Ushindani katika chaguzi zetu hauko balanced.

Ushindani katika chaguzi zetu hauko balanced.

Truths

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
1,494
Reaction score
1,504
Mbali na kasoro zilizozoeleka. Kulingana na maoni ya Zito wa ACT wazalendo. Na taathmini ya chama chake.

Kinachoonekana kwenye uwanja wa siasa ni ushindani usio na uwiano sawia

CCM amekua akishindana na vyama vingine katika uwiano usio na usawa kwa kiwango cha kukatisha tamaa.

CCM imetumia miaka miwili kuhubiri siasa na kujitangaza majukwaani huku ikipiga marufuku vyama vingine kujitangaza.

Na pale wapinzani walipojaribu waliishia kuswekwa ndani na wengine hata kupotezwa.
Haya ni kinyume na matarajio ya wengi kua upinzani umekua kufuatia matokeo ya mwaka 2015.

Hoja kua Serikali imetekeleza ahadi zake. Imejaa hadaa na usanii mwingi sana.

CCM imekua ikitoa kauli za kukatisha tamaa kwenye mikutano yao kua kuchagua upinzani hakutawasaidia kwakua wao ndio wenye Dola, ma director ni watu wao nk.

CCM imekua ikitumia vyombo vya serikali kuwaaminisha watu kua Hakuna msaada watakao upata kwa kuchagua Upinzani.

Leo hii wanajisifu kwa kurudisha maeneo ambayo Wapinzani walikua wameyateka.

Pamoja na mbinu hii ya kuzuia wapinzani kujitangaza. Wameahidi ushindi wanaouita wa Tsunami katika uchaguzi wa 2020

Wapinzani walishadhohofishwa kuanzia kwenye Media zote kama TV, Radio zote nchini na vitisho. Ambapo hawakutakiwa kusikika.

Utawala huu umeonesha wazi kua wapinzani ndio maadui wasiopaswa kuwepo.

Wanasiasa wa CCM watabaki kua watu wanafiki na ambao Ni Mungu tu anajua atawafanya nini..
 
Mwanzo nilikua mkosoaji mkubwa sana wa Chama cha mapinduzi, uozo ambao umekua unafanywa hauvumiliki kwa mtu mwenye akili timamu... Ila kwa mwenendo ule mke wangu akaniomba niache nitapotezwa maana hamna demokrasia Tanzania tunadanganyana tu...
Sasa hivi nimekua msomaji na msikilizaji ila inatia hasira saaaaaaana mpaka nahisi damu kuchemka ila ndo sitaki nimwache binti yangu mdogo akiwa hana baba
 
Yeah ni Kweli inakatisha Tamaa sana.

Pia Kwa unyang'anyi waliowafanyia cdm kwenye hizi chaguzi.

Pia nimegundua Zito anatumika na system kuwahadaa watanzania. Ila yule sio mpinzani.
Wenzake walishatangulia ndani ya Sisiemu siku nyingi. Na pia nimegundua kwanini hua hakamatwi anapotoa matamko yake.
 
Ukitaka punguza furaha yako na tabasamu lako ata miaka ya kuishi , jarbu kufatilia kampeni au chaguz za bongo.
 
Back
Top Bottom