Ushawahi kuibiwa kitu chochote na mpenzi wako?

Nimeenda kwake, kanitumia afu kasema hana pesa atanitumia baadae kwenye simu.
Kaenda kuoga nikasepa na flat screen yake pamoja na dekoda ya Azam.
Namba yangu ya simu hana....atanipataje.
Mpaka leo ninavyo
Kuna taswira naiona kwako !
 
Mimi nilinyolewa mavuzi ambayo nahisi yalipelekwa kwa mganga ili nimuache mke wangu nioe mchepuko. Ilikuwa hivi, mchepuko kila mara baada ya kunizoea alikuwa ana katabia cha kunililia niende hotelini kulala naye usiku mzima na nikawa nakataa kwa sababu nilikuwa (na bado nina) mke na watoto), nikimkatalia analia kama kafiwa na wazazi wake. Nikaingiwa na huruma, kwa hiyo siku nyingine aliponiomba kulala naye hotelini sikusita nikamkubalia. Tukawa tumeenda kulala hoteli moja hivi kule Kigamboni. Tulifanya yetu kisha tukalala, nashangaa nahamka usiku nakwenda kujisaidia haja ndogo nakuta sina vuzi hata moja yaani kipara tupu kama tako la mtoto mchanga. Nikarudi kumuhamsha mwenzangu kwanini sina mavuzi, akaniambia aliyanyoa kunisaidia kuondoa uchafu. Nikashikwa na wasiwasi huku nikijiuliza siku zote hajawahi niambia mavuzi yangu ni uchafu na si mavuzi ya kutisha kama msitu maana niliyanyoa kimtindo iweje leo hii? Kumuuliza kayaweka wapi akanijibu kwa hasira kuwa nayatakia nini kitu kichafu kisochofaa? Kwa kweli sikulala vizuri ile siku, kufika asubuhi ikabidi nikatishe our outing. Kurudi nyumbani nikamuaga nakwenda kuangalia familia na sikumtafuta tena kama siku tatu hivi kwa sababu nilihisi alikuwa kanichezea rafu, hivyo nikawa najitazamia kwanza. Baada ya siku 4 kupita akanitumia ujumbe kuwa anakwenda kwao kijijini, Tanga, atarudi baada ya wiki na nisimtafute. Ile wiki ikawa mwezi hajarudi, nikimpigia simu hapokei nikaacha kwani bado nilikuwa na hasira naye. Siku ya siku nikakutana na shoga yake pale stesheni, nashangaa anakuja huku ananikumbatia na kulia akinipa pole kufiwa na mpenzi wangu. Kumuuliza kulikoni, akaniambia si mpenzi wangu alifia kwa mganga alipoenda kwao kijijini. Yaani niliishiwa nguvu na kuyakumbuka mavuzi yangu huenda ndiyo yalikuwa chanzo maana sie wengine tumekingwa toka utotoni.
khaaa
 
Mimi kuna demu aliwahi kuondoka na tshirt yangu moja na boxer zangu kama tatu hivi, wiki nzima najiuliza, huyu fala anataka kuniroga nini? Nilipata stress kama wiki moja hivi, ila baada ya kuona niko kamili gado, nikampotezea, na Ikawa ndio mara ya kwanza na ya mwisho kumtafuta, demu mwenyewe ni kisu ila kapitia mahusiano mengi hadi unajiuliza kwa nini wana wanakimbia!
*** ndio ilikuwa siku ya kwanza kuja kwangu***
 
Mimi kuna demu aliwahi kuondoka na tshirt yangu moja na boxer zangu kama tatu hivi, wiki nzima najiuliza, huyu fala anataka kuniroga nini? Nilipata stress kama wiki moja hivi, ila baada ya kuona niko kamili gado, nikampotezea, na Ikawa ndio mara ya kwanza na ya mwisho kumtafuta, demu mwenyewe ni kisu ila kapitia mahusiano mengi hadi unajiuliza kwa nini wana wanakimbia!
*** ndio ilikuwa siku ya kwanza kuja kwangu***
Chaudokozi huyoo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom