujuta
   
 4. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inabidi ufueatilie kama kweli maneno ya kumpenda huyo mlini ni ya kweli kama kweli amesema hivo ni wazi kuwa lazima huyo mtu hakufai brother. Thanks
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,663
  Trophy Points: 280
  Sijasoma thread nzima lakini dogo nataka nikuambie jambo moja.Huyo g/friend wako lazima mtaachana tu.Unapoanza uhusiano na mwanamke mwenye umri chini ya miaka 25 lazima mtakuja kuachana tu!
   
 6. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Mdogo wangu pole sana kwa hali uliyo nayo. Itabidi tukuambie tu ukweli kutokana na uzoefu wetu, pia kwasababu wewe mwenyewe unahitaji ukweli kuliko unafiki. Lkn pia ni hali unayopitia. Awali ya yote napenda nikupongeze kwa tabia yako ya uwazi na unyenyekevu. Nimegundua hizo sifa kwako baada ya kusoma habari yako, kwani pamoja na kuwa ni post yako ya kwanza JF, lkn umetumia nidhamu katika kuwasilisha tatizo lako. Ni mara nyingi watu wanapotokea humu na post zao za kwanza, huwa hawana nidhamu na wanaandika kama vile yuko Facebook.

  Sasa nikirejea kwenye hoja yako, mchango wangu unaegemea kwenye halama nyekundu na hasa kwenye mstari. Kuhusu umri wa mchumba wako, ni kwamba kwenye huo umri yeye bado yuko kwenye hali fulani ya kutokuwa na uwezo wa kufanya maamuzi ya dhati katika kile anachoamini, hasa yanayohusu NDOA. Hivyo ni vigumu sana kufahamu kama ana nia thabiti ya kile anachokuambia.

  Jambo lingine, tena la hatari kwako ni hiyo kauli ya kwamba hana Upendo kwako bali kafuata mali, na bado anampenda jamaa mwingine. Huyo mchumba wako kama ametamka hayo, basi amekusaidia sana mdogo wangu. Huyo hata kama utaamua kujifariji kwamba atabadilika ukishamuoa, basi utakuwa unajidanganya kwasababu kama hatakusaliti kwa huyo jamaa basi atapata mtu mwingine anayempenda, na hizo pesa zako na usafiri wako ndizo zitatumika kulipia Guest ili wakafanye ufuska. Na itakapotokea ndipo utakapojua kwamba kumbe kusalitiwa ni kubaya na unaweza jikuta unatenda kesi ya mada kwake au kwa huyo ambaye atakuwa anacheat naye.

  Ni lazima tukubaliane kwamba wasichana wengi wa siku hizi wako motivated zaidi na mali bila kuzingatia upendo. Lkn mchumba wako asingepaswa kabisa kutamka maneno mazito kama hayo kwamba hana upendo kwako bali kafuata mali. Sasa jiulize hili swali, Je, siku mambo yakichacha kwako hali itakuwaje? Si unajua kwamba huna mkataba na Mungu kwamba wewe utakuwa na hali nzuri financially siku zote, je ikitokea hali imekuwa tofauti kiuchumi kwako na upendo hana kwako, je nini unategemea hapo?

  Kwasababu hana upendo kwako na maisha yamekuwamagumu, basi kuna hatari ya wewe kuwa depressed kabisa kutokana na maamuzi atakayochukua mkeo kwa kipindi hicho. Ndugu yangu, mimi sikuambii nini cha kufanya lkn ni wewe ndiyo unapaswa kupima hali ilivyo na kufanya maamuzi sahihi, kwani mwisho wa siku mzigo wote utakuwa juu yako. Hivyo jiulize maswali yafuatayo kabla hujafanya maamuzi;
  1. Je nini motive ya mchumba wako kukubali kuolewa na wewe?
  2. Je siku mali ikiyumba kwako hali itakuwaje?
  3. Kama hakupendi, je siku akikusaliti kwasababu hakupendi hali yako itakuwaje?
  4.n.k

  NB: Ndoa siyo majaribu na ndoa ni zaidi ya uijuavyo, hivyo ni bora uingie kwenye ndoa na mtu ambaye anakujali na anakupenda.
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  hebu mchunguze huyo mwanamke vizuri...
   
