Ushirikishwaji wa wanaume katika huduma za Mama na Mtoto

nation

Member
Jan 11, 2017
54
40
Ndugu wana JF,

Jamii zetu za kitanzania hawafahamu umuhimu wa wanaume kushiriki katika huduma zote anazopewa mama na mtoto wakati wanapokwenda hospitalini na hata pale nyumbani. Tumezoea kuwa mama akiwa mjamzito huenda mwenyewe hospitalini kwenye Clinik ya ujauzito.

Atapewa huduma yeye kama mama kwa mda huo kumbe basi wanapoenda Clinik pamoja na waume zao kwanza watapewa kipaumbele ya huduma watapewa ushauri na elimu mbalimbali kuhusu ujauzito wa huyo mama kwani jamani ujauzito ni kama ugonjwa kwa hawa mama zetu, utaelimishwa vitu vingi, alafu watapimwa virusi vya UKIMWI na Kaswende ili kujua afya zao na pale watakapogundulika wataanza matibabu mapema.

Pia ukiwa nyumbani utakuwa karibu naye kumsaidia kupika na kufua nguo za familia nzima kwani wakati wa ujauzito kuinama kwa huyu mama ni shida. Pia eleweni kuwa watoto chini ya miaka mitano wanatakiwa wahudhurie Clinik bila kukosa.

Hii inasaidia kujua afya na maendeleo ya mtoto wako wake zetu wanapokuwa wajawazito au wamejifungua kazi ya kumpeleka mtoto klinik ndo inaishiaga hapo. Kumbe basi wewe kama baba lazima ushiriki kumpeleka mtoto wako Clinik pale mwenza wako anapozidiwa na majukumu.

Nje na hiyo pia inaleta hamasa na upendo ndani ya familia pale baba anaposhiriki shughuli mbalimbali za nyumbani. Tuacheni mila zetu mbaya ya kumwachia kila kitu mama.

Nimeipenda sana hii ndo maana nimewashirikisha.
 
ndugu wana jf jamii zetu za kitanzania hawafahamu umuhimu wa wanaume kushiriki katika huduma zote anazopewa mama na mtoto wakati wanapokwenda hospitalini na hata pale nyumbani. tumezoea kuwa mama akiwa mjamzito huenda mwenyewe hospitalini kwenye klinik ya ujauzito. atapewa huduma yeye kama mama kwa mda huo.kumbe basi wanapoenda klinik pamoja na waume zao kwanza watapewa kipaumbele ya huduma watapewa ushauri na elimu mbalimbali kuhusu ujauzito wa huyo mama.kwani jamani ujauzito ni kama ugonjwa kwa hawa mama zetu.utaelimishwa vitu vingi. afu watapimwa virusi vya ukimwa na kaswende ili kujua afya zao na pale watakapogundulika wataanza matibabu mapema . pia ukiwa nyumbani utakuwa karibu naye kumsaidia kupika na kufua nguo za familia nzima kwani wakati wa ujauzito kuinama kwa huyu mama ni shida.
pia eleweni kuwa watoto chini ya miaka mitano wanatakiwa wahudhurie klinik bila kukosa.hii inasaidia kujua afya na maendeleo ya mtoto wako..wake zetu wanapokuwa wajawazito au wamejifungua kazi ya kumpeleka mtoto klinik ndo inaishiaga hapo. kumbe basi wewe kama baba lazima ushiriki kumpeleka mtoto wako klinik pale mwenza wako anapozidiwa na majukumu.
nje na hiyo pia inaleta hamasa na upendo ndani ya familia pale baba anaposhiriki shughuli mbalimbali za nyumbani. tuacheni mila zetu mbaya ya kumwachia kila kitu mama. nimeipenda sana hii ndo maana nimewashirikisha
tatizo ni mila zetu kuwa kama unafanya kazi za mwanamke ujue tayari kashakukamata. hii nimeipenda sana
 
Back
Top Bottom