USHINDI MKUBWA WA LOWASSA na MRAMBA unatuambia nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

USHINDI MKUBWA WA LOWASSA na MRAMBA unatuambia nini?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bongolander, Aug 7, 2010.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wakuu, matokeo ya kura za maoni yanaonesha kuwa Mh Edward Lowassa has won big, na Mh Basil Mramba has won big. Swali linakuja, ni kwanini haa jamaa wamepata ushindi mkubwa? NI kwamba wanafaa zaidi kuliko wagombea walioshindana nao? NI kwamba constituents hawajaui wagombea hao wamelifanyia nini taifa au wanasemwa vipi? Constituents huwa wananchagua mgombea kwa kigezo gani? au anayechaguliwa ni yule anayepenyeza Rupia zaidi?

  Kuna uwezekano kuwa shutuma wanazopewa si kweli ndio maana wananchi wao wanawaunga mkono sana? Kushindwa kwa Seleli kuna connection yoyote na hili?

  Tukiweka kwenye picha kubwa ya 31 Oct 2010, what conclusion can we draw from this?
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,723
  Trophy Points: 280
  Watanzania wanadanganyika
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 3,997
  Trophy Points: 280
  Watanzania wanaanza kukumbatia siasa za Kenya (i.e. Ubinafsi; as long as mwizi anafanya mazuri jimboni kwake then makosa ya wagombea kwa taifa hayawahusi Wanajimbo!) too bad on our cohesion as a nation! Naomba NEC iangalie hilo kwa umakini!
   
 4. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mmmh maskini sijui kama watanzania hawa wanajua nini kinaendelea anyway....its very sad...that they might not be able to know what is happening and what is NOT happening in the country
  mix with yours
   
 5. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mchango hapo juu umetoa jibu sahihi. EL, MRAMBA, CHENGE, wanajua muajiri wao ni wananchi wa jimbo na co mchango kwa taifa. Komba aliwahi kuwaambia NEC tutakaporudi majimboni wananchi hawatahoji EPA au Richmond bali watauliza zahanati, barabara, maji, umeme..... Karamagi hakulijua hilo akabaki na imani kama ya Kagasheki; Pesa ndo kila kitu! Kabwagwa vibaya sana.
   
 6. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  hapo iko namna.
  ni kweli wanajimbo kwa asilimia kuuubwaaaaaa hawana access ya kupata taarifa ya nini kinatokea katika dunia hii hususani nchini mwao.ukijiuliza ni wangapi walipata fursa ya kusoma habari za EPA nk.ni asilimia chache sana waliweza kuzipata habari hizo.
  La msingi wanaloliangalia ni je,wamepata maji,bara bara japo ya vumbi lakini inapitika,kiji zahanati ,....
  hapoinakuwa ndo mwiho wa mbwembwe zote.
   
 7. bona

  bona JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  majimbo yao wamenufaika na hawa wabunge, kwa mfano kama umechoka kuishi nenda monduli kamtukane lowasa mitaani uone raia wasio na hatia watavyokushuhulikia! wanasaidia sana wananchi majimboni mwao, sidhan kama kuna mwananchi anajali pesa anayopewa ni ya kifisadi au, hakuna pesa haramu!
   
 8. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  na maybe hata hawakuelewa ni nini kilichokuwa kinaongelewa kuhusu EPA.
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu the question is, Je watu wa Monduli have seen the improvement of their lives under leadership of EL, je watu wa Monduli hawajaeleimika kabisa na hawajui nini EL anafanya, au hawajui kuwa EL ni polarising figure kwenye siasa za Tanzania, au amewadanganya nini mpaka wao tu ndio wamuone wa maana sana kuliko sehemu nyingine za TAnzania. Au ni sisi hatujui kuwa EL is so good that anaweza kumpita mpinzania wake kwa kura zaidi ya 40,000?
   
 10. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hao jamaa wote wanaoonekena kushinda...sababu ni moja tu!!!!!!!!

  Taifa limepoteza mwelekeo halina mwenyewe...halina uelekeo wowote... Ni uozo wa jamiii umefikia kiwango cha juu!!