 8. ThePromise

  ThePromise JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usimbwage moja kwa moja bila uchunguzi,jaribu kumchunguza kwa kufuatilia kwa ukaribu nyendo zake,kuwa mdadisi katika mahojiano yenu,usichukulie kitu(dosari) kiurahisi hata kama ni kidogo kias gani,think out of the box:yaan jarib kutoruhusu mapenz yakufunge macho ktk kpnd hiki cha uchunguzi lazima utafanikiwa kugundua kitu mwisho wa siku ambacho kitakupaconfidence na reason ya kuchukua uamuz,either kumbwaga or kumlea ili aje awe mkeo kwan still ni mdogo huyo!all the best.
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Kaaa mbali na huyo x wako!
   
 10. binywa

  binywa Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Asante kwa ushauri huo ndugu yangu
   
 11. binywa

  binywa Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  thanks
   
 12. binywa

  binywa Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  najitahidi kufanya hivo lakini mwenzangu bado anaona anaibiwa....... hata hivo nakushukuru kwa ushauri huo ntaufanyia kazi
   
 13. binywa

  binywa Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Naamini hii yaweza kunisaidia....... jambo ambalo nimejifunza kwa mwenzangu huyu ni kuwa anapoona tatizo kwangu badala ya kuniambia utakuta anaenda kumwambia mtu mwingine. kuna maneno ambayo ninaongea nae tu lakini nashangaa nayakuta kwa watu wengine eti alienda kuomba ushauri. Nimejaribu kumwambia kua km anaona tatizo kwangu ni heri aniambie mimi kwanza kabla ya kwenda kumwambia mwingine so najikuta hata tukioana kuna mambo ya ndani yatakua yanatoka nje.

  Nilipomuuliza kuhusu huyo jamaa mlinzi mchumba wangu aliniambia kuwa ni kweli jamaa aliwahi kumtokea lakini yeye binti hakumkubalia ila kinachonichanganya ni kuwa jamaa mwenyewe nafahamiana nae vizuri na ktk hali ya kumdadisi jamaa amekataa kuwa hajawahi kumtokea huyo binti na hapa ndipo ninapopata wasiwasi na ninaona kuna kitu kimejificha ambacho sikijui....
  Nakushukuru kwa hizo hints
   
 14. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Hana lolote, sababu ni hiyo hapo red. Hakupendi ila anapenda unavyompeleka saluni na kumnunulia brekiberi.
  Kaka kimbia hapo, sio kwako shauri yako.
   
 15. kapistrano

  kapistrano JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,204
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kuwa makini ndugu yangu kisema kuwa fulani nimeachana naye uwe unamanisha kimaneno hadi vitendo hapo uhusiano wako utadumu kinyume na hapo utaomba sn ushauri humu jamvini na pia una sababu ya kumuuliza maana umesema umesikia kwa mtu na usipenda kusiliza maneno ya watu take care.
   
 16. c

  chwechinyong JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 224
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Napata alama ya taa nyekundu mbeleni juu ya huu uhusiano wako based on the following fact:
  1: kukushuku kwa mchumba wako kwamba bado unatoka na x wako...hii inanipa shaka kwamba huenda yeye ndo anafanya hilo na ndo maana anashindwa kujiamini
  2: kueleza mambo yeni kwa wengine bila ya kukuuliza wewe...hii utakuja kuiona athari yake baada ya kumuoa.kwani mambo mengi haya ya ndani huenda akategemea ushauri toka nje zaidi ya kukushirikisha wewe mme wake kwa wakati huo.kitu ambacho kitakusababishia depression kubwa
  3: inaelekea huyo mchumba wako anatabia ya kukuchunguza chunguza...kwa maana hana imani nawe na ndo maana mara kwa mara ameweza kukushutumu kutoka na x wako hata kama hufanyi hivyo
  4: kitendo cha mchumba wako kusema kwamba jamaa alishawahi kumtokea na jamaa kukataa kuna mambo mawili hapo; aidha jamaa kweli anayoka na mchumba wako ila hataki uhisi kitu ndo maana kakataa au kama si hivo basi huyo mchumbaako ana mapenzi na huyo jamaa na huenda ikawa yeye ndo anajolengesha kwa jamaa

