Ushawahi kufananishwa!!?

Muuza simu used

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
4,393
Reaction score
7,108
Kama ilivyo ni kawaida mtu na mtu kufanana na hali hiyo inaweza kukutokea popote na siku yoyote!je ni faida zipi au hasara zipi ulizowahi kuzipata kwa kufananishwa na mtu Fulani?kuna watu walishawahi kufananishwa na mwizi!

Unaweza ukapokea kipigo cha mbwa koko wakati wewe sio muhusika.
Pia unaweza kufananishwa na mtu Fulani maarufu etc
Kuna kisa kimoja ambacho kiliwahi kunistua sana ni kwamba nilishawahi kwenda kwenye restaurant moja hivi kupata msosi,muhudumu alikuwa na mama mmoja wa makamo Fulani hivi baada ya kunipokea pale kabla ya kuniuliza nilikuwa nahitaji chakula gani aliniangalia sana kisha akaanza kulia sana tena kwa sauti ya juu!
Nilishangaa sana nisijue kulikoni!baada ya muda alivyotulia akajikaza akaniambia nafanana sana na mtoto wake wa kiume ambae alikuwa amepoteza maisha siku chache zilizopita!.
Hakika nilishangaa sana na nikajihisi nimekosa Amani na huzuni iliniingia.

Je?wewe ulishawahi kufananishwa na nani na kipi kilikukumba kiwe ni negative ama positive?


Sent by Diaspora
 
mademu wengi ndio hujifanya wananifananisha na mwishowe naishia kuwatafuna
 
Hahahaa nakumbuka Siku moja Huyo mmama kanikumbatia yuko za Sikh subi nikawa namuangalia tu sielewi Hata kinacho endelea akaniuliza were so mtoto wa kambuje nikamwambia hapana kabak mdogo gaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaa nakumbuka Siku moja Huyo mmama kanikumbatia yuko za Sikh subi nikawa namuangalia tu sielewi Hata kinacho endelea akaniuliza were so mtoto wa kambuje nikamwambia hapana kabak mdogo gaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maeneo ya mbagala kuu,nimejibanza sehem kando ya barabara kutokana na adha ya mvua,nimevalia kapelo nyeusi,fulana nyeupe,suruali nyeusi na raba nyeupe,ilikuja Prado ikafunga breki za haja,MTU aliyekuwa pembeni ya dereva akanyoosha mkono na kunipa bahasha ya khaki,kisa gari ikaamsha kwa speed za ajabu kama unavyojua hekaheka za hili jiji.
Ilikuwa bahasha ya haja,GOD is able,toka siku hiyo sijakosa kwenda kanisani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah hyo hadi kero tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah.....siku ukipata wasaa nenda Uchina au Ujapani,,,,,,,πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Jamani huwa nahisi mkosi kila sehemu ngeni niendayo lazima nipambane na kisanga cha kufananishwa, nilikuwa chuo kuna mkaka wa kimang'ati kiukweli tulifanana mwenyew nilikili nikimtizama najiona sura yangu, siku moja natembea barabarani nasikia mtu akiniita ananikimbilia kwa nyuma Fulani kaita sana aliponikalibia nikageuka alipigwa butwaa akadai nafanana sana na mshikaji wake huyo wa chuo na hivi majuzi tu nimefananishwa na aslya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me Juzi tu kuna jamaa Napita nkashangaa ananichekeaa tabasamu Kama lotee hivii nkaonaa ngoja nimsalimieee duuh akavua na Kofiaa akasema daah dogoo miaka mingii sanaaa...!! Ebuu niangaliee vipi hunikumbukii!??? wewe si mtoto wa mzee Fulani nkamwambia sioo akasema Kuna jamaa Mrangi ni mtoto wa mwanajeshi mnafanana sanaa yanii daah... Nkamwambia me Mchagaaa akasemaa daah poaa mzee ilaa Yulee atakuwa pachaa wakooo....haaa ha ha nkasepaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…