Ushuhuda: Jinsi nilivyonusurika kifo

Ganda Mweri

JF-Expert Member
Mar 8, 2018
293
855
Wasalaam ndugu zangu, nikikumbuka hiki kitu huwa ninajisemea kwamba, Acheni Mungu aitwe Mungu.

Nikiwa kijana mdogo miaka kadhaa iliyopita , Nyumbani kwetu kulikua na kisima ambacho wakazi wengi wa kijijini kwetu, walikua wakija kuchota maji kwa bei ya sh 100 kwa ndoo kubwa na 50 kwa ndoo ndogo.

Siku moja nikiwa hapo kisimani alitokea Dada mmoja aliyekuwa amekuja kuchota maji, lakini hakuwa na hela. Sasa Mimi nikawa ninamzuia kuchota maji huku nimekizingira kisima.

Sasa yule Dada kiutani utani akasema tena nitakusukuma humo, kipindi anasema hivyo akawa amenisukuma moja kwa moja ndani ya kisima. Hapo hapo yule Dada akaanza kupiga yowe.

Ninachokumbuka kipindi natua mle kwenye kisima nilitua kwenye tope moja kwa moja, na nikawa najaribu kutoka, maji yakanileta mpaka juu kisha nikazama tena, Ila kipindi narudi juu kwa Mara ya 3 nakumbuka kuna kitu kilinishika baada ya hapo nikajikuta hospital.

Kumbe yule Dada kipindi anapiga yowe , Kuna mwananchi alikuja akaingia ndani ya kisima na kunitoa huku nimeshapoteza fahamu na kunipeleka hospital ilikua ipo jirani tu na nyumbani kwetu.

Sasa kipindi nimetoka hospital, Mama akaniambia, sasa mwanangu ulikua unataka kujiua kwa sababu ya Grace?? Kumbe yule Dada aliwaambia, kwamba Mimi nimejirusha kisimani kwa sababu nimemtongoza akanikataa.

Mimi nikamwambia mama ukweli, kwamba yule binti ndiye aliyenisukuma , baada ya kumdai hela ya maji.

Wazazi wakataka kwenda kumshtaki, lakini majirani wakashauri tuyaache , kwa sababu wote tulikua vijana wadogo.

Mungu ni mkubwa hicho kitu ndio huwa nasema kila siku, Kama kuna MTU aliyewahi kuponea tundu la sindano kama Mimi naomba atushirikishe .
 
Duuh pole sana mkuu....
Binafsi nishawahi pata ajali ya kupinduka na gari mara tatu tofauti namshukuru Mungu sikuwahi pata hata jeraha... Ajali moja gari ilikua nyang'anyang'a ila sikuumia hata tone.... mara zote nilikua naendesha mwenyewe....
Mpaka sasa nikiwa kwenye gari speed ikifika 120 mwili unasisimuka...
 
Mimi nakumbuka Tundu lissu alipopigwa lisasi 38 lakini amepona
Duh nilianguka na pikipiki Helmet ikapasuka vipandevipande, nikaja tena kupinduka na gari, iliviringika mara tatu nikapone.
hii ya mwisho ndo Kali, niligonga demu mwenye moto bila condom nikapona tena,
Aisee acheni Mungu aitwe Mungu, hakika Mungu siyo Kama Mr Alcohol.
 
kama yangu tumebana hatukwenda shule tumeenda kuogelea bwawani siku Huyo mvua imenyesha bwawa limejaa mwenyeji nika tangulia sasa kiangazi bwawa likikauka wanakijiji wanachimba Visima vidogo ndani ya bwawa nika kwama ndani ya moja ya kisima mguu ulinasa. nilipigana kama dk 6 nikaanza kunywa Maji nikafanikiwa kutoka sikuongea Na MTU nikubeba nguo hadi home baadae kama wiki moja akavuta MTU Na bwawa likafungwa
 
Duh nilianguka na pikipiki Helmet ikapasuka vipandevipande, nikaja tena kupinduka na gari, iliviringika mara tatu nikapone.
hii ya mwisho ndo Kali, niligonga demu mwenye moto bila condom nikapona tena,
Aisee acheni Mungu aitwe Mungu, hakika Mungu siyo Kama Mr Alcohol.
Duuh!! Huyo demu mwenye moto bado yupo??
 
