Ushirikiano chini ya utaratibu wa pande nyingi waisaidia Afrika kutimiza ufufukaji wa uchumi na maendeleo ya Afrika

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
72
111
Ushirikiano chini ya utaratibu wa pande nyingi waisaidia Afrika kutimiza ufufukaji wa uchumi na maendeleo ya Afrika

Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wametoa tena mwito wa "Kuhamisisha na kuiunga mkono Afrika" ili kulisaidia bara la Afrika kukabiliana na changamoto kubwa zilizoletwa na janga la COVID-19, ikiwa ni miezi sita baada ya janga hilo kuenea barani Afrika. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, kuunga mkono ufufukaji wa uchumi barani Afrika bado kunahitaji raslimali nyingi, na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Bw. David Malpass, amesema katika miaka mitatu ijayo Benki hiyo itatoa mkopo nafuu wa dola za kimarekani bilioni 50 kwa nchi za Afrika, na kuunga mkono ufufukaji wa uchumi wa Afrika na kuhimiza maendeleo ya muda mrefu barani humo.

Ingawa nchi za Afrika hazijaathiriwa sana na maambukizi ya virusi vya Corona kama iliyo katika mabara mengine, na hata baadhi ya nchi kama Senegal na Mauritius zimefanya kazi haraka na yenye mafanikio makubwa katika kupunguza kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona, madhara yake kiuchumi ya maambukizi hayo yameziacha nchi hizo katika wakati mgumu, na kuhitaji uingiliaji wa kifedha. Eneo la Afrika kusini mwa Sahara kwa mfani, linakabiliwa na upunguaji wa mara ya kwanza wa uchumi katika miaka 25 iliyopita, na mwaka huu uchumi wa eneo hilo utapungua kwa asilimia 2.1 hadi 5.1, huku kiwango cha uzalishaji wa mazao ya kilimo kikipungua kwa asilimia 2.6 hadi 7. Nchini Kenya takwimu zimeonesha kuwa kati ya mwezi Aprili na Juni mwaka huu, watu zaidi ya milioni 1.7 nchini Kenya walipoteza ajira kutokana na madhara ya virusi vya Corona.

Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limesema athari zinazoletwa na maambukizi ya COVID-19, sio kama tu zimebadilisha mwelekeo imara wa ongezeko la uchumi, lakini pia zimesabisha mapato ya familia kupungua kwa asilimia 12, na kama hatua hazitachukuliwa hali hiyo inaweza kuendelea zaidi. Serikali za nchi nyingi za Afrika zimetoa hatua za mfululizo za kuchochea uchumi, ambazo zimetumia asilimia 2.5 ya pato la taifa kukabiliana na athari hizo. Mchumi mwandamizi wa benki ya dunia barani Afrika Bw. Albert Zeufack amesema njia ya kufufua uchumi wa nchi za Afrika itakuwa ndefu na ngumu, lakini kuweka kipaumbele katika hatua za sera na uwekezaji ambao unashughulikia changamoto ya kutengeneza nafasi za ajira zilizo bora na jumuishi, kutaweka mazingira ya uchumi kufufuka kwa haraka zaidi na kwa nguvu zaidi barani Afrika.

Lakini wakati jumuiya za kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF wana sauti moja kuhusu mpango wa kusaidia kuchochea uchumi wa nchi za Afrika, nchi kubwa duniani zimekuwa na maoni tofauti. Kwa sasa baadhi ya nchi kubwa za magharibi ambazo ni washirika wa jadi wa nchi za Afrika zimekuwa zikitekeleza sera za kujilinda na hata uwekezaji wao katika nchi za Afrika umepungua. Mkurugenzi Mtendaji wa Peter Kagwanja, Taasisi ya Sera ya Afrika, ambayo ni taasisi ya ushauri bingwa ya eneo la Afrika Mashariki anaona tofauti na nchi za magharibi, ushirikiano na China unatoa mkakati wa kukabiliana na changamoto za kupambana na virusi vya Corona na hata kufufuka kwa uchumi wa nchi za Afrika, ikihimiza kuimarisha uzalishaji viwandani kupunguza umaskini, kutoa nafasi za ajira na kuboresha maisha ya watu. China imetoa mfano wa kuigwa kwa jumuiya ya kimataifa katika ushirikiano na Afrika.Miaka ya hivi karibuni, China imeunga mkono kithabiti Afrika kuchukua njia ya kujiendeleza, huku ikishirikiana na baadhi ya mashirika ya pande nyingi kutumia nguvu zao bora kuanzisha ushirikiano na Afrika katika sekta za kilimo, hifadhi ya mazingira na mafunzo, ili kuzisaidia nchi za Afrika kupunguza umaskini, kustawisha uchumi na kuhimiza maendeleo ya kijamii.
 
Back
Top Bottom