  Hakuna kiongozi mweneye mapenzi ya kweli na nchi...

  In that case kipofu yeyote anaweza kuitwaa jamii yeyote na kuchukua uongozi na kila kitu kikonekana its ok
   
 11. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #11
  Aug 7, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  nasikitika sana watu wengi bado mnafikiria kishule shule, Tanzania haiko hivyo. Kuna picha tofauti sana na ile ya ki-academia kuhusu siasa na maisha ya watanzania ya kila siku. Wapiga kura [walio wengi] wana factors zao za kumchagua mtu kwenye uongozi...kubwa kuliko zote ni pesa, kwamba amewapa ngapi kabla wao hawajampa fursa ya kwenda kufaidika huko mjengoni? Hivyo its lyk some kind of business where kila mmoja anataka kufaidika kivyake...wewe ukienda na misifa na mikakati yako endelevu, wao hawakuelewi kabisa, labda kama uwe na pesa za kuwapa pia! Na tutaendelea sana kupiga kelele kuhusu rushwa na ubadhilifu na upotevu wa uzalendo, mikataba ya ovyo n.k. lkn ukweli uko wazi - kama wapiga kura ili wakupe uongozi basi ni lazima walambe kwanza, wewe ukiingia huko utakuwa mzalendo kweli?

  Kura ziko directly proportion na pesa unazotoa...

  halafu hizi lugha za EPA, RICHMOND, RADA sijui madudu gani, kule kwenye grassroots ambako wapiga kura wapo wanajua mlidhulumiana tu ndo maana leo mnashindana, wao wanaamini kuwa kila mwanasiasa anafaidika sana na cheo alichonacho na ndo maana amekuja kuomba tena uongozi...hivyo nao wanakaa mkao wa kula tayari tayari!
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  message nzuri zaidi ni kuwa ufisadi,wizi,rushwa na kuwagawia kitu kidogo wapambe wako inalipa.
   
 13. P

  Pokola JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  :nod:Ni kwamba..,tusifikiri wananchi wa majimbo ya watu hao ni malaika... Mimi nawafahamu Wa.... wa kule rombo kwa mramba.. Wanapenda shekeli kuliko hata uhai wao!! Huwaambii ki2 mbele ya rupia meku!!!:disapointed:

  Kule Monduli pia nimeishi sana, pale mnadani siku ya j2 mheshimiwa huwa anabwaga ng'ombe hata 10 (ile jamii mbele ya nyama haimkumbuki hata muumba!!) Ukipandishia ile pombe ya kirong'oti ndo kura unalamba kwa kwenda mbele yeroo!! Unasahangaa?? Hehe, umechelewa.:bored:

  KIFUPI NI KUWA; GIVE 'EM FOOLS WHAT THEY WANT, U WILL KILL THEIR REASONING!! Tehe, tehe, tehe.... :love:
   
 14. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Oooh pole yake,inawezekana wananchi walikerwa kwa Karamagi kutozungumza kihaya kwao!!!
   
 15. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,544
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  watu wengi wanakuwa mavuvuzela tu . hamjui lowassa amefanya maendeleo gani jimboni monduli kwenye sekta zote . iwe ni maji , umeme , barabara ,elimu na afya . mi sijui mnaongea nini . Monduli ilikuwa nyuma kwenye maendeleo ya kila kitu. lowassa . lowassa ni mwanaume .
   
 16. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Dr. umeweka ukweli vizuri zaidi.... hakuna kingine si kwamba wananchi wanawapenda, bali wamenunua kura kwa bei nzuri.....It's sad lakini ndio reality ya tulipofikia...kazi tunayo , aluta continua!!!!
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii ya lowassa ni mwanaume ina utata kidogo. Ni sawa na kauli aliyotoa kiongozi mmoja mwanamke? au ina maana nyingine? Unajua kuwa watu wanaiba sana na wanatumia pesa walizoiba kujaribu kumhonga Mungu hata watu waliwaibia?
   
Loading...