Moyo ndicho kiungo pekee mungu amekipa kazi ya kupenda na kuchukia, hivyo moyo ndio chombo pekee kinachohifadhi upendo na chuki....kuna aina mbalimbali za upendo na chuki...... Kumpenda mtu na kumchukia mtu hautokei tu bila sababu..kuna sababu ambazo mtu humfanya mtu kumchukia au kumpenda mtu fulani....... Unaweza kumchkia mtu kwa vile huyo mtu amefanana sura na mtu ambae alishawahi kukufanyia ubaya basi unaweza kumchukia mtu huyo...hiyo ni moja ya sababu.
Vilevile mungu amewaumba wanadamu tofauti na mfanano ndani ya mioyo yao.....unaweza ukakutana na mtu kwa mara ya kwanza wote mkajikuta mnapendana hapo inaonesha mfanano wa mioyo yenu pia unaweza ukakutana na mtu kwa mara ya kwanza wote mkajikuta kuna uzito flani ndani ya moyo wa kila mmoja juu ya mwanzake hapo kunautofauti mkubwa wa mioyo yenu hivyo mnajikuta mnachukiana tu bila sababu.
Vilevile namna mtu anavyojiweka na anavyochukuliwa na mwenzake hufanya kujenga chuki ndani ya moyo mfano: mtu kupenda usharobaro uliopitiliza,nyodo, dharau na kujiona,ukali vyote hivyo hufanya moyo kumchukia mtu.