Ushirikina wamtisha katibu ccm

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
37,289
Likes
6,730
Points
280

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
37,289 6,730 280
Ushirikina wamtisha katibu CCM


na Stella Ibengwe, ShinyangaKATIBU Msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Kishapu mkoani hapa, Alli Makoa nusura aachie wadhifa huo kutokana na kuhofia kuuawa baada ya kutishwa na baadhi ya makada wa chama hicho.
Hatua ya katibu huyo inafuatia tetesi zilizozagaa kuwa katika wilaya hiyo viongozi wa CCM, hasa makatibu wanakufa kutokana na sababu ambazo hazieleweki jambo ambalo alielezwa kuwa na yeye ajiandae kufa.
Katibu huyo alitoa kauli hiyo kwenye sherehe za kuaga mwaka 2009 na kuukaribisha mwaka mpya 2010 wilayani humo, ambapo alisema baada ya kukaa kwa muda mrefu alibaini kuwa mambo hayo ni uzushi tu unaofanywa na watu waliokuwa na lengo la kumtisha ili aache kufanya kazi aliyotumwa. “Niliogopa sana, nilijua hata mwezi sitamaliza kutokana na maneno hayo niliyopewa kuwa viongozi wa CCM hapa wanakufa, tena ghafla tu, kwa kweli nilifikiria sana,” alisema Makoa. CCM wilayani Kishapu ilimpoteza katibu wake wa wilaya, John Pissa (65) aaliyefariki dunia mwaka jana baada ya kugongwa na trekta ambapo kifo chake kilizua mambo mengi zikiwemo imani za kishirikina.


h.sep3.gif


 

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
37,289
Likes
6,730
Points
280

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
37,289 6,730 280
Alifikiri uongozi ccm maisha plus
akipenda masoud umeupata loh
pole mkuu gangamala angalia tu wasikutoe kafaara ya chama
 

Forum statistics

Threads 1,191,688
Members 451,730
Posts 27,717,611