  cha kufanya
  1: kaa chini na mwenza wako,mueleeze userious wako juu ya mahusiano yenu na nini unakitaka na nini hukitaki ikiwemo hilo la kuwashirikisha wengine katika mambo yeni bila ya wewe kujua au kukushauri
  2: mueleze ukweli kwamba umesikia maneno hayo ayasemayo kwa wengine na usikilize utetezi wake utakuwaje
  3: kuweza kweli kuthibitisha kwamba anakupenda au yupo kwa ajili ya ulichonacho...jaribu siku moja moja akikuomba kitu kumwambia kwamba kwa sasa hali yangu si nzuri..subiri baada ya siku mbili tatu..then.sikilizia atalipokea vipi hili

  baada ta hapo..wewe ni mtu mzima.siwezi kukutolea maamuzi kwani maamuzi kamili unayo wewe.
   
 17. c

  chwechinyong JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 224
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Napata alama ya taa nyekundu mbeleni juu ya huu uhusiano wako based on the following fact:
  1: kukushuku kwa mchumba wako kwamba bado unatoka na x wako...hii inanipa shaka kwamba huenda yeye ndo anafanya hilo na ndo maana anashindwa kujiamini
  2: kueleza mambo yeni kwa wengine bila ya kukuuliza wewe...hii utakuja kuiona athari yake baada ya kumuoa.kwani mambo mengi haya ya ndani huenda akategemea ushauri toka nje zaidi ya kukushirikisha wewe mme wake kwa wakati huo.kitu ambacho kitakusababishia depression kubwa
  3: inaelekea huyo mchumba wako anatabia ya kukuchunguza chunguza...kwa maana hana imani nawe na ndo maana mara kwa mara ameweza kukushutumu kutoka na x wako hata kama hufanyi hivyo
  4: kitendo cha mchumba wako kusema kwamba jamaa alishawahi kumtokea na jamaa kukataa kuna mambo mawili hapo; aidha jamaa kweli anayoka na mchumba wako ila hataki uhisi kitu ndo maana kakataa au kama si hivo basi huyo mchumbaako ana mapenzi na huyo jamaa na huenda ikawa yeye ndo anajolengesha kwa jamaa

  cha kufanya
  1: kaa chini na mwenza wako,mueleeze userious wako juu ya mahusiano yenu na nini unakitaka na nini hukitaki ikiwemo hilo la kuwashirikisha wengine katika mambo yeni bila ya wewe kujua au kukushauri
  2: mueleze ukweli kwamba umesikia maneno hayo ayasemayo kwa wengine na usikilize utetezi wake utakuwaje
  3: kuweza kweli kuthibitisha kwamba anakupenda au yupo kwa ajili ya ulichonacho...jaribu siku moja moja akikuomba kitu kumwambia kwamba kwa sasa hali yangu si nzuri..subiri baada ya siku mbili tatu..then.sikilizia atalipokea vipi hili

  baada ta hapo..wewe ni mtu mzima.siwezi kukutolea maamuzi kwani maamuzi kamili unayo wewe.
   
 18. binywa

  binywa Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Asante ndugu yangu kwa ushauri wako nitafuatilia. Kuhusu kuongea nae nitafanya hivo kwa mara nyingine coz nimeshaongea nae kwa zaidi ya mara mbili lakini kwa kuwa wajibu wangu ni kumkumbusha nitafanya hivo tena kwa msisitizo mkubwa
   
 19. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kweli kazi si kupenda bali kazi ni kumpenda akupendaye....... kaza msuli kijana labda utafanikiwa cha muhimu uupate ukweli ili hata unapoamua kumwacha uwe na sababu ambazo zinaeleweka vinginevyo utaonekana haukua serious.
  Kila la kheri
   
 20. K

  Kigali Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa hali hii kaka huyo mwanamke atakusumbua, kama hutajali achana nae anza process upya
   
Loading...