kyanaKyoMuhaya
JF-Expert Member
- Jul 8, 2012
- 1,952
- 939
Aiseeh! Wanaume nimechoka!
John na Jeff walikuwa majirani na marafiki mpaka wake zao wakawa mtu na dada yake. John akaharibu akawa mpenzi wa mke wa Jeff jina lake ni Jessica. Mapenzi kikohozi Jeff akashtukia deal lakini akawa mtulivu na urafiki ukaendelea watu wakawa wanashangaa. Leo kulikuwa na ugomvi wa wanawake makelele hadi.
Kisa, kumbe Jeff alikopa kwa John milioni 5 akaongezea milioni 5 akanunua gari akaandikisha jina la mke wake. lakini gari anaendesha mwenyewe mke wake hajawahi kulipanda kwani wana gari jingine lenye jina lake ndio anaendesha mke wake.
sasa kivumbi kilianzia kwa John kudai hela yake maana aliona halipwi wala jamaa hajali. John amedai wee mwishowe akajibiwa nenda kamdai Jessica atakulipa nimeshamwambia. John akashtuka, akagwaya akarudi nyumbani dissappointed, akamsimulia mkewe alivyomkopesha Jeff na hataki kulipa na kuwa amesamehe deni. Siku akitaka kulipa alipe au aache. mke wa John kaona hasara kwa familia, kamfuata shosti dada mara nyingi amkumbushe shemeji alipe deni, Jessica hakuthubutu. Sasa leo mke wa John kamfuata Jeff ofisini na kumkumbusha ujumbe aliompa Jessica. Jeff akashtuka hajawahi pewa ujumbe wowote na Jessica. mke wa John hakuamini, ndio amerudi anampasha Jessica na umekuwa Ugomvi mkubwa. John Yuko kwake katulia na Jeff yuko sebuleni hana habari, wanawake wanatoana macho. Hivi wanaume wakoje. karibu kila mtu anajua picha isipokuwa mke wa John, Jeff keshachukua fidia yake ya ugoni. yaani usipime .