AshaDii, heshima kwako.Sitaki hata fikiria the agony of reality..... Ni mbaya!
"Nyumba yangu sio mzinga wa nyuki unaingia na kutoka utakavyo."Dingi, uko sawa! Niliwahi pata hgeli, baada ya miezi 2 akawa kachangamka haswaa. Siku ya off yake ya jumapili akasema anaenda kwa dadake wapi sijui. Saa moja usiku ananipigia,'dada, samahani naomba nirudi kesho manake bado niko kwa dada na naona giza lishaingia'. Nilijibu kitu kimoja tu, ukilala kwa dada yako, kesho kabla ya saa mbili uwe umeshakuja kuchukua vitu vyako! Nyumba yangu sio mzinga wa nyuki unaingia na kutoka utakavyo. Tunapanga ratiba na tunazifuatilia kuzikeleza.
Huwa nashangaa sana watu wanaolala kwa 'watu' (sio wapenzi wao, ieleweke), ni kama kutoheshimu nyumba yako kama danguro!
"Nyumba yangu sio mzinga wa nyuki unaingia na kutoka utakavyo."
Hilo neno limenifanya nicheke.....................Mwanangu una visa wewe!
Kuna jambo ambalo pia sikulizungumza kwenye uzi huu, nalo ni hili la ma-house girl wetu, kuna baadhi yao ukitoka na mkeo au mumeo kwenda kazini, nao huigeuza nyumba kuwa danguro, utakuta wauza mchicha, wauza samaki na wenye kuuza bucha humalizia shida zao humo, ili dada aweze kupata discount ya bidhaa ili kupata cha juu kwa ajili ya kununulia skin jinzi.
mimi nimejikaza nikapanga ka nyumba kangu kana bedroom mbili kuna ndugu zangu watoto wa mauncle na mamamdogo wapo chuo wengine sijui wapo wapi wakaja wakataka kufanya makazi nikawatoa baruti,ningekubali tungekuwa 7 eti
nikawaambia kwangu sio hosteli
watu si wangeona ni danguro jamani?
daaah nyumba moja wasichana saba ukizingatia tunarudi usiku sometimes hadi saa kumi usiku watu wasingetuelewa nakwambiaOfcoz kama hakukuwa na sababu nzuri ya kuja kubanana nao hapo ulikuwa sahihi. Lakini danguro haina maana ya kuishi watu wengi sehemu moja. Danguro ni nyumba isiyo na nidhamu, at least machoni pa watu. Inahusika na umalaya na ubadilishaji wa wenza bila kujali.
Hahaha, kama visa ntakuwa nimerithi kwako!
Hgeli wangu ana clear instructions, hana ruhusa ya kupata mgeni bila clearance yangu, na ni lazima niwepo! Jumapili yote ni off day, na kama ana mgonjwa tunafanya utaratibu aende tena na ma-hotpot ya misosi kabisa!
My maid doesn't shop for me, no!! So hakuna mchuuzi anaeniletea kitu na kuna limit ya access ya nyumbani kwangu! Naenda sokoni mwenyewe sana akibahatisha chumvi iishe na nisijue ndo atanunua dukani!
Hayo maisha ya kama danguro ni sign ya disorganised life! Kuna dada alitelekezwa na celebrity flani, jamaa kaenda ng'ambo kamuacha na binti, sasa hivi she is in form 3 nadhani. Kila siku mama anarudi na 'uncle' na kumuambia mwanae 'muambie uncle asante, ndo kakulipia ada. Babako wala hajali, anauza jina tu!'. Nikikaangalia kale kabinti, nachoka manake lazma ataishia mulemule, kama ma-uncles hawatamuwahi! Sad indeed!
daaah nyumba moja wasichana saba ukizingatia tunarudi usiku sometimes hadi saa kumi usiku watu wasingetuelewa nakwambia