maji ni hatari nakumbuka mwaka 2014 nikwenda msasani beach kupunga upepo,mara nikapata na mawazo ya kuogelea.
mtu mzima nikaingia majini kuanza kuogelea huku nikiwa najifundisha mwenyewe maana nilikuwa sijui vizuri,kumbe maji huwa yana rudi dah- ilikuwa hatari kila mtu niliyekuwa nae karibu alikuwa anajiokoa nilijaribu kupiga kelele hakuna anaye niskia.
kwa kweli nilikiona kifo changu! nilikuwa nimevaa boxer na vest tu lakini niliiona vest nzito kama kilo 100 za mawe sikumbuki niliivua vipi ile ves, badaye nikaanza kupiga piga miguu huku nikinywa maji naibuka juu na kurudi chini.
badaye msuli ulinibana hapo ndipo niliona kifo nilipambana sana badye nikashindwa nikajiachia kurudi chini vile narudi chini nikawa nimekanyaga chini ya maji-huku kwa juu maji yakiwa yamenivuka pua nilitoka mbio.

maishani mwangu nimenusurika ajali nyingi ila hii ya maji baharini sito isahau hata siku moja na hadi leo sijawahi kanyaga baharini wala ziwani-nimeyaogopa maji kama ukoma
 
Duh nilianguka na pikipiki Helmet ikapasuka vipandevipande, nikaja tena kupinduka na gari, iliviringika mara tatu nikapone.
hii ya mwisho ndo Kali, niligonga demu mwenye moto bila condom nikapona tena,
Aisee acheni Mungu aitwe Mungu, hakika Mungu siyo Kama Mr Alcohol.
ahahaaa eti umetoka kugonga demu Mwenye nn !!?
 
Dah.. kuna siku nakumbuka kwenye mwaka 2003 au 2004 hiv pale kimara bucha nusu nipige bonge ya mzinga na gari.
Tumetoka maeneo ya kibamba mida ya mchana tunaenda ubungo. Niko na pick up hilux 2.8 manual. Tumefika kimara ndo tunaingia double road ikaja landcruiser imechoka choka ikanichomekea. Dogo mmoja akasema bro huyo jamaa anakuchezea na gar yake imechoka choka unakubali. Kweli bhana ujana maji ya moto. Nilikua namba tatu nikavuta mbili... Jamaa akashtuka namtafuta tukaanza kucheza draft balaa... Mpaka nafika kimara korogwe niko speed 120 na hiv mchana enz hizo barabara nyeupeee. Nakamata slope ya kimara butcher nenda speed 130 km/h. Niko upende wa kulia wa double road... Jamaa wa mbele mara akamate breki za gafla... Wee... Kuweka mguu kati hola... Ikabid nitoke niende barabara ya kushoto kwangu...
Kutokana na speed kubwa ya gar na kukata kona kwa gafla tair za upande mmoja zikanyanyuka nikawa natembelea tair mbiz za kushoto. Nikakata kulia kuweka gar sawa... Tair za kushoto zikanyanyuka gar inatembelea tair za kulia. Hata sijui nilipata wap control gar ikayumba sana halafu ikatulia.
Hakuna mtu aliyemsemesha mwenzake tena kwenye gari mpaka tunafika ubungo. Na nilitembea na speed ya 40km/hr mpaka nafika.
Mungu alikua upande wetu siku hiyo.. la sivyo ningeshasahaulika
 
Nimecheka utafikiri mazuri eti hamna aliyemsemesha mwenzake pole lakini
 
Kutokana na speed kubwa ya gar na kukata kona kwa gafla tair za upande mmoja zikanyanyuka nikawa natembelea tair hahahahaha nimecheka kama mazuri vile
 
Nakumbuka nipo mdogo wakati asubuhi huamuka kuelekea sokon kutafuta vyuma/vibomba vya baiskel kutengeneza magari. Mti ulikuwa umeanguka ukaziinamisha nguzo za umeme na nyaya ambazo hazina magamba nilikuwa ninajiuliza nikienda kugusa kitatokea nini dah niliziendea wakati umeme upo mwili nzima ulisisimuka ghafla nikakuta nimeacha. Hakika nilipona ile siku.
 
Mimi nasikitika ile Helicopter iliyoanguka kipindi kile cha kampeni pale Airport haikuondoka na mtu mmoja fulani....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom