Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
• Wataalamu wa Ulaya nao wafichua mianya ya wizi wa kura
• Wakiri Chadema iliungwa mkono, Dk Slaa aliepusha vurugu
Uhalali wa Rais Jakaya Kikwete kuwa madarakani unazidi kutia shaka baada ya ripoti ya mwisho ya waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU) kutoa maelezo yanayothibitisha kuwapo kwa mwanya mkubwa wa kura kuibiwa na matokeo kubadilishwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.
Wakati rais Jakaya Kikwete na chama chake walidai kura zisingeibiwa kwa sababu kila chama huruhusiwa kuweka wakala wake, ripoti hiyo ya ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Jumuiya ya Ulaya (EU) inawaumbua, baada ya kueleza waziwazi bila kumung'unya maneno kwamba mawakala wa vyama vya siasa na waangalizi wa uchaguzi hawakuruhusiwa kushuhudia ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa ukifanywa na Tume ya Uchaguzi (NEC).
Ujumbe wa waangalizi hao wa EU ukiongozwa na Mbunge wa Bunge la Ulaya, Daid Martin, ulikuwepo nchini tangu September 29 hadi Novemba 28 mwaka jana na ulisambaza waangalizi wake 103 katika mikoa yote 26 ya Bara na Visiwani.
Katika ripoti hiyo ambayo Tanzania Daima Jumapili inayo nakala yake, wataalamu hao wameeleza kuwa matokeo ya kura za urais mwishowe yalijumlishwa na viongozi wa Tume ya Uchaguzi, NEC wakiwa peke yao bila ya kushuhudiwa na mawakala wa vyama vya siasa, utaratibu ambao kwa mtazamo wa kawaida, ulitoa mwanya mkubwa kwa kura kuibiwa au matokeo halali kubadilishwa, huku ukiwepo uwezekano wa Kikwete kupendelewa kwa sababu ya kile kinachoifajhamika kuwa ndiye aliyewateua kuiongoza Tume hiyo kutokana na mamlaka yake ya uteuzi akiwa kama rais………………..
Habari zaidi katika Tanzania Daima Jumapili
My take:
Hili ni kosa kubwa walilofanya wapinzani kutosisitiza kuwepo kwa mawakala wao kushuhudia majumuisho hayo ya kura uliofanywa na NEC ingawa huenda sheria/kanuni hairuhusu kuwepo kwa mawakala wa vyama.
Lakini kubwa zaidi kwa nini EU katika taarifa yao wasiseme tu kwamba "ingawa uchaguzi ulikuwa huru, lakini matokeo hayakuwa ya haki?"